Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Mungu yupo clear atleast kwenye Dini yetu hajaumba Binadamu na Majini isipokua wamuabudu itakua intimidation kama Mungu anacompete na mtu,
Intimidation haiitaji competition ili iwe intimidation: to frighten or threaten someone, usually in order to persuade the person to do something he or she does not wish to do:
hapa kakuumba wewe na anaweza akakufanya chochote unaweza ukaabudu vile vile asikupe hizo benefit anakumiliki asilimia 100.
Naam kwahio hata wale slave traders walikuwa na traits au walifanya kile ambacho God qualities...,
Again unatumia Akili ya kibinadamu, Divine power its beyond our comprehension, umekuwa coded uwe na free will unachagua unachofanya unaweza ukashukuru ama kukufuru, ila ukishukuru Mungu anajua Outcome na ukikufuru pia Mungu anajua Outcome. Thats part ya power za Uungu.
And whichever I do it is written ? Kwahio siwezi kubadilisha lolote, ni kama naangalia mkanda recorded na hapa ninarewind mara ya pili chochote nachofanya leo au jana is just waste of time au kukamilisha the written word ?
Na ndio Mungu ameumba na kuweka vyote hivyo Ukimwi, Slavery, Gharika etc, na kila tabu unayopata utakuwa compensated vyote hivyo vimeweka kama Test kwa mwanadamu.
Test wakati anajua kila kitu na kimeandikwa na wino umeshakauka ? Hio sio test labda sema kukamilisha kile alichoandika / kudhamiria na kila kiumbe ni character ana-play part wengine wapo doomed no matter what.. Au nimekosea wapi ?
Pia naona mkuu unachanganya Sana Doctorine ya Ukristo na Uisilamu, mimi muisilamu kama ulivyosema juu vyema tutumie logic ya ninachokiamini. Kwenye Uisilamu Mungu haishii tu kama All loving, Unaweza pitia online Majina 99 ya Mwenyez Mungu according to Uisilamu Mungu ni Destroyer, Avenger, Just etc.
Okay hapo nimekuelewa sasa hapo kwenye Avenger ana avenge nini wakati wote ni characters kwenye a written word ambayo wino umeshakauka huwezi ukafutika if we are all characters and we are playing our parts huwezi ukapata hero without a villain
Kabla ya Mtume Muhammad imani yetu ni kwamba Adhabu ilikuwa ikitoka papo hapo, wa Sodoma, Gharika, Upepo, etc hao wa Nuhu tayari walishamtimiza miaka yao duniani, hivyo iliandikwa kwenye lifespan yao baada ya miaka hio 1000 uma wao utaisha kwa Gharika.
kwenye huu muendelezo wa maandiko uliandikwa at once au episode baada ya episode yaani alitengeneza shetani ili aasi ili Adam akija shetani amdanganye ili apewe adhabu ? au episode ikiisha inaandikwa nyingine kulingana na iliyoisha ?

Pili babu zetu waliokuwa na miungu yao wenyewe hawakupata hizi memo au shetani aliwapa wrong version of the truth..., sababu wakati kina Daud wanafanya yao Mizimu ya Mababu zetu na kwa imani zao walikuwa wanafanya yao huku.... (Na je watahukumiwa au wao ni poa tu sababu hawakujua hence wanapata free Pass)?
 
Imagine umeweza kufanya identification ya mawazo yangu bila kile kifaa chako.😂 Simple proof kwamba yanaexist beyond the five senses.
Kwahio unaamini watu wanaojiita mind readers ?

Huyu jamaa amesema mawazo yako baada ya wewe kuyacommunicate yalivyokuwa kichwani mwako hakuweza kujua kama ulikuwa unapanga kuiba au kufanya nini..., ila sehemu za ubongo zinafanya kazi continously and the mind wanders (ingawa kuna wale wanaopractice meditation watakwambia wanaweza kuufanya ubongo wao ukawa calm na ku-clear all thoughts without any activity (anyway that's their claim....)
 
