Kwanini nyumba ikifika hapa inakuwaga ngumu kumalizia?

Kwanini nyumba ikifika hapa inakuwaga ngumu kumalizia?

Nguvu ya kuanzia msingi hadi kwenye lenta inakuwaga ya kasi san,a kuanzia hapo hadi kumalizia wengi hurudi nyumba nini shida?

View attachment 3086249
Ukishabadilisha tu lugha kwenye ujenzi kutoka Kiswahili kwenda kiingereza ndipo mambo yanapoanza kuwa magumu.

Mfano; Najenga ukuta sasa hivi ni tofauti na kusema Nafanya "finishing" 🤣
 
Kwa sababu tunafosi kujenga.

Mimi nikishakuwa na bajeti ya gharama ya nyumba mpaka inaisha nikahakikisha kwamba kiasi hicho ninacho kwa muda huo ndio nitaanza kujenga.

Kujenga tuna ku overrate sana wakati ni process za maisha kama process zingine.

Kwa maisha yangu mimi pakukaa sio tatizo,tatizo vyanzo vys mapato ndio shida,ninachofanya ni kupambana nipate biashara safi nitoboe na hapo nitajenga within a few weeks mjengo unasimama.
Quote:
"........within a few weeks mjengo unasimama."
Mkuu; labda iwe ni nyumba ya mbao tupu. Kwa nyumba ya blocks sio rahisi kivile kwani kunahitajika pia muda wa kusubiri ili sementi ikomae e.g. lenta ni siku 7(Wiki 1)halafu katika hatua hiyo kama alivyosema mtoa mada, kuna vitu vinaingiliana au kutegemeana yan lazima viende kwa pamoja. lakini mafundi lazima wasubiriane e.g. :
1. Huwezi kupiga ripu kabla hujafanya wiring na kuweka mfumo wa maji ndani ya nyumba n.k.
2. Mafundi wanazingua sana- leo yupo kesho ana dharura
3. Wewe Tajiri pia unaweza kupata dharura e.g. kusafiri, kuugua n.k.
4. Hali ya hewa inaweza ikawa kikwazo e.g. mvua au upatikanaji wa maji n.k.
Kwa mantiki hiyo, ujenzi wa nyumba utaonekana kama unasuasua japokuwa kimchakato ni ujenzi unaendelea kwa kasi nzuri.
Mimi nadhani kama kila kitu kitakwenda sawa kama ulivyopanga i.e. mafungu yapo na mafundi wakawa waaminifu, ili nyumba (Jengo la kawaida) lisimame, muda sio chini ya miezi 6+.
 
Nguvu ya kuanzia msingi hadi kwenye lenta inakuwaga ya kasi san,a kuanzia hapo hadi kumalizia wengi hurudi nyumba nini shida?

View attachment 3086249

Si kweli ,watu wanatembea na nyumba mfukoni....Kuna Jamaa yupo State ,alikuja ndani ya miezi mitatu alimalzia mjengo kila kitu ,hakusimama hata hatua moja ilikuwa mwanzo mwenga kuanzia msingi kupaua ,finishing ,perving ,garden ,umeme ,maji ,fense.
 
Inakuwa ngumu kwa sababu ni sehemu inakutaka ufanye vitu viwili vyote kwa wakati mmoja...

Nikimaanisha huwezi kupaua ukaacha usubirie kupiga bati...ni lazima upaue na kuweka bati kwa wakati huo...Na hapo ndipo kipengele kinapoanzia..

Wakati huko kwingine una maamuzi...unaweza kuanza msingi...Ukapumzika ukajipanga kwa ajili ya Boma....Ukipadisha Boma kabla ya lenta unaweza kusubiri tena.. ukaweka lenta kabla ya kozi ya mwisho vile vile ukasubiria...
 
Mkuu ujenzi una maajabu unaweza kugombana na mafundi bure kama haupo site mda wote

Unaweza kupiga bajeti na ukazidisha lakini isitoshe kabisaa
Ndiyo ni kweli kabisa hususan pale inapotokea badiliko kwenye bei za vifaa, gharama ya usafirishaji, uaminifu na umakini wa mafundi.
Haiwezekani ukawepo site muda wote kama nyapara/msimamizi saa zote kwani wewe binafsi pia unayo majukumu mengine muhimu.
Halafu usisahau pia kwamba, kwa bahati mbaya baadhi ya vifaa vinaweza kuharibika e.g. kuvunjika kwa ceiling boards(Gypsum boards), sink za vyooni, Vioo au kitasa kuwa ni kibovu n.k. Tena inawezekana ukalazimika kubomoa sehemu fulani ambayo imejengwa vibaya au unataka kufanya maboresho katika ramani yako. Mambo ni mengi yanayoweza kuyumbisha bajeti ya awali kiasi kwamba ile 25% uliyoweka kama tahadhari ikaisha na bado isitosheleze.
 
Back
Top Bottom