Kwa hiyo unapingana na Biblia inapoosema Yesu ni kuhani wetu mkuu, yu hai siku zote akituombea? Waroma kwa kupotosha Biblia mmekubuhu hata aibu hamna?
Ndugu yangu baki kwenye siasa huku unapwaya sana. Waandishi wa vitabu vinavyounda Biblia ni wengi lakini unajua akina nani walichambua vitabu vyote wakaona hivyo unavyojua leo ndio vinastahili kuwekwa pamoja? Unajua injili zilikuwepo nyingi na sio nne tu unazoona leo?Hii makala au riwaya ina walakini mwingi na haina mantiki kabisa! Mwandishi anapaswa kujua kuwa Bibilia haikuandikwa na mtu mmoja,na ilikuwa kazi ya watu wengi mno kutafisiri lugha ya michoro ya zamani ili kupata maana
Luther hakuwa na hoja yoyote na Bibilia as alikuja kuisoma Biblia ukubwani sana,wakati huo Wakatoliki walikuwa na Mithali/Misali za waumini ambayo ni kama Biblilia iliyochujwa sana,ni Bibilia halisi ndio ikimfungua Luther hadi akaona mistari inayosema kuwa kwa kupigwa kwake Yesu sisi tumesamehewa bure,qakati huo msamaha ulikuwa unatolewa kwa fedha! Unalipa ndio upate msahama
Umetoa wapi hili fundisho? Au ndio umeamua kuamini unachotaka?Watu wakishashiba makande bwana, watataka kutunisha matumbo yao ili watu waone la nani ni kubwa kama wale jamaa zangu wa Ethiopia wanaotembea chululu zipo nje![emoji23][emoji23]
All in all dini zilikuja kwa mashua tu, kinachopaswa kufuatwa ni imani thabiti ya mtu.. ukimwamini Mungu, ukaacha uovu, inatosha hayo mengine tuwaachie Wajerumani na Waitaliano.
Nmeamua kuamini nnachotaka😊
Ndugu yangu baki kwenye siasa huku unapwaya sana. Waandishi wa vitabu vinavyounda Biblia ni wengi lakini unajua akina nani walichambua vitabu vyote wakaona hivyo unavyojua leo ndio vinastahili kuwekwa pamoja? Unajua injili zilikuwepo nyingi na sio nne tu unazoona leo?
Nani aliamua mpangilio wa hivyo vitabu? Kianze kipi, kifate kipi hadi ufunuo? Walitumia utaratibu upi kupata mpangilio? Unajua biblia unayotumia leo mpangilio wa chapters umewekwa mapema karne ya 13 na Askofu Steven Langton na chapters za bible zimewekwa kwa verses baadae kabisa! Zote hizi ni kazi za Kanisa Katoliki ambalo ndio lilisimamia michakato yote na kupitisha matumizi yake kwa waamini.
Usisahau kazi hii yote inafanyika hakuna makanisa ya kilokole zaidi ya Kanisa Katoliki ambalo baadae liligawanyika na kuzaliwa Orthodox church ambalo pia ni apostolic church.
Kanisa ni moja tu, ndio maana hutokaa usikie makanisa ya Katoliki maana Kristo hakusema atajenga makanisa yake bali atajenga Kanisa lake! Kanisa Katoliki! Ndio alama pekee ya kanisa la Kristo ulimwenguni tukiamini imani moja, ubatizo mmoja na mchungaji mmoja.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu wanadanganya pia kuwa madhehebu yote yametoka kwenye ukatolik. Nadhani ndo wanavyodanganywa huko.Usisahau siasa ndio inaratibu maisha yetu ya kila siku
Hitimisho lako kuwa Biblia imeandikwa na Wakatoliki ni upotoshaji mkubwa.
