Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Wengine ni matapeli,
Anakutamanisha na Bei rahisi ila gari iko mikoani ili ukikolea anakuambia tuma hela ya mafuta uletewe Dar.

Mkuu mtu unaanzaje kutuma pesa? Mimi gari naifuata mwenyewe na naikagua mwenyewe. Tunamalizana hapo nasepa nayo

Kutuma pesa kwa mtu usiemjua unataka lawama tu
 
Habari za asubuhi wakuu.

Kwa muda kidogo nimekua nikifanya utafiti mdogo wa madalali wauzaji wa magari instagram na social media nyingine.

Kuna kitu nimegundua nikaona nijadiliane nipate majibu sahihi.

Nimeona madalali wa mwanza wanauza gari kwa bei rahisi sana ukilinganisha na wa Dar es Salaam (kwa gari zenye specificationa sawa)

Mfano
Toyota crown
Mwanza nakuta nyingi average milion 8 (zinaanza 7m mpaka 10m hivi) ila dar es salaam average milion 11 (zinaanzia 10m mpaka 13m).

Toyota mark x
Mwanza around 5.5m mpaka 7m, ila Dar es salaam around 8m mpaka 11m

Toyota kluger
Mwanza 9m mpaka 14m.. ila Dar es salaam 14 mpaka 18

Toyota harrier tako la nyani
Mwanza 14m mpaka 18m
Dar 16 - 22m

Sasa ndugu zangu naomba kujua sababu ya utofauti huu mkubwa wa bei! Je madalali wa Dar ni kwamba wanapiga cha juu kingi au watu wa mwanza wana pesa sana ndio sababu wanauza bei ndogo?

Maana nimeshawishika kidogo kununua harrier kwa hawa jamaa wa Mwanza maana bei zao kitonga sana.

Nawasilisha
Mwanza ni mji wa watu wenye hela, madini, samaki, etc. Hivyo mtu akitumia gari kidogo anataka apate lingine unakuta magari mengi yapo sokoni
 
Binafsi sina gari ila nachangia kama mkazi wa maeneo ya Mwanza.
Mwanza magari yapo ya hali nzuri sana na kinachofanya bei iwe nzuri ni kwamba watu wa huku wapo real sana na hawapendi ubabaishaji. Biashara nyingi za huku hazipitii kwa dalali. Huku hata kiwanja utakipata kwa bei kamili toka kwa mnunuzi. Wengi wanaamini dalali anaweza kukufanya bidhaa yako isinunulike hara kwa kujipangia bei yake.

Taarifa ya kuuzwa kwa kitu huku unaweza kuipata kwa mtu na huyo mtu akakupa hadi namba za mwenye mali . Kwa daslam kuonana na mwenye mali hiyo ni bahati ya mtende. Kwahiyo niseme tu huku sio gari hata kiwanja ukiuziwa 2M jua ni ndio hiyo pesa imemfikia mwenye kiwanja.
Jibu sahihi kabisa,Dar/Arusha mtu alikupa tu no. Ya mwenye Gari/ kiwanja tu nae anajiweka kama dalali tayari anafukuzia posho hapo.Ndio hua Wanapakwa Mafuta tu.Pumbavu zao
 
Halafu wanaendekeza njaa,kuna mwaka niliuza gari kupitia dalali wa migo pale bila yeye kujua,baadae huko akaja kujua yule mteja aliyomleta ndie niliemuuzia alilalamika sana nimpe hata ya maji lakini ndio ikawa too late,mteja kafika bei niitakayo mimi na tena laki 7 juu,dalali hataki kuuza eti laki 7 ndogo na hapo hapo kwangu ilibidi ale kama 2 hivi,dogo wangu mmoja akachukua namba ya mteja kijanja pale pale,tukamuita docho tukafanya biashara
Hahah hii ndio dawa Yao.Safi sana mkuu.
 
Dah aiseeh hapo kuipata gari straight kwa mmiliki ndio changamoto ilipo.

Unaeza kutusaidia mbinu gani tunaweza tumia kuwakepa madalali, kumpata mmiliki moja kwa moja?

Maana unaweza kuta unaliwa zaidi ya 4m na madalali
Binafsi huwa nikipata namba ya gari huwa sihangaiki na madalali bali naangalia usajili ni nani mmiliki ila changamoto huwa inakuwepo iwapo aliyeuza mwanzo hakubadilisha jina, ila huwa kafanikiwa kuunganishwa na huyo mwenye jina lililopo kwa kadi ya gari hilo.

NB: Hii si kwa kila mtu anaweza kufanya hivi
 
Back
Top Bottom