Kwasababu hawezi.
Iko hivi, hakuna mtu anaweza kutibu ugonjwa wowote kimiujiza, kwasababu Mungu hayupo. Wanachofanya hawa watumishi uchwara wanachagua wagonjwa mepesi ambayo dalili zake zinaweza kupoa kutokana na imani ya mtu. Pia wanachakachua vipimo, wanafanya utapeli, utaskia mtu anashuhudia kapona ukimwi ushahidi ni kwamba kapima kabla na baada ya huduma.
Ubongo wako unaweza kufanya afya yako kuimarika kwa muda mfupi, ikiwa utapata sababu ya kuamini hivyo. Hii inaitwa the 'placebo effect'. Wale majamaa wanategemea hii, atakuombea, na kwa vile wewe una imani, utaona dalili za kuumwa zitapungua kwa muda.
Ila hii ni kwa matatizo mepesi ambayo hayaonekani moja kwa moja mfano kichwa kuumwa, stroke, pressure, homa, hata wale wanaotupa fimbo na kutembea, maumivu kwenye joints yanaisha kwa muda mfupi.
Wasichoweza kufanya sasa, ni mfano mtu hana mkono, halafu wamuombee mkono utokee tu wenyewe, au mtu ana usonji halafu ajitambue haraka, mtu ana uvimbe, utoweke hapo hapo, mtu ana jeraha la nje lipone hapo hapo. Hawawezi.
Halafu sasa ile placebo effect ikishaisha kwenye ubongo wako huwezi kuwalaumu, watakuambia umekosa imani. Na hii inatengeneza kinyume chake kinaitwa 'nocebo effect' yaani hali yako inadhohofika kwasababu una mashaka.
Na mimi nawaona ni matapeli kwasababu hivi vitu huwezi kuvifanya bila kuwa na ufahamu navyo. Wangekua kweli wanafanya kazi ya Mungu wangejaribu kwenda huko mahospitalini, ila hawaendi. Ina maanisha wanauelewa mchezo.