Mbona unazunguka wewe mwenyewe pale mwishoni umesema hata kama hakitayajua mawazo specifically bado sio ushahidi wa kuwepo vitu beyond the physical world
Wewe ni Mkristo je unaamini Madhehebu mengine / dini nyingine kwamba zipo sahihi ?

Kama jibu ni Hapana nini kilikufanya usiziamini ?, Si ni hata kama sio physial world si zitakuwepo !!!! Hence in your logic basi ni za kweli !!!
 
Mvutano wa kihisia unanogesha maisha. Hatuwezi kuwa kama maroboti ndo mana tumepewa kitu cha kutufanya tuwe na mabadiliko ya kihisia. leo una furaha kesho unanuna leo uko peace na mtu kesho mnagombana ilimradi tu maisha yasonge.
Kwahio huko mbinguni ambapo tumeambiwa hatuwezi kuasi tena na wadau humu ndani tutakuwa kama ma-robot ?
Favoritism ni kitu ambacho Mungu ametaka kiwepo ndo mana hata wewe ukija kuwa na watoto kuna mmoja utampenda sana kuliko wote.
Kwahio chochote alichotaka kiwepo ni kizuri ?, Pili sijasema kipo au hakipo nimesema yeye pia anacho ? Kuwa na favoritism ni weakness ya kibinadamu (naam weakness na sio strength) kwahio Mungu na yeye anayo hii, alafu kumbuka wewe ukiwa na watoto hauwezi kujua outcome au characteristics za hao watoto baadae, ila yeye aliyeumba tunaambiwa alijua hata kabla hajaumba (kwahio aliumba huyu ili ampende zaidi kuliko yule)?
 
Ushajuliza kwa nini Solar system haijawahi kuwa na makosa yoyote miaka billions of years?

Unajua impact ya dunia hii kusimama kwa sekunde tu nini kitatokea?
Unamaanisha nini kuhusu makosa ? like anything solar system ipo powered na sun / jua...,(like any other stars) lipo powered na hydrogen na tunaweza kuestimate ni miaka mingapi hio nishati itakwisha na ikiisha inajulikana what will happen...

Sasa sijui hili linanielewesha vipi kwenye mjadala at hand ?
 
Kwahiyo sasa hivi unakubali mawazo yanaexist in their own form beyond the five senses?
Mkuu sijui unataka kuonyesha nini kwamba kitu haki-exist mpaka ukione ? au ukikiona ndio kina-exist au sababu haujakiona na unaweza usikuone na kina-exist hivyo kila kitu kina-exist ?

Yaani huu mvutano sioni unaongeza nini kwenye mtiririko wa maandishi yako labda naomba unieleweshe !!!
 
Pia kumbuka kuna Miungi wengine ambao wana nguvu na wanatenda miujiza pia kwa wawaaminio...refer kwa Nabii Elia alivyotaka kuwaaminisha watu ni Mungu yupo anastqhili kuabudiwa.

So Ulimwengu umeubwa kwa sheria ambazo mwanadamu ni vigumu mno kuiIjua zote.
Kwanini niende mbali hizi ni Imani hata mababu zetu walikuwa na imani zao kabla ya watu kuja kuwaambia ni Imani za Kishenzi chukueni hizi doctrines za waarabu na wayahudi...

Kule America wazazi walinyanganywa watoto wao na kupelekwa kwenye mashule kuwa indoctrinated na kufanyiwa cleansing ya kuwaondoa upuuzi (all in the name of God) nadhani hapo neno free will liliwapita kando.....
 
Mungu ametupa Sign za uwepo wake, kutokana na Kitabu changu ninachokiamini. Pia kuna Tafiti mbalimbali zinazokazia.

Anasema Mtume wetu Muhammad (S.A.W) kwamba watu wote wamezaliwa katika Natural state ya kumuamini mungu ila ni Society ndio zinawafundisha vyengine ie Atheist, hili linatiliwa mkazo na tafiti mbalimbali duniani
Kwamba hao Atheist hawakuzaliwa au Society haikuzaliwa au ni nini chanzo cha kuwabadilisha hao watoto kama from inception and second zero kila mtu aliamini ?
1. Utafiti wa Innate Religion.
Kila mtoto anaezaliwa anaamini kuhusu Supernatural being, watoto wote wanakuwa na Dini asili ya kuamini mungu na Atheism inafundishwa.

