Did I say that ?!!!Kama huamini universe imetokea kwa Chance ina maana kuna Designer na kama kuna Designer mtaje ama Explain zaidi.
Nina uhakika tungejua kuonge kama kina simba, au Virus au Bacteria na wenyewe kama wana Bible yao wangesema haya haya kwamba Mungu katupenda sasa sisi bacteria hadi katupa uweze wa ku-regenerate kwa kasi sana...Chochote anacho kifanya Mungu ni chema. Ingawa kwa macho yetu ya nyama tunaweza kulaumu hapa na pale.
Mwanadamu ndiyo kiumbe pekee aliye pendwa sana na Mungu hadi akamuumba kwa mfano wake na kumpatika kila hitaji lake.
Nice explanation according to your faith...Swali lako ni fikirishi! Ngoja nijaribu hivi.
Kwenye spritual life, Kuna timing mkuu.Hata wewe ukifa kabla hujatubu dhambi zako,hauna tena chance ya ku-negotiate(japo kuna baadhi ya dini zinasema inawezekana kumuombea marehemu toba,sijui maandiko wanayotumia).Ila kwa jinsi ya maandiko matakatifu (biblia takatifu) usipoweza kutengeneza mahusiano yako na Mungu ungali hai,hakuna chance tena ya kufanya hivyo mara baada ya kufa . So it is too late kwa Shetani kuomba toba.kitendo cha shetani kufukuzwa,ilikuwa ni spritual death kwa shetani.Ndiyo maana anachosubiri ni hukumu tuu.
Pia tukumbuke kwamba Mungu na Shetani hizi ni Kingdom mbili tofauti zenye mamlaka kamili(Ijapokuwa Mungu ni mkuu) bado shetani anweza fanya copies ya mambo ya Mungu kudanganya watu.Again,fahamu mpaka sasa Shetani mwenyewe anajiona hana kile cha kumfanya aombe msamaha kwa sababu ana mamlaka kiasi anaona mambo yake yako on-track na pia ana watu wafuasi kibao nyuma yake.So akiweka chini siraha watu wake watabaki wapi by now? ikiwa tuu kuiunganisha simba na yanga kuwa yanga ni ngumu kuliko hili,au angalia kinachoendelea sasa Urusi na Ukrane kama haiko rahisi kwa ukrane kuachia nchi si zaidi sana kwa shetani?.Au ulikuwa unamanisha Mungu aseme sawa bwana shetani,mimi nimeamua kuwa chini yako sasa?
Mwisho kabisa,Mungu ametoa uhuru wa kuchagua unachoona kinafaa,ila ametoa angalizo juu ya mwisho wa kila njia utakayoamua kuiendea.
Ubarikiwe
Okay ni sawa kwa Imani yako ila kuna wanaosema / amini kwamba huyu Shetani alikuwa pia Malaika ila hao ni wao, twende na wewe...Malaika sio mashetani...ushetani ni sifa ya kiumbe muasi kwa Mungu.
Malaika wao wameumbwa wakiwa hawana hiyari, wanatenda yale waliyoamrishwa.
okay... ila nina swali hivi unaweza kwenda mbinguni kwa kutenda mema bila kuamini au inabidi uamini pia ? Kama inabidi uamini pia kuna swali hapo chini........Binadamu na Majini wao wana hiyari ya kufanya mema au kufanya maovu ila ndio kumewekwa mafikio ya machaguo yetu...kuwa kuna pepo kwa ajili ya walioamini na kutenda mema na kuna moto kwa ajili ya waliokadhibisha.
Sasa wale wanaomanini vinginevyo walipata amnesia au wasiokumbuka imekuwaje na Je wanaokufa siku ya kuzaliwa huoni ni kama mtihani huu wamefanya cheating ? (Free Pass to HEAVEN) ?Nafsi zimeshaumbwa kabla ya kuletwa hapa ulimwenguni na Mungu alishazibainishia njia ya kweli ni ipi na akazionya pia juu ya upotovu. Wote mimi na ww tumekiri kuwa hapana mola isipokuwa Mungu mmoja , baada ya hapo Mungu ndio anatupa mtihani kwa kutuleta humu duniani katika vipindi tofauti...
