Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Naona dalali wa Dar umekuja kwa kasi ya hatari
Tangu nimenunua gari hili mwanza halijawahi kunisumbua Kwa lolote ni mwaka wa pili Sasa. Ni hii juzijuzi nilipotuma hiyo thread kutafuta msaada na ishu ilikuwa ndogo tu, plug moja ilikuwa haichomi. Nimebadili plug na chombo imetembea Sumbawanga dar bila shida.

Kwanza magari yenu ya Dar mabodi yameliwa na chumvi, madalali wengi matapeli. Sitaki hata kuwadikia.

Kaka nenda mwanza kanunue, watafute Sham motors, hawana ubabaishaji na hawauzi magari mabovu. Mi niliona gari mtandaoni, wakataka nilipie advance ili lisiuzwe nikalipa nilipoenda,hakukuwa na longlongo, Tena wanakwambia kama hujaridhika unaweza kubadili gari au uchukue ela Yako. Sijawahi kujuta kununua gari mwanza.
 
Tupo huo ujanja tudake magari aisee mana kuna jamaa yangu ana 13m ila bado hajapata gari ya kununua mpk leo kwa dar
 
Mi nahitaji kluger Kama kwa mwanza namba DY ni m13 Hadi m15 tunafanya biashara
 
Hii gari ukiichukua ukaileta hapa Dar ukaivesha rim kali na make up kidogo tu unauza 12m yani umekosa sana 1Om mtu haruki.
 
Dar madalali ni mabingwa wa kushusha kilometre πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ gari ikifanyiwa soap sop ikapigwa Ikeda yani lazma uingizwe kingi. Watu wanalamba 3M wanagawana biashara inaisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…