Utafiti huu umefanywa Oxford University, Researcher 57 wamehusika maeneo tofauti 40 katika nchi 20 sehemu zote zenye dini na wasio na dini na zote zime conclude watoto wanazaliwa wakiamini Mungu na maisha baada ya Dunia

Kuamini A, Mwingine akaamini B Mwingine akaamini C na Wengine kina babu zetu walioambiwa ni wapuuzi wakiamini mizimu yao na wakati wewe unajua muumba ni mmoja conclusively inaonyesha zote haziwezi zikawa kweli kwamba at most kwenye mfano wangu hapo juu 75% ni uongo..

Pili argumentum ad populum.., Hata kipindi ulimwengu mzima wanaona kwamba kuwatumikisha wenzao kama watumwa ni sahihi (hata vitabu havijawahi kupinga) haimaanishi ilikuwa sahihi
2. Tunamuogopa mungu hata kama akili zetu haziamini.

Utafiti mwengine very interesting even Atheist ambao hawaamini mungu miili yao ina wa betray, walichukuliwa Atheist 13 wakapewa maneno ya mabaya dhidi ya Mungu japo akili zao zipo sawa Ngozi zao zilikuwa zinaonesha uoga.


Ulifanya University of Helsinki Finland.
Kwamba nikiambiwa kuna zimwi mla watu nje alafu nisiamini nikapelekwa nje nikaogopa kwamba automatically hilo zimwi lipo ?!!!

Hivi hapa proof yako ni kwamba sababu mfano Atheist ni waongo au labda wanafiki kwahio the opposite ya wanachosema ndio ukweli ?
We examined whether atheists exhibit evidence of emotional arousal when they dare God to cause harm to themselves and their intimates. In Study 1, the participants (16 atheists, 13 religious individuals) read aloud 36 statements of three different types: God, offensive, and neutral. In Study 2 (N = 19 atheists), 10 new stimulus statements were included in which atheists wished for negative events to occur. The atheists did not think the God statements were as unpleasant as the religious participants did in their verbal reports. However, the skin conductance level showed that asking God to do awful things was equally stressful to atheists as it was to religious people and that atheists were more affected by God statements than by wish or offensive statements. The results imply that atheists' attitudes toward God are ambivalent in that their explicit beliefs conflict with their affective response

So mkuu Kumuamini Mungu ni natural miili yetu ipo programmed kuamini hilo na dalili zipo wazi.
Duh kwahio huoni kwamba huenda hayo maneno mabaya (offensive waliyopewa kuyasema ndio yaliwafanya wafanye walichofanya) najua kabisa jirani yangu hawezi kunifanya kitu ila haimaanishi nitafutahia au kutokusita kumshushia matusi (Kuwa Atheist does not mean you are a bad person) Ingawa that is an argument for another day I believe Human Beings are not Good People....
 
Tofautisha uthibitisho na Sign, hakuna uthibitisho physically mpaka siku ya kiama, ila zipo sign kibao. Moja wapo ni hio. So kama unaamini ama huamini hizo sign its up to you hulazimishwi ila wengine tunaamini.
Kama zile sign walizokuwa wanaamini watu kwamba solar eclipse ni sign kutoka kwa muumba mpaka walipo-know better ? Au unajuaje kama hizi signs now are real tofauti na wale waliodhani then ?
 
Binadamu ni kiumbe wa mwisho kabisa kuumbwa na Mungu. Kabla ya mwanadamu kuletwa kuishi katika dunia hii walikuwapo majini wakiishi na wao ndio walikuwa watawala, ila walikuja kufanya ufisadi mkubwa na umwagaji wa damu.Mungu alituma jeshi la malaika kuja kuwapiga vita na wengi walikimbilia mapangoni,misituni,majangwani ,baharini na kwenye visiwa. Mungu ndipo aliamua kuumba kiumbe mpya kuja kuwa mtawala/kiongozi katika dunia hii nae si mwingine bali ni mwanadamu. Malaika walistaajabu sana kwanini Mungu anataka kuumba kiumbe mwingine aje kuwa mtawala ardhini wakati majini walishafanya ufisadi na umwagaji wa damu mkubwa.? Mungu aliwajibu kuwa anayajua yale wasiyoyajua.So watulie waone ufundi wake.