Ngoja kidogo..., hizi habari wewe kuja kuzipata vema na haya mafundisho yalikuwa kabla au baada ya Mtume Muhammad kuja na kuelezea ?!!! Sasa wale waliokuja kabla walijua vipi au waliambiwa na nani kuhusu mapato tuliyoambiwa na Mungu ? (Yaani walijua vipi mafundisho ya Mtume ambaye alikuwa bado hajaja)?kuna waliotangulia miaka mingi iliyopita nasi tumefuatia ,tutakufa na wataendelea kuja wengine mpk pale ulimwengu utakapofika tamati kisha tutakwenda kulipwa kwa yale tuliyoyatenda katika siku ya hukumu.
Mababu zetu wasingehoji walichoambiwa huenda mpaka leo kungekuwa kuna mabwana na sisi watwana kazi yetu ni kuwalamba miguu...Mungu hapangiwi wala haulizwi kwanini kaumba Moto na Pepo....bali sisi viumbe ndio tugakaokwenda kuulizwa. Mungu ni mfalme na anamiliki kila kitu, unapata wapi authority ya kuhoji God's will?
Na unataka unachoamini wewe kwamba ndio kiwe universal ? Nimekuuliza swali mtenda mema asiyemuamini unayemuamini wewe atakwenda au hataenda mbinguni.., yaani kutokumuani tu unayemuamini ni guarantee ya kuwa doomed ?twende taratibu, swali weka moja moja, ukienda haraka huto elewa.
Mungu ninaemzungumzia mimi ni Mungu aliye baba wa roho zetu.. muumba wa ulimwengu.
Matendo ya Mitume 17:24-28
[24]Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
[25]wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.
[26]Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;
[27]ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.
[28]Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu.
Okay who am I to argue with your faith........Huna excuse....Jua kuwa tupo hapa duniani kwa ajili ya mtihani.
Maisha yetu yapo katika mfumo huu!!
Mungu kwa hekima,utashi na mapenzi yale aliamua kutuumba ili atufanyie mtihani! Viumbe vyote vilihudhurishwa mbele yake, akauliza nani yupo tayari kufanyiwa huu mtihani wa kupewa amana!! ?
Jua,milima,wanyama,bahari,malaika,mwezi,mbingu,nyota,miti na ardhi vyote vilikataa kuibeba hiyo amana badala yake mwanadamu alikubali kubeba hiyo amana.
Amana yenyewe ni hii kuwa atafanya aliyoamrishwa na ataacha aliyokatazwa kwa maana ya kuwa mtiifu. Viumbe wengine waliogopa kubeba kutokana na uzito wa suala hili ila mwanadamu ali underestimate uzito wa jambo hili akabeba majukumu. Ila aliambiwa kuwa akifaulu kutekeleza hayo atalipwa malipo makubwa ambayo ni Pepo na akishindwa basi ataadhibiwa kwa moto.
Viumbe vingine vilistaajabu kuona kiumbe dhaifu kama binadamu kukubali kubeba mzigo mzito.
Mwandamu yeye alichagua hiyari hivyo viumbe vingine havina hiyari ya kutenda kama mwanadamu.
Babu yangu mzaa babu yangu mzaa babu yangu ambaye hakukuta hivi vitabu na alikuwapo hata kabla Mtume ambaye kafanya hii habari / knowledge kuwa mainstream hajazaliwa unawemuweka katika kundi gani ?Nafsi inapoletwa duniani huwa ineletwa kwa ajili ya mtihani hivyo ili kuwe na fair test kila nafsi huanza ikiwa haina kitu kichwani!! Ila humu duniani Mungu tayari ameshatanguliza kuweka uongofu kupitia vitabu vyake vitukufu,mitume na manabii (wa kweli).
Kwahio watoto wote wanaokufa kabla ya kuwa wakubwa wamepewa free pass yaani wa mtihani wao ambao kule walikubali kubeba huu mzigo mzito wamekuja huku na kukuta kumbe kwao mzigo ni rahisi kuliko ?!!!!Hivyo ni jukumu lako mwanadamu kuutafuta ukweli kama vile unavyohangaika kila siku kuutafuta mkate wako.
