Kwanini ndizi mshare hazipatikani Kanda ya Ziwa?

Kwanini ndizi mshare hazipatikani Kanda ya Ziwa?

Uchagani haswa kwa warombo kila ndizi kule ina matumizi yake kwenye kupika. Matoke, mlali ,mshare ,kinairobi, nyoro, kitarasa ni favorite kwa mlo wa kawaida au machalari.

Halafu kunayo inaitwa mkonosi hii ni special kwa mtori/kiburu/kibulu na pia kuchoma au ku fry zikiwa mbivu na pia kutengeneza mbege.

Halafu kuna wanaziita kimulia na zenyewe ni suitable kwa mtori. Pia kuna ndizi mtotoo ambazo nadhani ni ng'ombe hizi ni best katika kutengeneza mbege . Doh nimepakumbuka huko.
Habarii mwanamaee..... Hbr yafo meku
 
ndizi matokeo Haina mpinzani.
Matoke ile ya Bukoba? Sijui wenyeji wanapendea nini! Nishazila mara kadhaa! Ladha yake sasa, unaona Bora unywe uji kuliko hiyo ndizi. Kwa aliyezoea MSHARE matoke ni "mabaya"
 
Nimeisha sana Kagera kiukwel nilipata shida kuzoea ndiz za kule.
Yaan wanakula mindiz fulan Mbeya tunaita eselya wao eti ndio ndiz yenye hadhi wakat Mbeya hayo mandiz tunawapikia Nguruwe.
Kuna Kambani za kuiva wao wanaita ndiz Sukari.
Kiukwel watu wa Kagera waje Mbeya kujifunza namna ndiz zilivyo .
Mindiz ya Kagera kwanza Haina Radha kabisa ila wao wanavyoyapenda sasa .
Wao ni ndiz maharage ,Au Magimbi mixer maharage.
Kiukwel watu wa mkoa ule hawajui vyakula vingi ,Hadi makande ya mahindi mabichi hawayajui kabisa.

Chakula kikuu Kagera ni Ndiz maharage ,Magimbi maharage ,mihogo maharage ,Wali maharage, tofaut na hapo hamna jipya.
Hata watumishi wa umma wakitoka ule mkoa wakaenda mikoa mingine hasa hii ya nyanda za juu kusin hawatak kabisa habar za kurudi kwao wanaona kama walikosa vitu vingi Sabab ya kuwa gizan .
Kuna Wilaya kama Misenyi ,Ngara ,Biharamulo ,ni Wilaya maskin sana Kwa ule mkoa na watu wa hizo Wilaya wanaish Maisha ya kizaman sana alaf wajuaj balaa wakat ukwel ni kwamba ni Washamba sana.
Uchafu sasa ndio usiseme hasa Wilaya ya Ngara wahangaza unakuta jitu linatema mate barabara Nzima .
Kamasi yanatolea mkono Tena mbele za watu.
Hovyo sana hao watu Sitaman hata kurud huo mkoa.
 
Mwanza, Shinyanga, Kahama, Geita, Kagera, na Kigoma! Kote huko sijawahi kukutana na ndizi mshare. Ndizi zinazopikwa maeneo tajwa ni ndizi ambazo kwa Arusha na Kilimanjaro, ukikuta mtu kazipika, ujue ni amekosa kabisa cha kupika. Si matumizi yake.

Nilikula ndizi kwa mara ya kwanza jijini Mwanza mwaka 2010. Nilishangaa nilipokuta ni ndizi ambazo kwa Arusha na Kilimanjaro zinatumika kwa kupikia mtori au kuvundikwa kwa ajili ya kutengenezea pombe. Nilikula kwa kuwa sikuwa na namna, isitoshe, nilikuwa ugenini na ziliandaliwa kwa ajili yangu.

Tokea nikiwa mdogo, nilikuwa nikijua kuwa ndizi zinazotumika kupikia "ndizi" ni NDIZI MSHARE, KIMALINDI, n.k., lakini si ndizi ng'ombe.

Ni kwa nini hizo ndizi hazipatikani Kanda ya Ziwa?
Zipo za Musoma ila kwa waatalamu waliotokea Moshi unajua apa umepigwa
 
Nakumbuka kipindi hicho naishi Mwanza nilikua nazipata soko kuu japo zilikua bei kidogo. Huwezi kupika mchemsho wa nyama na ndizi ukatumia bukoba ndizi mshare ndo inakua poa. Binafsi bukoba naitumia kwenye mtori kuila kawaida mara chache sana.
 
Nani kakuambia wakikosa ndizi ndio wanapikia mshare?
Mshare sio option ya mwisho, kimalindi ndio ya mwisho kabisa ila kutegemea na eneo mfano arusha Zina anza mshare then ndizi ngombe mwisho kabisa ndio kimalindi.
 
Tembea uone.

Mimi mpaka leo nashangaa hao wa rugaruga wana kula je hizo ndizi ngumu kama miogo, mwanzoni ni lidhani na kwa ajili ya walevi kukatia hungerover zao za pombe, mpaka nilivo ona mama mjamzito naye anazila ndo ni kajifunza kwamba.

Hujafa hujaumbika
Kama anavyoshangaa ndivyo nami nilishangaa Kilimanjaro wanavyokula ndizi ngumuuu eti hadi za kukaanga ndio hizohizo🙆🙆🙆
Unakula ndizi zinabaki zimesimama tumboni!! Halafu hazina hata ladha.
 
Kama anavyoshangaa ndivyo nami nilishangaa Kilimanjaro wanavyokula ndizi ngumuuu eti hadi za kukaanga ndio hizohizo🙆🙆🙆
Unakula ndizi zinabaki zimesimama tumboni!! Halafu hazina hata ladha.
Nachoona ni kawaida kila mmoja kuvutia kwake,
wala ndizi wa kagera wengi tunashangaa ndizi za k'njaro ngumu mbaya nyeusi, binafsi zilinishinda kabisa, mbeya ndizi zipo ila ni km hazina ladha, hizo mshale kwa bk zinaitwa nkonjwa zinapatikana sana kyaka ni ndizi adimu sana na hutumika kwa kukaanga au kuchoma sio kupika, kwa zilizobaki ndizi bukoba inatafutwa,
 
Back
Top Bottom