Nikijibu swali lako ni kuwa Kifo kililuwapo kabla ya Adam na Mungu alitangulia kuumba Pepo na Moto kabla ya kutuumba . Ilikuwa ikijulikana kuwa kuna siku ya mwisho (Qiyama) ila hakuna anayejua itakuwa lini.
Kwahio aliumba pepo na moto ili aje achome wakosefu, akaumba malaika ambao alikua watakuja kuwa mashetani ili akimweka binadamu waweze kumlaghai ili aweze kuchoma wengi zaidi na wengine akawaumba vizuri ili wao wafaidike baadae ?

Am I following you Correctly ?
 
Kwahio aliumba pepo na moto ili aje achome wakosefu, akaumba malaika ambao alikua watakuja kuwa mashetani ili akimweka binadamu waweze kumlaghai ili aweze kuchoma wengi zaidi na wengine akawaumba vizuri ili wao wafaidike baadae ?

Am I following you Correctly ?
Malaika sio mashetani...ushetani ni sifa ya kiumbe muasi kwa Mungu.

Malaika wao wameumbwa wakiwa hawana hiyari, wanatenda yale waliyoamrishwa.

Binadamu na Majini wao wana hiyari ya kufanya mema au kufanya maovu ila ndio kumewekwa mafikio ya machaguo yetu...kuwa kuna pepo kwa ajili ya walioamini na kutenda mema na kuna moto kwa ajili ya waliokadhibisha.

Nafsi zimeshaumbwa kabla ya kuletwa hapa ulimwenguni na Mungu alishazibainishia njia ya kweli ni ipi na akazionya pia juu ya upotovu. Wote mimi na ww tumekiri kuwa hapana mola isipokuwa Mungu mmoja , baada ya hapo Mungu ndio anatupa mtihani kwa kutuleta humu duniani katika vipindi tofauti...kuna waliotangulia miaka mingi iliyopita nasi tumefuatia ,tutakufa na wataendelea kuja wengine mpk pale ulimwengu utakapofika tamati kisha tutakwenda kulipwa kwa yale tuliyoyatenda katika siku ya hukumu.

Mungu hapangiwi wala haulizwi kwanini kaumba Moto na Pepo....bali sisi viumbe ndio tugakaokwenda kuulizwa. Mungu ni mfalme na anamiliki kila kitu, unapata wapi authority ya kuhoji God's will?
 
Kuamini creator ni step ya kwanza it doesnt matter huyo creator ni nani hayo mambo ya Uisilamu ama ukristo ama Uhindu etc yanafuatia baadae, ukienda moja kwa moja kwenye dini unakuwa umeruka step.

Pia huo utafiti nilioweka unaongelea Exactly unachojadili hapa, watoto hawaamini mungu sababu ya Msikiti ama Kanisa, wanaamini mungu sababu wamezaliwa hivyo
Nilikuuliza swali hapo awali huenda ushajibu sababu post ni nyingi na ninasoma polepole post baada ya post...

Kama ukitaka au kwa nguvu zako ukijaribu ku-create nothingness ambayo sidhani kama ina-exist kwenye test tube ndogo tu..., ukaondoa kila kitu ambacho sasa wewe unadhani kwamba hakuna kitu tena..., Je hakuna uwezekano wa kukuta mold au viumbe fulani ndani ya hio tube na kutokana na mazingira tofauti na happenstances tofauti test tube hizo ukichukua ukazipeleka sehemu mbalimbali unadhani zitakuwa sawa baada ya muda...

Je bila mkono wako au wa mtu / kitu chochote hatuwezi kupata life form baada ya muda na hio life form ikipatikana ni wewe ndio utakuwa creator ?

