SWALI LA DADA BEA ALILOULIZA JANA INBOX
Shalom mchungaji. Namimi naomba kuuliza. Kwanini biblia tunayotumia sisi ina vitabu pungufu ukilinganisha na ile ya kikatoriki?
Na kuhusu kuombea waliolala mauti ipo kwenye kitabu cha wakababayo(kama nakumbuka vizuri) nimesoma kwenye hio Biblia. Naomba kueleweshwa tafaadhali
JIBU LA MWALIMU CONRAD KWA FAIDA YA WOTE
Biblia ya vitabu 72 inakubaliwa na Kanisa Katoliki na ile yenye vitabu 66 inakubaliwa na makanisa ya Kiprotestanti. Hii ni kusema kuwa, kiujumla, vitabu vyote vilivyopo kwenye Biblia ya Kiprotestanti vimo kwenye Biblia ya Kikatoliki; lakini ile ya Kikatoliki ina vitabu 6 zaidi.
Vitabu 6 zaidi
Vitabu 6 vilivyomo kwenye Biblia ya Kikatoliki, ambavyo havimo kwenye ile ya Kiprotestanti ni hivi vifuatavyo:
1. Tobit
2. Judith
3. Maccabee 1 na Maccabee 2
4. Wisdom of Solomon
5. Ecclesiasticus (Sirach)
6. Baruch
Vitabu hivi viliingiaje?
Baada ya Wayahudi kutawanywa na Mungu kwenye mataifa mbalimbali nje ya Israeli kutokana na dhambi, wengi wao walizaliwa wakati dola ya Ugiriki (Uyunani) iliyoenezwa na Alexander the Great ilipokuwa ndiyo dola kuu kwenye dunia ya wakati ule. Kwa hiyo, wengi wao hawakujua Kiebrania. Matokeo yake ilionekana haja ya kuwatafsiria Biblia ya Kiebrania (Agano la Kale) katika lugha waliyoijua, yaani Kiyunani.
Wataalamu takribani 70 walikutana katika mji wa Alexandria, Misri, kwenye mwaka 200 KK na kuandaa Biblia yenye vitabu vyote vinavyopatikana kwenye Biblia ya Kiebrania. Lakini pia waliongezea vitabu hivyo 7 tulivyotaja hapo juu. Biblia hii imekuja kukubaliwa na Kanisa Katoliki pia.
Vitabu hivi viliachwaje?
Kufuatia mwenendo usio wa KiMungu uliokuja kujitokeza kwa miaka mingi ndani ya Kanisa Katoliki, baadhi ya watu, kama vile Martin Luther, walianza kuhoji mafundisho fulanifulani ya Kanisa Katoliki na pia vitabu hivyo 6 ambavyo havikuwamo kwenye Biblia ya Kiebrania. Mfano wa mafundisho yaliyohojiwa ni Kanisa Katoliki kusema kwamba mtu anaweza kutoa fedha kununua msamaha wa dhambi kutoka kwa Mungu kwa ajili yake au kwa ajili ya wafu wake, n.k.
Ilibainika kuwa vitabu hivi vina mafundisho potofu, hivyo haviwezi kuhesabika kuwa ni Neno la Mungu. Matokeo yake, Luther na wanamageuzi wengine waliamua kukubaliana na vitabu vilivyo kwenye Biblia ya Kiebrania na kuacha vile 6 vilivyoongezwa kwenye Biblia ya Alexandria (inayoitwa Septuagint).
Tofauti tu ni kwamba, Biblia ya Kiprotestanti ikawa ina vitabu 39 katika Agano la Kale ilhali ile ya Kiebrania ina vitabu 24. Hivi ni vitabu vilevile ila tu Biblia ya Kiebrania inaunganisha baadhi ya vitabu kama kitabu kimoja. Kwa mfano, vitabu 12 vya manabii ambavyo ni vidogovidogo (minor prophets), inavichukulia kama kitabu kimoja, lakini ni vitabu 12 tofauti kwenye Biblia ya Kiprotestanti.
Hebu sasa tuangalie vile vitabu ambavyo viliondolewa kwenye Biblia ya Kiprotestanti pamoja na baadhi tu ya upungufu wa vitabu hivyo uliosababisha kuondolewa kwake – lakini makosa na mapungufu yake ni zaidi ya haya yaliyoorodheshwa hapa:
TOBIT
Kitabu hiki ambacho kiliandikwa kwenye mwaka 726-722 K.K., kina mafundisho kadhaa kama vile hili linalosema:
For alms deliver from all sin, and from death, and will not suffer the soul to go into darkness. (4:8-11).
Yaani: Sadaka huokoa na dhambi zote, na kutoka kwenye mauti , na hazitakubali roho ya mtu iende gizani (yaani kuzimu).
Pia imeandikwa:
Prayer is good with fasting and alms more than to lay up treasures of gold: for alms delivereth from death, and the same is that which purgeth away sins, and maketh to find mercy and life everlasting (12:8-9).
Yaani: Kuomba ni kuzuri kama kukiambatana na kufunga na kutoa sadaka kuliko kujiwekea hazina ya dhahabu; maana sadaka huokoa na mauti, na pia hutakasa dhambi, na humwezesha mtu kupata rehema na uzima wa milele.
Kwa mtu yeyote anayemwelewa Bwana Yesu na mafundisho yake wala haihitaji ufahamu mkubwa sana kujua kuwa hiki si kitu cha kutoka mbinguni hata kidogo. Haya ni mafundisho kutoka sehemu nyingine kabisa!
USIKOSE SEHEMU YA 02