Mosi.Bibilia ya kwanza inasadikiwa iliandikwa kwa lugha ya Armaic hii ni lugha ya eneo la Mashariki ya Kati pamoja na pembe ya Afrika,ni miongoni mwa lugha za kwanza kuandikwa zaidi ya miaka 4500 iliyopita
Pili.Ukiristo kwa ujumla wake umeanza miaka 2000 baada ya ufufuo wa Yesu Kristo na ndio wakati Agano la jipya,tafsiri yake ni kuwa Ukatoliki umeanza karne ya kwanza yaani baada ya Yesu kufufuka
Tatu.Dini ya kwanza ya iliyotimia Bibilia ni Judaism ambayo ilianza miaka mingi kabla ya Yesu
Bikra Maria amebarikiwa , ni kweli ,hakupewa kazi ya kuombea watuMimi ni mkatoliki, nilibatizwa mwaka wa 1970, nilizaliwa mwaka 1968 NA sasa Nimefikisha miaka 50 na miezi kadhaa. Kwa kweli niseme tu, hizo kashifa dhidi ya kanisa letu hazikuanza Leo, zipo tangu zamani miaka ya nyuma sana na ziliasisiwa miaka 1880 NA waprostetant wa karne hizo NA baadaye walikuja wasabato akina Helen white na baadaye kabisa walikuja mathehebu ya kilokole ambapo mpaka wanaendeleza chuki zao NA kashifa zao dhidi ya kanisa NA Pope Francis.
Mimi nilibahatika kusoma baadhi ya nyaraka au vitabu mbalimbali vinavyoelezea historia ya mapapa NA ukatoliki, pope wa Kwanza kabisa ambaye kaburi lipo Vatican City pale Saint Peters Busilica, alikuwa mtume PETRO NA baadaye wengi wamekuja NA kuondoka duniani maana duniani tunapita tu, makao yetu ni mbinguni kwa Baba. Kuna suala LA kuwaombea materemu, waprotestanti wanalipinga hilo, lakini wanasahau kusoma MT 12:32, kumbe upo msamaha baada ya kifo. Kwahiyo, sisi hutuabudu sanamu na wala hatumtegemei mwanadamu kuishi bali tunayo SALA YA BABA YETU rejea misale ya waamini ambayo hiyo sala imerejea andiko LA biblia Mt 6:9-13.
Kuhusu sala ya bikira Maria, sisi hatumwabudi bali tunamwamba kupitia tu kwake kwa kuwa MUBGU mwenyewe kupitia malaika akimtamkia kuwa amebalikiwa NA kupewa NEEMA na Bwana NA Bwana yu pamoja naye na atamzaa MTOTO mwanaume NA jina lake ni YESU, mwana wa aliyejuu, Mungu mkuu rejea Lk 1:26-31, Isa 7:14, 9:6, MT 1:21-23, Lk 1:30-35.
Pia, Mama bikira watu walikuwa wakimfuata kumwomba amwambie mwanaye awatekelezee mahitaji yao, rejea wakati wa harusi ya Kana, hata DIVAI ilipokuwa ilipokuwa imewatindikia kwa biblia ya kiingereza by Gideon anasema when the wine ran out, the mother of Jesus said to the Jesus, they have no wine and Jesus said to his mother, my hour has not yet come and mother told the servants do whatever he tells you, Ina maana hawa watumishi wa waliomba kupitia kwa mama Maria na Yesu alifanya muujiza kwa kubadili maji kuwa divai, Yn 2:1-11.
Kwa Leo naishia hapa, nitaendelea tena kujibu hoja kwa kadiri MUNGU atakavyoniongoza.
Kulikuwa na madhehebu gani?Kuna watu wanadanganya pia kuwa madhehebu yote yametoka kwenye ukatolik. Nadhani ndo wanavyodanganywa huko.