Kuwepo kwa hizi unknown busara ni kuendelea kuumiza vichwa na kuhoji / kuchunguza ili kupata proof sio kunyanyua mikono kwamba haa sababu hatujui huyu atakuwa creator na ngoja tutumie kitabu hiki au kile ambacho walikitumia watu ambao probably the did not know better at the time kama muongozo wetu...

As a Society tutakuwa hatuwatendei Haki the coming generations....
 
Kwahio aliumba pepo na moto ili aje achome wakosefu, akaumba malaika ambao alikua watakuja kuwa mashetani ili akimweka binadamu waweze kumlaghai ili aweze kuchoma wengi zaidi na wengine akawaumba vizuri ili wao wafaidike baadae ?

Am I following you Correctly ?
Shetani yeye alishapewa mtihani wake wa kumsujudia Adam mara baada ya kushindwa katika suala la elimu ,ila akachagua tu kugoma kutokana na jeuri na kiburi.

Alijiona kuwa yeye ni bora kutokana na kuumbwa kwa moto na Adam aliumbwa kwa udongo. Iblis alikuwepo pindi Adam anaumbwa na alikuwa anauona uumbwaji wa Adam toka mwanzo mpaka anapuliziwa Roho kuwa kiumbe kamili ...so alikuwa na ego why ampe heshima kiumbe kipya ambacho kimeumbwa kwa material dhalili kama udongo??

Baada ya kumgomea Mungu ndipo alipolaaniwa, ila badala ya kuomba Msamaha na kujutia makosa yake, aliamua kumuomba Mungu amjaalie uhai mrefu, ombi lake alikubaliwa.

Ndipo akachukua kiapo kuwa atahakikisha anaupoteza uzao wote wa Adam na kuhakikisha kuwa anazoa kundi kubwa la kuingia nalo Motoni.
 
Nafsi zimeshaumbwa kabla ya kuletwa hapa ulimwenguni na Mungu alishazibainishia njia ya kweli ni ipi na akazionya pia juu ya upotovu. Wote mimi na ww tumekiri kuwa hapana mola isipokuwa Mungu mmoja ,
Mbona hii mimi sikumbuki na wewe ndio unakumbuka ?, Huoni kwamba ni uonevu kunihukumu mimi bila kunipa kumbukumbu ya mimi kukumbuka kukubaliana na huu mkataba
baada ya hapo Mungu ndio anatupa mtihani kwa kutuleta humu duniani
Kwahio ningekataa kukubali na hilo hapo juu nisingeletwa duniani Au? na wale wanaokufa siku ya kwanza wakizaliwa huoni kwamba mtihani wao ni rahisi ?
katika vipindi tofauti...kuna waliotangulia miaka mingi iliyopita nasi tumefuatia ,tutakufa na wataendelea kuja wengine mpk pale ulimwengu utakapofika tamati kisha tutakwenda kulipwa kwa yale tuliyoyatenda katika siku ya hukumu.
Mababu zetu walioabudu mizimu na wao walipewa huu mtihani wakasahau au ?
Mungu hapangiwi wala haulizwi kwanini kaumba Moto na Pepo....bali sisi viumbe ndio tugakaokwenda kuulizwa. Mungu ni mfalme na anamiliki kila kitu, unapata wapi authority ya kuhoji God's will?
Tusingehoji wala mababu zetu wasingehoji huenda mpaka leo sisi tungekuwa watumwa sababu tu ya ngozi ya babu yangu au sababu ya kuzaliwa na jina fulani...
 
achana na shetani, tuanze na wewe kwanini usimalize tofauti yako na Mungu..?
Mungu yupi wa Mababu zangu wa Israel wa Waarabu au Yupi ?

Na je mtenda mema asiyeamini unachoamini wewe na mnafiki anayeamini kama wewe kwa Imani yako ni nani atauona ufalme wa huyo Mungu wako ?
 
Mungu yupi wa Mababu zangu wa Israel wa Waarabu au Yupi ?

Na je mtenda mema asiyeamini unachoamini wewe na mnafiki anayeamini kama wewe kwa Imani yako ni nani atauona ufalme wa huyo Mungu wako ?
twende taratibu, swali weka moja moja, ukienda haraka huto elewa.

