Kwanini muonekano wa jengo Kanisa Katoliki Salasala uko tofauti na unafanana na makanisa ya KKKT?

Kwanini muonekano wa jengo Kanisa Katoliki Salasala uko tofauti na unafanana na makanisa ya KKKT?

Hiyo picha ya kanisa katoliki ndio mfumo wa sasa ulivyo. Nenda kama unaelekea kitunda ile njia ya kwenda machimboni utakuta lipo la hivo hivo,
Na hapo ndani ya hilo kanisa kuna kila kitu, juu kwenye kwa ndani unakuta picha zile zimechorwa zikiashiria yesu ambazo zimechorwa kwenye vitu kama plastic, Ndani ukiingia ndio unaweza kuhis kabisa upo Rome 🇮🇹 Italy. Lingine nililiona mazizini
 
Wadau hamjamboni nyote?

Ndugu zangu tumezoea kuona majengo ya Kanisa Katoliki maeneo mbalimbali yakiwa na muonekano wa kipekee unaoakisi majengo ya asili ya karne nyingi zilizopita.

Lakini ukitazama jengo la Kanisa Katoliki Salasala Dar es salaam muonekano wake uko tofauti kabisa. Yaani kwa haraka utadhani ni jengo la Kanisa la KKKT

Swali langu ujenzi huo umezingatia vigezo gani? Kwanini uwe tofauti? Kwanini usiendane na makanisa tuliyozoea kama vile St Joseph posta ya zamani au St Peter Oysterbay

Wenye elimu mtujuze
Mwanzilishi wa Kanisa la KKKT alikuwa Padri Mkatoliki aliyeacha na kuanzisha Kanisa lake. Kuna mambo machache tu ambayo hakukubaliana nayo ndani ya Kanisa Katoliki, lakini mengi alikubaliana nayo. Hivyo, similarities kati ya Kanisa Katoliki na KKKT na hata Kanisa Anglikana ni nyingi sana. Ni mambo machache tu kuna tofauti za tafsiri au mtazamo.
 
Back
Top Bottom