Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Naona dalali wa Dar umekuja kwa kasi ya hatari
Tangu nimenunua gari hili mwanza halijawahi kunisumbua Kwa lolote ni mwaka wa pili Sasa. Ni hii juzijuzi nilipotuma hiyo thread kutafuta msaada na ishu ilikuwa ndogo tu, plug moja ilikuwa haichomi. Nimebadili plug na chombo imetembea Sumbawanga dar bila shida.

Kwanza magari yenu ya Dar mabodi yameliwa na chumvi, madalali wengi matapeli. Sitaki hata kuwadikia.

Kaka nenda mwanza kanunue, watafute Sham motors, hawana ubabaishaji na hawauzi magari mabovu. Mi niliona gari mtandaoni, wakataka nilipie advance ili lisiuzwe nikalipa nilipoenda,hakukuwa na longlongo, Tena wanakwambia kama hujaridhika unaweza kubadili gari au uchukue ela Yako. Sijawahi kujuta kununua gari mwanza.
 
Binafsi huwa nikipata namba ya gari huwa sihangaiki na madalali bali naangalia usajili ni nani mmiliki ila changamoto huwa inakuwepo iwapo aliyeuza mwanzo hakubadilisha jina, ila huwa kafanikiwa kuunganishwa na huyo mwenye jina lililopo kwa kadi ya gari hilo.

NB: Hii si kwa kila mtu anaweza kufanya hivi
Tupo huo ujanja tudake magari aisee mana kuna jamaa yangu ana 13m ila bado hajapata gari ya kununua mpk leo kwa dar
 
Hapo nimekupata mkuu, but how about yale
Magari unakuta halijatumika sana nchini

Lets say namba DYZ, nmekuta harrier mwanza anauza 15m while dar 22m, na wote ni DY

Na pia dar gari hio hio moja unakuta bei tofauti, kuna harrier nmekuta madalali watano kila mtu bei yake 16m, 17.5m, 19m .. na ni gari hio hio
Mi nahitaji kluger Kama kwa mwanza namba DY ni m13 Hadi m15 tunafanya biashara
 
8ad2eca2-da54-4eff-bcf5-4db3c374da5e.jpg

6d72a4ed-cf28-4183-9d38-22645acd3a94.jpg

e117075b-73bc-404c-b872-4bd3c200c055.jpg

Hao ni madalali wawili kila mmoja ameweka bei yake.
 
Mwanza inaweza ikawa kimbilio wa wazee wa kuunga unga,maana zanzibar baada ya kuona watu wengi wanaenda kununua magari kule nao wakapandisha bei na hapo ulipie meli na ukifika bara ulipie ushuru,crown kama hii inauzwa m 7 mwanza kweli kucheleView attachment 2285065
Hii gari ukiichukua ukaileta hapa Dar ukaivesha rim kali na make up kidogo tu unauza 12m yani umekosa sana 1Om mtu haruki.
 
1.Mwanza mzunguko wa pesa si kama dsm, so ukiweka bei kubwa wengi hawanunui.

2. Dsm gari ni almost basic need but mwanza ni luxury.. uhitaji wa gari mwanza si wa lazima sana kwasababu usafiri ausumbui sana na hauna kero, pia trip za mwanza ni fupi fupi tofauti na DSm

3. Utanzaji wa gari kanda ya ziwa ni mbovu sana kulinganisha na dsm.. ukienda gereji za mwanza ukaona jinsi wanavofanya service za magari, oil wanazotumia, transmission fluid wanazotumia yaan unakuta wanaweka mi lubex kwenye transmission wakat mwingine wanaongezea na mioil eti iwe nzito dah.. nilishangaa sana..

So ukija nunua wakati mwingine you buy a time bomb so mtu anakua anatafuta namna ya ku dispose gari mapema kabla halijamfia.
Dar madalali ni mabingwa wa kushusha kilometre 😂😂😂 gari ikifanyiwa soap sop ikapigwa Ikeda yani lazma uingizwe kingi. Watu wanalamba 3M wanagawana biashara inaisha
 
Back
Top Bottom