Kwanini Nchi za Kiislamu zinaendelea kukumbwa na umaskini? Sababu zilizofichika za Kihistoria na Kisasa

Kwanini Nchi za Kiislamu zinaendelea kukumbwa na umaskini? Sababu zilizofichika za Kihistoria na Kisasa

Nchi zote ulizotaja hapo ni kwasababu ya uchumi wa mafuta (dutch disease )

Kisa tu takwimu za Per Capita zinasema 10,000$; sio kwamba ndio hicho kiasi kimegawanyika ipasavyo kwenye mikono ya wananchi

Nigeria yenyewe hapo Per Capita unakuta inasoma kubwa ila ukienda kwenye uhalisia umakini kama wote

Mfalme wa Morroco kuahidi kujenga uwanja mbona kitu cha kawaida , hata Magu tungemsimika mfalme angewajengea Wanyarwanda hadi treni ya mwendokasi
Uisilamu na zaka inafanya Distribution ya keki ya taifa kuwa kubwa,

Hizo nchi zote za mafuta ukienda wasio na ajira wanalipwa, wasio na Nyumba wanajengengewa wasio na gari wanasaidiwa etc. Hapo Saudia masikini ni yule asie na Nyumba na Gari, unakuta Bilionea anadonate matrilioni ya hela kusaidia masikini.

Kuna mabilionea wengi mno huyu anatoa trilioni 30 huyu trilioni 60 etc kusaidia masikini watu wataachaje kuishi vizuri? Mambo hayo unayakuta kwa waisilamu tu, kote duniani hakuna dini inayoongoza kutoa Charity kushinda waisilamu.
 
Amka utajikojolea
 
Kuna mambo mawili kuna kua nchi ya kiislamu na kua nchi ya waislamu, Tanzania ni nchi ya waislamu sio ya kiislamu, elewa hilo mkuu ingekua ya kiislamu tungekua na sheria za kiislamu, ila hatuna ni ya waislamu wanao ongozwa na sheria za kawaida.
Nchi ya Waislamu na mnashindwa kujitoa kwenye kitanzi hata cha BAKWATA ndugu zangu, are you guys serious? 🤣🤣
 
Mbona Tanzania pamoja nakua na waislamu majority 60% na viongozi walio lelewa na kukuzwa kwa maadili ya kiislamu wa zaziba r na bara bado tunapiga hatua kila mwaka, kiuchumi.......bigup Mama Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.........japo wengi wanaumia kulikubali kwamba hi nchi ni ya kiislamu kimya kimya, tamaduni nyingi tunazo fanya hapa kwetu ni za kiislamu kabisa.
Acha upotoshaji waislamu Tanzania ni asilimia 31.5 according to.statistics
 
Hoja ni kwamba neenda kwenye website ya FBI na CIA uone nchi zinazo categorise kua na waislamu wengi Africa aTanzania ipo sensa ya CIA wanajua wenyew e waliifanya je mwaka 1965 waislamu Tanzania walikua 56% tangu huo mwaka waislamu hawaja ongezeeka unafikili na kufika 60%?
Mungekuwa wengi si mngekuwa na mahakama ya kadhi ? Mngekuwa wengi wahindi na waarabu wangemiliki kila kitu kila mkoa humu Tanzania. Mpaka magenge yangemiikiwa na wahindi na waarabu.
 
Acha upotoshaji waislamu Tanzania ni asilimia 31.5 according to.statistics
Ushahidi tafadhali mkuu, wewe unajua kwanini serekali haitaki kuweka lipengere cha dini kwenye sensa ya watu.
 
