Kwanini Mwamposa asiende kwenye mahosiptali kuombea wagonjwa na tukaona wanapona?

Kwanini Mwamposa asiende kwenye mahosiptali kuombea wagonjwa na tukaona wanapona?

Si comment chochote kwa sababu nipo dilemma kwasabu nmefika na nmejionea mwenyew
 
Hili ndio swali ninalojiuliza kama kweli huyu ni mchungaji wa ukweli.

Kwa mfano, kwanini tusimuone Mwamposa akiwa Ocean Road hospitali anaombea wagonjwa wa kansa na tukaona wananyanyuka vitandani au madaktari wakathibitisha kupona kwa hao wagonjwa?

Uhuru wa kuabudu umegeuka mtaji kwa wajanja wachache huku wajinga wakiwawatajirisha wenzao.
Mwivi haji ila achinje, aue na kuangamiza. Hawa manabii wa uongo kina mwamposa na wenzake ni watendaji kazi wa ibilisi, na walio wengi ma hospitalini ni kazi za ibilisi so yeye hudeal na fresh clients, kuwaibia nyota zao na kuwapakaza magonjwa yasiyomithilika. Endeleeni kula keki za upako, chumvi, maji ya maiti na hayo mafuta.
 
Mwamposa anadili na mambo ya Giza,

Sasa unaumwa malaria wakati si mambo ya giza.mahospitali kunamda unaumwa madaktari wanakwambia jiongeze,nenda kienyeji

Mwamposa anadili na mambo ya Giza,sio magonjwa ya kawaida
Ok, basi ni sawa kama hospitalini hakuna mambo ya giza.
 
We unasali/swali wapi? Na je Mungu wenu haponyi magonjwa, kama anaponya kwanini kiongozi wako wa kiroho humwambii aende hospital kuwaombea wagonjwa. (Simtetei mwamposa ila swali lako la kitoto Bwana
 
We unasali/swali wapi? Na je Mungu wenu haponyi magonjwa, kama anaponya kwanini kiongozi wako wa kiroho humwambii aende hospital kuwaombea wagonjwa. (Simtetei mwamposa ila swali lako la kitoto Bwana
1. So unakubali Kuna miungu tofauti na yote inaweza kuponya? Sasa unajuaje tofauti ya mtu kupona kiasilia na kuponywa kimiujiza
2. Kiroho ndo nini
 
Siku nikiona Hawa manabii wanamponya Kiwete yaani ambaye hana miguu kabisa nikashuhudia Kwa macho yangu akinyanyuka na kutembea, ndipo nitawaamini, au nikiona mtu ninaye mfahamu kuwa ni kipofu au Kiwete na ameponywa hapo nitajiunga nao
 
Ni yupi alishawahi kufanya hivo na matokeo yakaonekana! Wengi wetu tulishapumbazwa hivo tumebaki tukitegemea miujiza ambayo haipo kabisa! Ee Mungu tunakuomba ukatunusuru na hawa aina ya watu ni hatari sana [emoji1431]
 
Mchungaji Mwamposa akamatwa baada ya vifo vya waumini​

Ndugu ya waliofariki katika ibada ya mafuta ya mpako

Maelezo ya picha,
Ndugu ya waliofariki katika ibada ya mafuta ya mpako

Watu 20 wafariki dunia mjini Moshi walipokuwa wakikusanyika katika viwanja vya Majengo kuhudhuria Ibada iliyoongozwa na Mtume Boniface Mwamposa.
Watu hao wamefariki dunia baada ya kukanyagwa na wenzao wakati wakitoka katika lango moja waliloelekezwa kupita ili kukanyaga mafuta ya upako.
Katika tukio hili watu 16 wamejeruhiwa.
Kiongozi wa kanisa la Inuka Uangaze, anayejitambulisha kama nabii na mtume Boniface Mwamposa , hii leo amelazimika kusitisha ibada kwa ajili ya kuitikia wito wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Tanzania kulikotokea vifo vya waamini wake.
Hospitali

Maelezo ya picha,
Baadhi ya waumini wakiwa hospitali

Mwamposa ambaye huendesha ibada zake katika eneo la Tanganyika Packers, leo Jumapili Februari 2, Nabii huyo amelazimika kufupisha ibada ya kwanza na kuanza safari ya kuelekea Moshi alikoitwa na polisi.
Ibada huwa inaisha majira ya saa saba lakini leo imeisha saa nne na nusu asubuhi.

Maelezo ya video,
Aliyenusurika kwenye tukio la kukanyagana asimulia
Gazeti la Mwananchi limeandika kuwa jana katika kongamano lake la kukanyaga mafuta ya upako mkoani Kilimanjaro, watu 20 walipoteza maisha wakisukumana kukanyaga mafuta hayo.
Wakati hayo yakiendelea, waumini wa nabii huyo wamemkingia kifua na kueleza suala la watu kukanyagana kwenye mikutano mikubwa ni kawaida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia za watu 20 waliopoteza maisha wakati wakitoka katika Ibada huko Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Magufuli ameeleza kusikitishwa na idadi kubwa ya vifo vya Watanzania waliopoteza maisha katika matukio hayo na amewaombea Marehemu wote wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wapone haraka na kurejea katika majukumu yao.
Idadi ya vifo vya watu huenda ikaongezeka

CHANZO CHA PICHA,GODFREY THOMAS , AYO TV
Maelezo ya picha,
Idadi ya vifo vya watu huenda ikaongezeka

Aidha amemtaka mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro bi. Anna Mghwira kufikisha salamu zake za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na vifo hivyo.
Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wote kuchukua tahadhali katika matukio yote yenye viashiria vya hatari ikiwemo mikusanyiko mikubwa ya watu na amevitaka Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha vinasimamia ipasavyo tahadhali za kiusalama.
chanzo. Watu 20 wafariki wakikimbilia mafuta ya upako Tanzania - BBC News Swahili
 
Siku nikiona Hawa manabii wanamponya Kiwete yaani ambaye hana miguu kabisa nikashuhudia Kwa macho yangu akinyanyuka na kutembea, ndipo nitawaamini, au nikiona mtu ninaye mfahamu kuwa ni kipofu au Kiwete na ameponywa hapo nitajiunga nao
Hutoona kamwe, utabaki kusikia story za watu walioponywa lakini wako mbali na huwezi kuthibitisha
 
Ukitaka kujua vizuri hao watoa ushuhuda jiulize kuna mkazi wa hapo hapo kawe aliyepona? Ina maana kawe hakuna wagonjwa au wote hawana imani
Mkuu umepiga Ikulu?

Au jiulize kuna kiwete yeyote uliyekuwa unamjua anatembea kwa kusota matako ambaye amepona?
 
We unasali/swali wapi? Na je Mungu wenu haponyi magonjwa, kama anaponya kwanini kiongozi wako wa kiroho humwambii aende hospital kuwaombea wagonjwa. (Simtetei mwamposa ila swali lako la kitoto Bwana
Yaaani mwapomposa Ana nguvu ko wote wanao shudia waongo haya mambo watu tuache kuhukumu .mimi binafsi na ushuda tena kwa njia TV sio Kawe .ko kila mtu abaki na imani yake mambo imani wanapona wanashudia ko wote wanapangwa
 
Kwani magic shows au kwa jina lingine mazingaombwe, si unajua yamepangwa na bado unashuhudia, au unadhani ni wachawi kweli wale
 
Back
Top Bottom