Mtihani huu una muda maalumu kwa kila mtahiniwa kuna ambao wamepewa muda mrefu na wengine mfupi. Mtoto toka anapozaliwa mpk kufikia baleghe huwa hana dhambi! Ila kalamu inaanza kuandika mema na mabaya yake mara baada tu ya kuwa ameshabaleghe kwa maana sasa anaelewa lipi jema na lipi ovu.
And this was known all along that it would happen as it did happen ?Let's not forget. Shetani alipoasi, alisababisha ^system disorder^ ulimwenguni kote. I mean, harufu ya dhambi aliyoileta duniani haiwezi kuondolewa tu hivihivi. Lazima ing'olewa ^mizizi, shina, na matawi^ yake yote.
He has already seen and he knows au unamaanishi nini itamwonesha ? and for whose benefit ?Na, most importantly, uong'olewaji huo unafanyika katika namna ambayo daima itamwonesha Mungu kwamba ni mwenye haki na upepo.
But it was known all along ? And who created sin by the way ?The ultimate goal now is to eventually eradicate sin completely never ever to resurface again.
Unaweza kuiweka hapa hii story kwa faida ya wengi ? Kwani Shetani yeye hana mabawa ?Huku tena tunaambiwa shetani alipotupwa duniani, akaja kuanza kukimbizana na mwanamke gani sijui.. mara mwanamke akapewa mabawa ili shetani asimkamate!! Yaani shetani huyuhuyu ambae ametoka kupigana na Mungu, eti akashindwa kumkamata yule mwanamke 😆😆 seriously?
Kuna baadhi ya vitu ukisoma kwenye hivi vitabu yani unaona kabisa ni alfu lela ulela.
Unajua kitu kinaitwa figure of speech .....Ndiyo maana kuna umuhimu mkubwa sana wa kuisoma Biblia na kuielewa vizuri. Maswali yako yote (na zaidi) yanajibiwa humo.
Nimecheka sana ulivyosema kwamba Shetani na jeshi lake walikuwa ^wananunua silaha za maangamizi^! (Russia au Marekani?)🙂
Suala la imani ni tete. Linaweza kua sawa na hadithi ya kuku na yaiMimi nadhani kuna kitu hakipo sawa kwenye hizi habari za Mungu na shetani.
Kwanza kabisa, iliwezekana vipi kwa shetani (malaika) kumsaliti Mungu? Ni kipi hasa kilichomsukuma shetani kumsaliti Mungu?
Pili, tunaambiwa THELUTHI MOJA ya malaika mbinguni walimuunga shetani mkono!! Yaani katika kila malaika 10, zaidi ya malaika watatu walikua upande wa shetani! Ni kipi hasa ambacho malaika walikerwa na utawala wa Mungu kiasi cha kufikia theluthi yao kuunga mkono upinzani?
Tatu, tunaambiwa shetani alikua na JESHI na kwamba jeshi hilo lilienda vitani kupigana na jeshi la malaika!
a) Ina maana wakati shetani ana organize jeshi lake, wanafanya mazoezi, wananunua silaha za maangamizi, wana plan attacks nk Mungu yeye alikua amekaa tu anawaangalia? Si yeye anaona kila kitu?
b) Vita kati ya malaika wa Mungu na wa shetani ilipiganwa vipi? Wakati hao wote ni roho na tunajua roho haziumii wala hazifi? Silaha gani zilitumika? Ushindi ulipatikanaje?
Nne, tunaambiwa katika vita hiyo, shetani na jeshi lake walichakazwa vibaya sana na kutupwa duniani. Lakini hata hivyo, shetani na Mungu waliendelea kushirikiana katika "projects" mbalimbali, huku wakikutana mara kwa mara kupiga soga, kupanga majaribu nk.
Huku tena tunaambiwa shetani alipotupwa duniani, akaja kuanza kukimbizana na mwanamke gani sijui.. mara mwanamke akapewa mabawa ili shetani asimkamate!! Yaani shetani huyuhuyu ambae ametoka kupigana na Mungu, eti akashindwa kumkamata yule mwanamke 😆😆 seriously?