Mungu ninaemzungumzia mimi ni Mungu aliye baba wa roho zetu.. muumba wa ulimwengu.

Matendo ya Mitume 17:24-28
[24]Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
[25]wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.
[26]Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;
[27]ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.
[28]Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu.
 
Kwahio huko mbinguni ambapo tumeambiwa hatuwezi kuasi tena na wadau humu ndani tutakuwa kama ma-robot ?

Kwahio chochote alichotaka kiwepo ni kizuri ?, Pili sijasema kipo au hakipo nimesema yeye pia anacho ? Kuwa na favoritism ni weakness ya kibinadamu (naam weakness na sio strength) kwahio Mungu na yeye anayo hii, alafu kumbuka wewe ukiwa na watoto hauwezi kujua outcome au characteristics za hao watoto baadae, ila yeye aliyeumba tunaambiwa alijua hata kabla hajaumba (kwahio aliumba huyu ili ampende zaidi kuliko yule)?
Unajua kama biblia inasema ufalme wa mungu upo ndani yako?
 
Mbona hii mimi sikumbuki na wewe ndio unakumbuka ?, Huoni kwamba ni uonevu kunihukumu mimi bila kunipa kumbukumbu ya mimi kukumbuka kukubaliana na huu mkataba

Kwahio ningekataa kukubali na hilo hapo juu nisingeletwa duniani Au? na wale wanaokufa siku ya kwanza wakizaliwa huoni kwamba mtihani wao ni rahisi ?

Mababu zetu walioabudu mizimu na wao walipewa huu mtihani wakasahau au ?

Tusingehoji wala mababu zetu wasingehoji huenda mpaka leo sisi tungekuwa watumwa sababu tu ya ngozi ya babu yangu au sababu ya kuzaliwa na jina fulani...
Huna excuse....Jua kuwa tupo hapa duniani kwa ajili ya mtihani.

Maisha yetu yapo katika mfumo huu!!

Mungu kwa hekima,utashi na mapenzi yale aliamua kutuumba ili atufanyie mtihani! Viumbe vyote vilihudhurishwa mbele yake, akauliza nani yupo tayari kufanyiwa huu mtihani wa kupewa amana!! ?

Jua,milima,wanyama,bahari,malaika,mwezi,mbingu,nyota,miti na ardhi vyote vilikataa kuibeba hiyo amana badala yake mwanadamu alikubali kubeba hiyo amana.

Amana yenyewe ni hii kuwa atafanya aliyoamrishwa na ataacha aliyokatazwa kwa maana ya kuwa mtiifu. Viumbe wengine waliogopa kubeba kutokana na uzito wa suala hili ila mwanadamu ali underestimate uzito wa jambo hili akabeba majukumu. Ila aliambiwa kuwa akifaulu kutekeleza hayo atalipwa malipo makubwa ambayo ni Pepo na akishindwa basi ataadhibiwa kwa moto.

Viumbe vingine vilistaajabu kuona kiumbe dhaifu kama binadamu kukubali kubeba mzigo mzito.

Mwandamu yeye alichagua hiyari hivyo viumbe vingine havina hiyari ya kutenda kama mwanadamu.

Nafsi inapoletwa duniani huwa ineletwa kwa ajili ya mtihani hivyo ili kuwe na fair test kila nafsi huanza ikiwa haina kitu kichwani!! Ila humu duniani Mungu tayari ameshatanguliza kuweka uongofu kupitia vitabu vyake vitukufu,mitume na manabii (wa kweli).

Hivyo ni jukumu lako mwanadamu kuutafuta ukweli kama vile unavyohangaika kila siku kuutafuta mkate wako.

Mtihani huu una muda maalumu kwa kila mtahiniwa kuna ambao wamepewa muda mrefu na wengine mfupi. Mtoto toka anapozaliwa mpk kufikia baleghe huwa hana dhambi! Ila kalamu inaanza kuandika mema na mabaya yake mara baada tu ya kuwa ameshabaleghe kwa maana sasa anaelewa lipi jema na lipi ovu.
 
Back
Top Bottom