Kwanini namuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan?

Kwanini namuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan?

Ni sawa pia
Ila kwa taarifa yako sasa, Dunia imehamia Middle East. Kule ndo kwenye fedha na kule ndo kwenye picha halisi ya dunia iko wapi na inaenda wapi.

Ndo wanaendesha Dunia. Usishangae sasa wachezaji wanahamia Ligi ya Saudia.

Jifunze elimu haina mwisho
Sipati picha tukiipata kiongozi Kutoka bukoba itakuwaje!!!

Kila kiongozi akija, anakuja na muono wake binafsi, ghafula wote tunafuata maono binafsi,

Tunahitaji MAONO ya nchi, Dira ya nchi Kwa miaka 200 ijayo,

Rais akiingia madarakani anakuta ramani mezani ya tuendako.

Katiba mpya ni sasa, Si BAADAYE.

Amen
 
Sipati picha tukiipata kiongozi Kutoka bukoba itakuwa,

Kila kiongozi akija, anakuja na muono wake binafsi, ghafula wote tunafuata maono binafsi,

Tunahitaji MAONO ya nchi, Dira ya nchi Kwa miaka 200 ijayo,

Rais akiingia madarakani anakuta ramani mezani ya tuendako.

Katiba mpya ni sasa, Si BAADAYE.

Amen
Kwa kulitambua hilo ndo mana Tume ya Mipango imerudi katika kipindi chake.

Simpambi tu. Nafuatilia sana utendaji wa Serikali yake na naufanyia sana tathmini.
 
Thamani ya Samia itakuja kuonekana siku hayupo madarakani...
Tena ikiwezekana tupate jitu lenye Sera za Magufuli aturudishe upya kwenye "kuunga mkono juhudi" bila kuuliza swali wala kupinga kitu
Kama tunataka kwenda mbele kweli. Ni lazima tujitahidi sana kuepuka kupata viongozi ambao wana mlengo wa kushoto hasa wenye nationalist ideas.

China ambao wana asili ya ukomunist wanaepuka sana kuwa na Kiongozi wa namna hiyo ndo mana sasa soon wataenda kuiongoza Dunia.
 
Una miaka 47 kweli au ni 17? Wasomi wote wanasema watu 1.5milioni wameiuza nchi ya watu 60 mili lakini wewe hilo hulioni? Halafu unasema eti watanzania ni wajinga? Hapo mjina ni nani?

Hivi kwaanza una watoto au umepuyanga nchi za watu ukasahau kuacha alama duniani? Kama unao, je unafikiri kwa mikataba hii wajukuu wako watakuwa na haki yoyote hapo Kilimanjaro?
 
Kumekuwa na maneno maneno humu kuwa mimi na wenzangu tunaomuunga mkono Rais Samia basi kama sio Waislamu basi ni Wazanzibar na kama hauko kote huko basi wewe ni chawa wake.

Hizi ni siasa za majitaka ambazo kusema kweli zimeegemea kwenye vihoja badala ya hoja.

Kwa upande wangu Mimi Lord Denning, mimi sio wa asili wa Zanzibar wala sio muislamu. Ni mkristo mkatoliki na kusema kweli simjui Rais Samia, Sijawahi onana nae na wala hanijui.

Katika uzoefu wangu wa kufuatilia siasa za dunia ikiwemo Afrika na Tanzania naweza kusema Mimi Lord Denning naweza kuwa mmoja wa watu wachache sana wanaoifahamu dunia na siasa zake. Kwa umri wangu wa miaka 47 sasa nimeenda nchi nyingi, karibu mabara yote. Na kote huko nilikofika nimekuwa nikijifunza sana historia ya sehemu husika, siasa zake, maisha ya watu na uchumi wao

Kwa upande wa marais wa Tanzania nimebahatika kuwepo kipindi cha Nyerere ingawa nilikuwa mdogo, kipindi cha Mwinyi nikiwa na akili, kipindi cha mkapa hadi saivi nikiwa mtu mzima na akili zangu.

Nilimkubali sana Mkapa na sera zake za kiuchumi. Nikamkubali sana Kikwete maana nae kwenye uchumi alienda sawa pamoja na kuyumba maeneo kadhaa na nikatofautiana na Magufuli hasa kwenye sera zake za kiuchumi za state capture na sasa namuunga mkono Samia kwa sababu so far nimemsoma na kumuelewa kuwa anaenda vizuri sana kwenye sera za kiuchumi.

Kwanini namuunga mkono Rais Samia?

1. Wanasiasa wengi wa nchi yetu ukiondoa Mkapa walikuwa wanaogopa kufanya maamuzi positive kweli kiuchumi kwa kuogopa siasa ila Samia hayuko hivyo. Kwa nilivyomsoma Samia, anajua sana geopolitics, anapenda vitu vizuri, ni mkisasa kweli. Kwa sasa dunia ilipo na inapokwenda fursa ziko kwenye maeneo hayo. Moja ni kwa namna gani unavyojiweka na kujitangaza vizuri na pili ni namna gani unavyojiweka kisasa. Kwa maamuzi ya kuboresha sekta nyeti za kiuchumi ikiwemo bandari, utalii tena bila kujali siasa, kusema kweli amenivutia sana.

2. Tanzania kuna wajinga wengi sana na ujinga wao umewafanya kuwa masikini sana. Katika kuwaondoa kwenye ujinga wao ni lazima uwaonyeshe kweli kuwa wanatakiwa kuondoka katika imani na mazoea ya kijinga. Kwenye hili kusema ukweli wa Mungu wangu Samia anafanya vizuri.