Nchi nyingi zenye Waislamu wengi zinakabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi, hali inayochangiwa na sababu za kihistoria, kitamaduni, na taasisi. Nchi kama Morocco na Yemen, licha ya historia tajiri ya kiasili, zinakumbwa na viwango vya juu vya umasikini, huku wastani wa Pato la Taifa kwa kila mtu (GDP per capita) ukiwa chini kwa takribani dola 5,000 ikilinganishwa na wastani wa dunia. Sababu za hali hii ni mseto wa mambo ya ndani na nje yaliyofanya nchi hizi kushindwa kufanikisha maendeleo endelevu.

Mafanikio ya Kale na Sababu za Kuporomoka

Karne ya 10 BK, ulimwengu wa Kiislamu ulikuwa moja ya nguvu kubwa za kiuchumi duniani, ukichangia asilimia 10 ya Pato la Dunia. Hali hii ilitokana na ujuzi wa biashara, maendeleo ya kiteknolojia ya wakati huo, na mifumo ya kiuchumi iliyokuwa imara. Hata hivyo, mafanikio haya hayakudumu kutokana na sababu zifuatazo:

1. Ukosefu wa Makampuni Makubwa na Biashara za Kudumu

Sheria za urithi za Kiislamu zinasisitiza mgawanyo wa mali kwa warithi wengi. Hii ilisababisha mtaji kupunguzwa kwa kila kizazi, hali iliyosababisha biashara kuwa ndogo na kukosa uwezo wa kukua na kudumu kwa muda mrefu. Ukosefu huu wa uendelevu ulisababisha kudumaa kwa sekta ya biashara, huku uchumi wa nchi ukitegemea zaidi shughuli za viwanda vidogo na kilimo.

2. Ukosefu wa Mfumo wa Kibenki Imara

Sheria za Kiislamu zinazopiga riba zilisababisha maendeleo duni ya sekta ya benki. Hali hii ilifanya iwe vigumu kwa wafanyabiashara kupata mikopo ya kupanua shughuli zao. Matokeo yake, sekta ya kifedha ilibaki kuwa dhaifu, ikizidisha matatizo ya kiuchumi.

3. Udhaifu wa Mifumo ya Kisheria

Utegemezi wa ushahidi wa mdomo katika sheria za Kiislamu ulipunguza uaminifu katika mikataba ya biashara. Hii ilisababisha wawekezaji wa kigeni kuwa waangalifu, hali iliyozuia mtiririko wa uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI). Ukosefu wa uwekezaji uliathiri ukuaji wa viwanda, huku wafanyabiashara wakihangaika kupata ulinzi wa kisheria kwa mali zao.

4. Utegemezi wa Uongozi wa Kidini

Katika historia ya nchi nyingi za Kiislamu, viongozi wa kisiasa walitafuta uhalali kutoka kwa mamlaka za kidini. Hii ilizuia mageuzi ya kiuchumi, kwa kuwa mabadiliko yoyote yaliyoonekana kutishia ushawishi wa kidini yalipingwa. Matokeo yake, juhudi za kuimarisha uchumi zilikwama.

Tamaduni na Ubunifu: Sababu za Mkwamo wa Maendeleo

1. Kupungua kwa Ubunifu wa Kiteknolojia

Katika kipindi cha mabadiliko ya viwanda duniani, ulimwengu wa Kiislamu uliachwa nyuma. Marufuku ya mashine ya uchapishaji katika baadhi ya maeneo ya Kiislamu ni mfano dhahiri wa jinsi tamaduni zilivyozuia maendeleo. Wakati mataifa ya Magharibi yalikuwa yakichapisha vitabu na kusambaza maarifa, nchi nyingi za Kiislamu zilichelewa kujiunga na mapinduzi haya ya maarifa. Hii ilizuia maendeleo ya kielimu na kiuchumi, huku ulimwengu wa Kiislamu ukipoteza nafasi yake kama kitovu cha uvumbuzi.

