Quran huiamini kwa hivyo samaki hukaangwa kwa mafuta yake
Kiarama ilikuwa ndio lugha inayozungumzwa na Wayahudi wa Palestina. Kwa hiyo, inaaminika kuwa Yesu na wanafunzi wake walikuwa wakizungumza na kufundisha kwa Kiarama.
Mapokeo ya mdomo kwa mdomo ya mwanzo kabisa ya matendo na maneno ya Yesu bila shaka yaliduru katika Kiarama.
Hata hivyo, Injili nne zimeandikwa kwa kauli tofauti kabisa, Kigiriki, lugha ya ustaarabu wa ulimwengu wa eneo la bahari ya kimediterania, ilihudumia makanisa mengi, na kuyafanya yawe ya Kigiriki (Yanatumia Kigiriki) badala ya Kipalestina (Kiarama).
Alama za Kiarama bado zipo katika Injili za Kigiriki.
Kwa mfano, katika Marko 5:41, “Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.”
na Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”