Mabadiliko yanayofanyika katika uendeshaji wa uchumi wetu ili kutufanya tuendeshe uchumi katika mazingira yenye ushindani ili kupata matokeo mazuri kweli yamenifanya nijitokeze wazi kumuunga mkono huyu Mama.

Tanzania shida kubwa iliyopo ni watu kutopenda ushindani. Na ndo mana ubora katika mashirika ya Umma umekuwa finyu sana. Kutufanya tuondokane na mentality hii inanifanya kumuona Rais Samia kama Rais bora zaidi kuwa nae katika kipindi hiki.

Mwisho napenda kumaliza kwa kusema uongozi na maendeleo ya kweli ni matokeo ya kutumia akili vizuri. Sio rasilimali wala sio utajiri ulio nao kama Taifa. Kuna sehemu Tanzania tunatakiwa kufika ila ili tufike lazima tutumie kweli akili zetu vizuri hasa katika kujua Dunia ipo wapi, inaenda wapi na itakuwa wapi katika siku nyingi zijazo.

Ili tufike huko lazima Watanzania tutumie akili zetu vizuri. Tuifanye nchi yetu kuwa sehemu ya mjadala wa dunia kama sehemu nzuri ya kuja, kuwekeza na kuishi ikiwemo kufanya starehe. Na ili tutimize hili lazima tuite watu wenye akili tofauti, wabadirishe fikra zetu, na watufanye tuwaze vizuri. Ni lazima tubadiri mfumo wa elimu yetu ili kutufanya tuende kama dunia inavyoenda ili tusiachwe nyuma.

Asanteni
Lord Denning
Kilimanjaro
Nonsense
 
Hebu acheni kumdharau kisa mwanamke mnajua mkimsifia Kaukuu ka wilaya mezani .mama anapendwa na watanzania wote hadi wapinzani .ila sasa tumeacha kumuunga mkono hadi atutolee hilo Jinamizi la jehanam aka DP WORLD
 
Kwa kulitambua hilo ndo mana Tume ya Mipango imerudi katika kipindi chake.

Simpambi tu. Nafuatilia sana utendaji wa Serikali yake na naufanyia sana tathmini.
Ukubali pia, fursa za kiuchumi kuangalia uarabuni Si maono ya nchi ni maono binafsi ya aliyepo.

Tume ya mipango itaangalia aliyepo anasema nini, anawaza nini.

Tunahitaji Tume ya mipango HURU isotokana na chama Dola pekee.
 
Una miaka 47 kweli au ni 17? Wasomi wote wanasema watu 1.5milioni wameiuza nchi ya watu 60 mili lakini wewe hilo hulioni? Halafu unasema eti watanzania ni wajinga? Hapo mjina ni nani?

Hivi kwaanza una watoto au umepuyanga nchi za watu ukasahau kuacha alama duniani? Kama unao, je unafikiri kwa mikataba hii wajukuu wako watakuwa na haki yoyote hapo Kilimanjaro?
Sasa wewe tufanye ni msomi. Niambie nchi imeuzwaje?

Usikimbie!
 
Hebu acheni kumdharau kisa mwanamke mnajua mkimsifia Kaukuu ka wilaya mezani .mama anapendwa na watanzania wote hadi wapinzani .ila sasa tumeacha kumuunga mkono hadi atutolee hilo Jinamizi la jehanam aka DP WORLD
Jinamizi kivipi?
 
Case closed

You can't defend your point, that's all!!

So will just consider it as hate speech!
My points are well above your head.

Shills like you can’t go toe to toe with me.

I’ll wash and fold you like a pretzel.
 
Kwa upande wangu sijawahi kumkubali hata mara moja kwa sababu sioni aliko faulu hata sehemu moja, Kila sehemu ana jipapatua bila mafanikio,huko kwenye uchumi ndio kafeli zaidi Kila siku uchumi unazidi kuanguka,
anacho weza yeye ni kukopa na kuwapa mianya wezi kuendelea kuiba kwa kadri wanavyo penda, alafu anawauliza eti "bado hamja tosheka" 🤔🤔
Hana sifa na haiba ya uongozi hata kidogo ame tuonesha mwenyewe kwamba hatoshi kwenye nafasi iliyo muangukia kama ngekewa
 
Kwani Bukoba kuna shida gani?
Sipati picha tukiipata kiongozi Kutoka bukoba itakuwaje!!!

Kila kiongozi akija, anakuja na muono wake binafsi, ghafula wote tunafuata maono binafsi,

Tunahitaji MAONO ya nchi, Dira ya nchi Kwa miaka 200 ijayo,

Rais akiingia madarakani anakuta ramani mezani ya tuendako.

Katiba mpya ni sasa, Si BAADAYE.

Amen
 
My points are well above your head.

Shills like you can’t go toe to toe with me.

I’ll wash and fold you like a pretzel.
No more arguments

Refer the post herein above

Case is closed!
 
Hapo umefanya generalisation. Kuna watanzania tena wengi sana nikiwemo mimi ambao hatuoni shida kwenye huo mkataba
again ni haki yako na hao wengine kujiondoa ufahamu.

Nimesema Watanzania hawajaridhika na mkataba, hivyo, haina maana hawaungi mkono uwekezaji huo wa Bandari.

Wewe huoni kuna tofauti kati ya Kuunga mkono na Kuridhika kwa jambo?

amani ikufikie
 
Back
Top Bottom