Kwanini Mwamposa asiende kwenye mahosiptali kuombea wagonjwa na tukaona wanapona?

Kwanini Mwamposa asiende kwenye mahosiptali kuombea wagonjwa na tukaona wanapona?

Kule.................
Kule kuna watu wenye imani tofauti.
Kule sauti za juu hazitakiwi.
Kule kuna mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza.
Hospital ni sehemu ambayo ina taratibu na sheria zake za afya.
Mungu si all powerful lakini
 
Ukisoma vitabu vingine ndo utagundua ukatoliki nao ni bomba la uhuni..sema Baki tu huko coz ndo unapotaka. 😂Ila ni mule mule tu ..mnapigwa kiakili
Ila bora kama mtu anashindwa kuacha kabisa bora abaki huko ukatoliki ,ama uluther kuliko kwenda kwa walokole .
 
Ila bora kama mtu anashindwa kuacha kabisa bora abaki huko ukatoliki ,ama uluther kuliko kwenda kwa walokole .
Any form of religion ni mind control mtu akishakuambia amini yupo mtu invisible anakuangalia 24/7 anataka uamini hivi ufanye hivi or else ukifa unaenda kukaangwa.. hio ni mental abuse
 
Umewahi kuumwa wewe na kulazwa hospitali? Mtu yuko ICU au MOI anaweza kwenda huko kuombewa?

Huyo jamaa Angalia vitu vingi anavyoandika. Hawezi hata kuelewa kitu basic mtu akiwa ICU anakuwaje! Hawa watu walishalevywa na “HAUNA IMANI” Imani ni Utumwa yaani huwezi kuwa na fikra tunduizi mbali na kufungwa ndani ya boksi hilo.
 
Kuna mtasha mmoja alishangaa na kucheka alipokua anaona mara Kwa mara naangalia vipindi mbalimbali vya manabii Hawa wa bongo. siku Moja akaniambia hayo unayoona ni uwongo, nikamshangaa na kubisha sana.... Kuna siku akanibebea kitabu kinaitwa CHURCH MAFIA, baada ya kukimaliza nikaona nibaki tu na Ukatoliki wangu
Kinahusu nn mkuu in a nutshell.
 
Kuna Nabii James Nyakia yuko pale Mwenge mpakani mpaka kulaza wagonjwa analaza hata sijui kama Wizara ya Afya wana taarifa naye. Anafanya vipimo vya CT Scan,X-ray MRI kwa kutumia viganja vya mikono yake na wajinga wanamuamini. Vipimo hivyo ni Tsh.10,000/- na matibabu ni kachupa kadogo ka asali ka ml 20 na bei ni kuanzia 70,000/- hadi 300,000/- Huyu jamaa anawanyoosha kweli kweli wajinga.
Mkuu huyu naye katokea wapi?🤣🤣🤣 uwepo wa Hawa watu unaonyesha ni jinsi gani ujinga na upumbavu ulivyo kwa kiwango kikubwa, Hawa watu ni tishio kwa Taifa lenye kuhitaji maendeleo Kama hili.
 
hospitali wanaamini katika Tiba ya kisayansi mkuu na wala hairuhusiwi mtu kwenda kutoa tiba ya mombi walatiba asili. kama unaumwa nenda Kawe akakuombee utapona. Hata Yesu mwenyewe hakuwahi kwenda Hospital hata aliposikia rafiki yake Mkubwa Lazaro anaumwa hakutaka kwenda kumwangalia walakumuombea hadialipokufa.

Kama unahitaji Kuombewa au una ndugu yako mgonjwa basi mpeleke akafanyiwe maombi kisha uje na mrejesho

Mwisho sio magonjwa yote yanatibika kwa maombi.

Kumbe yesu baadhi ya magonjwa kwake ni ngoma nzito??? Sasa mbona huwa wanasema anaweza yote??
 
Uhuru wa kuabudu umegeuka mtaji kwa wajanja wachache huku wajinga wakiwawatajirisha wenzao.
Ndugu, hao wanaoenda kwake wanafanya hivyo kwa hiyari yao, hawajalazimishwa. Hauna sababu ya kuwa na uchungu na hela isiyo ya kwako, otherwise uniambie kuwa ulimpa mtu hela ya ada ukashangaa akaipeleka kwa Mwamposa
 
Kumbe yesu baadhi ya magonjwa kwake ni ngoma nzito??? Sasa mbona huwa wanasema anaweza yote??
Yesu Anaweza yote Kwa wanaomwamini halazimishi mtu

Aliye hospitali anaamini dawa zaidi haiwezekani umfuate hospital mtu ana Imani kwenye dawa
Kote duniani Kuna uponyaji aina mbili wa Hospital na spiritual Healing .Mtu mwenyewe huamua aende wapi Huwa hawaingiliani
 
Mgonjwa yupo icu amfate?
Ndugu zake wamfuate.

5 Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,

6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.

7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.

8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

9 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.

13 Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile.
 
Kwann hao wagonjwa wasiende kwa mwamposa kuponywa hadi wafatwe hospitalini.

Mimi nina tatizo flani naumwa

Nimezunguka kwa hao wote mnaoita ni manabii na waombeaji.

Nimepakwa mafuta ya upako nmeombewa sana kwa miaka mingi. Mpaka nikakata tamaa

Nawahakikishia wenye matatizo halisi hawaponi. Wanaotoa shuhuda wamepangwa ili sisi wenye matatizo halisi tupigwe pesa.

Wale wengine atakuja siku ya kwanza anaombewa anapona ndio wanawaonesha kwenye TV

Sisi ambao hatuponi unaambiwa huna imani na haujaokoka ndo mana haujapona (wakati kwenye ushuhuda unakuta mpaka malaya wamepona) kwahio wanakupangia ratiba ya mafundisho kuongeza imani yako na kuokoka utakua unaenda kila siku na matukio yote utaambiwa uwe unahudhuria.

Utaliwa pesa mpaka uchoke.

Kama huamini mpeleke ndugu yako ambae anaumwa serious kwelikweli muone kama atapona.

For years nmehangaika mpaka nmejifunza kuishi nalo. Maana wote ni walewale tu utapoteza muda na pesa.

Hata hao mnaowasifiaga hapa ni waongo tu.

Take it or leave it ila me naongelea my personal experience. Hili tatizo nnalo since 2008, now nmejifunza kuishi nalo tu
 
Back
Top Bottom