Kuna baadhi ya vitu ukisoma kwenye hivi vitabu yani unaona kabisa ni alfu lela ulela.
unaweza kusema vipi Aliyetengeneza hawa hawa hausiki kwenye haya matukio?
kwenye free will huwezi kusema mtu kapewa chaguo la kuchagua either shetani au Mungu wakati anaambiwa akichagua shetani atachomwa milele na akichagua mungu ataishi milele kwa raha mustarehe (hio ni intimidation) na chaguo hilo ni la kushinikizwa....
And How is That......., Kwamba chagua dhambi nikuchome, au nichague mimi nisikuchome !!!!, Pili katika chaguzi zako nimeweka vikwazo ambavyo vitapelekea ugumu wa kunichagua ?
Exactly. God knows the end from the beginning.And this was known all along that it would happen as it did happen ?
He has already seen and he knows au unamaanishi nini itamwonesha ? and for whose benefit ?
But it was known all along ? And who created sin by the way ?
Sijaelewa unachouliza...mwanzo nilikwambia kuwa Mungu ana maamuzi yake , yaani anafanya vile apendavyo wakati wowote ule. Yes uumbaji wa mwanadamu ulikuwepo katika mipangilio au maamuzi yake kabla hata ya kumuumba mwanadamu. Hakuna aliyeyajua haya ila YEYE mwenyewe.Naomba u-pause kwa sekunde chache alafu jiulize Mungu anajua kitakachotokea Kama jibu ni ndio nadhani usingeweka baadhi ya maelezo yako hapo chini kama ni hapa Okay tuendelee.
Angejua haya yatafanywa na Majini si angeweza kutengeneza Mwanadamu kabla au sio kwamba aliamua kuumba kiumbe mwingine sema ule muda wa kuumba kiumbe mwingine ulifika
Okay....
Bali Mungu ?
Simlazimishi kuamini ninachokiamini kama vile mchungaji asivyoweza kumlazimisha punda kunywa maji mara baada ya kumfikisha lamboni.Sawa wewe unayemtisha na kumuona duni yeye mwenye mtizamo tofauti na wako huoni kwamba na wewe ni walewale tu, tukiwa na open mind hapa huenda akabadilika akawa kama wewe ukimuonyesha kile unachokiamini wewe kwa mtizamo wake (sio kwa kutumia katiba yako lakini kama the only proof) sababu Katiba yako (Kitabu chako) kwake hakifanyi kazi na hakiamini ukishaamini kitabu hicho basi wewe ni muumini unayehitaji uelewa zaidi
Kujiua kutokana na changamoto za kimaisha ni aina ya mwisho ya kukata tamaa juu ya uwezo wa Mungu katika kukutatulia shida zako. Maisha haya ni mtihani tu hivyo usitegemee kuwa yatakuwa marahisi vile unavyotaka wewe. Ukiwa tajiri kuna mitihani na ukiwa masikini vilevile kuna mitihani yake.If that was the case hakuna watu wangejiua ?!!!, Kuna saa na wakati kujiua ni shortcut yaani mpambano wa kitaa unakuwa mgumu zaidi....
Au hujasikia watu kwenye pain wanaomba wapewe sumu wafe!!!
Elimu ya Mungu ni pana sana kiasi ukiamua kuitafakari sana kiundani unaweza ukakufuru ikiwa kama huna imani moyoni mwako na kama una imani ndani yako basi inakuzidishia zaidi imani juu ya uwezo wa Mungu.Mungu anajua kuwa mtu huyu atachagua "A"
Mpaka hapo "A" ishakuwa ni lazima
Kama "A" ishakuwa lazima maana yake huyo mtu hawezi kuchagua vinginevyo
Kama huyo mru hawezi kuchagua vinginevyo, basi hayuko huru.
Hivyo kila kitendo afanyacho, atafanya akiwa hana uhuru
Ili uhuru uwepo inatakiwa kuwa na multiple options ambazo ni possible
Since "A" haiwezi kuepukika maana yake iko fixed, choice kuwa fixed....hakuna uhuru
Kwahio in Short dhambi kubwa kuliko zote kwa Imani yao ni wale wanaoamini Mungu Tofauti na unayemwamini wewe ?
Au sijakupata vema ?