2. Utamaduni wa Kudumu na Hali ya Mabadiliko Polepole

Muunganiko wa mamlaka za kidini na kisiasa ulisababisha tamaduni za nchi za Kiislamu kuwa sugu kwa mabadiliko. Maamuzi mengi ya kisiasa na kiuchumi yaliathiriwa na hofu ya kupoteza uhalali wa kidini, hali iliyosababisha maendeleo kuwa polepole au kutokuwepo kabisa.

Njia za Kutatua Changamoto Hizi

Ili kuboresha hali ya kiuchumi katika nchi zenye Waislamu wengi, juhudi za kina zinapaswa kufanywa kwa kuzingatia maeneo yafuatayo:

1. Mageuzi ya Sheria za Urithi

Kuweka mfumo wa urithi unaoruhusu mali za familia kubaki kuwa za umoja badala ya kugawanywa. Hii itasaidia biashara kukua na kudumu kwa vizazi kadhaa.

2. Kuimarisha Mfumo wa Kibenki

Kukuza mifumo ya kifedha inayofuata kanuni za Kiislamu lakini inayotoa suluhisho mbadala kwa riba, kama vile mikopo ya msingi wa hisa au ushirika wa faida na hasara.

3. Kuwekeza katika Ubunifu na Teknolojia

Kuanzisha sera zinazohamasisha uvumbuzi na matumizi ya teknolojia za kisasa. Mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuweka kipaumbele katika elimu ya sayansi na teknolojia ili kujiweka sawa na mataifa mengine.

4. Kutenganisha Dini na Siasa

Ingawa dini ina nafasi muhimu katika maisha ya kijamii, kuna umuhimu wa kutenganisha maamuzi ya kisiasa na ushawishi wa kidini ili kuwezesha mageuzi ya kiuchumi na kijamii.

5. Kuvutia Uwekezaji wa Kigeni

Kuimarisha mifumo ya kisheria ili kuongeza uaminifu kwa wawekezaji wa ndani na wa nje. Ulinzi wa mali za wawekezaji na mikataba yao utasaidia kuvutia mtaji unaohitajika kwa maendeleo ya viwanda.

Hitimisho

Changamoto za kiuchumi zinazokumba nchi nyingi za Kiislamu hazisababishwi tu na ukoloni bali pia historia ndefu ya masuala ya kitamaduni na taasisi. Ili kuboresha uchumi wao, nchi hizi zinapaswa kukumbatia mageuzi ya kimuundo na kiutamaduni, kuimarisha elimu, na kushirikiana na jamii ya kimataifa. Hii inaweza kusaidia kufungua mlango wa maendeleo endelevu na kurejesha nafasi yao katika uchumi wa dunia.
umeongea vizuri lakini hoja zako hazina msingi wowote, Uislamu umepanga taratibu zake vizuri na zikifuatwa zina matokeo chanya, na mambo yaliokatazwa yote yana athari mbaya, watu wengi wamefilisika kwa sababu ya riba na watu wengi wametajirika kutokana na utaratibu mzuri wa mirathi , na nyie wakristo ndio mnaongoza kwa kupigania mirathi
 
Nakubaliana na Weww Kabisa..
Ila Kumbuka Dubai na UAE inaongoza kuwa na Uchumi Mkubwa
Ukilinganisha na nchi za Afrika, ni kweli. Lakini ukilinganisha na nchi za Magharibi, UAE ipo kwenye kundi la kati. Mashariki ya kati, nchi zenye higest GDP per capita ni Qatar na Israel. Lakini kiteknolojia Israel ipo mbali sana ukilinganisha na Qatar au nchi nyingine yoyote ya Mashariki ya kati.
 
Mbona Tanzania pamoja nakua na waislamu majority 60% na viongozi walio lelewa na kukuzwa kwa maadili ya kiislamu wa zaziba r na bara bado tunapiga hatua kila mwaka, kiuchumi.......bigup Mama Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.........japo wengi wanaumia kulikubali kwamba hi nchi ni ya kiislamu kimya kimya, tamaduni nyingi tunazo fanya hapa kwetu ni za kiislamu kabisa.
Wewe, unaota. Tangu lini Tanzania ina waislam 60%?

