Kwanini muonekano wa jengo Kanisa Katoliki Salasala uko tofauti na unafanana na makanisa ya KKKT?

Hiyo picha ya kanisa katoliki ndio mfumo wa sasa ulivyo. Nenda kama unaelekea kitunda ile njia ya kwenda machimboni utakuta lipo la hivo hivo,
Na hapo ndani ya hilo kanisa kuna kila kitu, juu kwenye kwa ndani unakuta picha zile zimechorwa zikiashiria yesu ambazo zimechorwa kwenye vitu kama plastic, Ndani ukiingia ndio unaweza kuhis kabisa upo Rome 🇮🇹 Italy. Lingine nililiona mazizini
 
Mwanzilishi wa Kanisa la KKKT alikuwa Padri Mkatoliki aliyeacha na kuanzisha Kanisa lake. Kuna mambo machache tu ambayo hakukubaliana nayo ndani ya Kanisa Katoliki, lakini mengi alikubaliana nayo. Hivyo, similarities kati ya Kanisa Katoliki na KKKT na hata Kanisa Anglikana ni nyingi sana. Ni mambo machache tu kuna tofauti za tafsiri au mtazamo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…