Waislam kwa Tanzania, hawafiki hata 40%.

Here are some statistics on the religions practiced in Tanzania:
  • Christianity: 55.3% of the population practices Christianity

  • Islam: 31.5% of the population practices Islam

  • Traditional faiths: 11.3% of the population practices traditional faiths

    • Non-religious: 1.9% of the population is non-religious or adheres to other faiths
    • Roman Catholic: 27% of respondents in rural areas and 20.8% in urban areas identify as Roman Catholic
    • Hinduism: A minority religion practiced by about 50,000 people in 2010
    • Zanzibar: Islam is the most prominent religion on the Zanzibar archipelago, with 99% of the population identifying as Muslim
 
Ukilinganisha na nchi za Afrika, ni kweli. Lakini ukilinganisha na nchi za Magharibi, UAE ipo kwenye kundi la kati. Mashariki ya kati, nchi zenye higest GDP per capita ni Qatar na Israel. Lakini kiteknolojia Israel ipo mbali sana ukilinganisha na Qatar au nchi nyingine yoyote ya Mashariki ya kati.
Israel Ni nchi ya Kikristo????
 
Mbona Tanzania pamoja nakua na waislamu majority 60% na viongozi walio lelewa na kukuzwa kwa maadili ya kiislamu wa zaziba r na bara bado tunapiga hatua kila mwaka, kiuchumi.......bigup Mama Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.........japo wengi wanaumia kulikubali kwamba hi nchi ni ya kiislamu kimya kimya, tamaduni nyingi tunazo fanya hapa kwetu ni za kiislamu kabisa.
Acha Kujiongelesha wewe yaani umeandika kinyume chake eti waislam wengi kuzidi wakristo tz🤣🤣😂😂🙄🙄🙄🙄
 
Wewe
Hoja ni kwamba neenda kwenye website ya FBI na CIA uone nchi zinazo categorise kua na waislamu wengi Africa aTanzania ipo sensa ya CIA wanajua wenyew e waliifanya je mwaka 1965 waislamu Tanzania walikua 56% tangu huo mwaka waislamu hawaja ongezeeka unafikili na kufika 60%?
Wewe umejifungia pwani tembea uone acha kudanganya watu kilaza wewe utachekwa
 
Ukilinganisha na nchi za Afrika, ni kweli. Lakini ukilinganisha na nchi za Magharibi, UAE ipo kwenye kundi la kati. Mashariki ya kati, nchi zenye higest GDP per capita ni Qatar na Israel. Lakini kiteknolojia Israel ipo mbali sana ukilinganisha na Qatar au nchi nyingine yoyote ya Mashariki ya kati.
Kamba, UAE ingekua Ulaya still ingekua top 10 ya Nchi Tajiri per capita,

Screenshot_20241222-151546_Pixel Launcher.png

Kwenye data Za ulaya ingekua hapo no 7, na hata Ukiwa weka Uingereza (walijitoa EU ndio maana hawapo kwenye hizo data) inakua ya 8.

Kuiita nchi iliopita ujerumani, Italy, Spain, Ufaransa etc kwamba uchumi wake per capita ni wa kati kunazidi kuonyesha bias zako humu.
 
Ukilinganisha na nchi za Afrika, ni kweli. Lakini ukilinganisha na nchi za Magharibi, UAE ipo kwenye kundi la kati. Mashariki ya kati, nchi zenye higest GDP per capita ni Qatar na Israel. Lakini kiteknolojia Israel ipo mbali sana ukilinganisha na Qatar au nchi nyingine yoyote ya Mashariki ya kati.
Pia Israel haijaipita UAE gdp per capita, data za 2023 wamepitwa na 2024 Uchumi wa Israel umekongoroka sasa hivi hata 50K per capita hawafiki.
 
Back
Top Bottom