Ukweli ni kuwa ukatolik ukishirikiana na serikali ulikandamiza madhehebu mengine na kuwaua waumini wake , hivyo kupelekea kutokuabudu waziwazi
Na baada ya upinzani kutoka ndani yao wenyewe kwa wenyewe, ikashindikana kuthibitiana ndio madhehebu mengine yakaanza harakati zake waziwazi
Wakatolik hawakuandika biblia yoyote. Kwanza hawapendi watu wasome biblia kwa kuwa mambo mengi wanayofanya hayaendani nayo
Kwamba vitabu vya agano jipya vilikuwako kabla hata Kristo kuzaliwa [emoji16] . Unajua leo Petro, Paulo achili mbali akina Musa ukiwaambia una bible ambayo unaiamini watakuona kichaa! Hata hilo neno bible hawalijui yaani [emoji16].Usisahau siasa ndio inaratibu maisha yetu ya kila siku
Hitimisho lako kuwa Biblia imeandikwa na Wakatoliki ni upotoshaji mkubwa.
Mosi.Bibilia ya kwanza inasadikiwa iliandikwa kwa lugha ya Armaic hii ni lugha ya eneo la Mashariki ya Kati pamoja na pembe ya Afrika,ni miongoni mwa lugha za kwanza kuandikwa zaidi ya miaka 4500 iliyopita
Pili.Ukiristo kwa ujumla wake umeanza miaka 2000 baada ya ufufuo wa Yesu Kristo na ndio wakati Agano la jipya,tafsiri yake ni kuwa Ukatoliki umeanza karne ya kwanza yaani baada ya Yesu kufufuka
Tatu.Dini ya kwanza ya iliyotimia Bibilia ni Judaism ambayo ilianza miaka mingi kabla ya Yesu
Unaweza tupa Mifano ya hayo nadhehebu na hizo serikali?? Ukishasema dhehebu(denomination) maana yake imetoka mahali....unless hujui maana ya dhehebu.....Ukweli ni kuwa ukatolik ukishirikiana na serikali ulikandamiza madhehebu mengine na kuwaua waumini wake , hivyo kupelekea kut
Hii ni kwa mujibu wako....Wakatolik hawakuandika biblia yoyote.
Hivyo wao kutokupenda wao watu wasome biblia ndio Kanata uhalali was wao kutoku-compile bibliaKwanza hawapendi watu wasome biblia kw
Kwamba vitabu vya agano jipya vilikuwako kabla hata Kristo kuzaliwa [emoji16] . Unajua leo Petro, Paulo achili mbali akina Musa ukiwaambia una bible ambayo unaiamini watakuona kichaa! Hata hilo neno bible hawalijui yaani [emoji16].
Vitabu vya Bible vimekusanywa, kuhalalishwa karibia karne baadae. Wakristo toka awali hawakuwa na kitabu kama hiki ukichonacho leo. Hujiulizi nani alijipa mamlaka ya kuchagua injili, nyaraka tena nyingi zikachukuliwa za St Paulo akapanga mtiririko wa vitabu iweje, chapters, verses! Mnafikiri vilishuka tu kama quran ya wenzetu?
Nenda kafatilie mtaguso gani ulipitisha Bible na ilikuwa dhehebu gani na wakati huo yalikuwepo madhehebu mengine? Nitajie majina ya hayo madhehebu hapa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani leo mitume mfano wakifufuka mnafikiri wataingia kanisa lolote tu kisa kuna mapambio? Watataka kujua warithi wa nafasi zao toka awali, alafu watafatilia namna imani ilivyorithishwa hadi leo ili walitambue kanisa la Kristo. Maana ahadi ya Kristo ni kujenga Kanisa lake na si kujenga makanisa yake.
Yaani Paulo akiingia Kanisa Katoliki anaweza kuendesha misa yaani [emoji16] maana taratibu ni zile zile toka Kanisa la kwanza kama ilivyoandikwa kwenye matendo ya,mitume, ibada ya neno alafu kumega mkate! Yaani Kristo alitupa sababu moja kuu ya sisi Wakristo kukutana, kumega mkate!
Sent using Jamii Forums mobile app
SWALI LA DADA BEA ALILOULIZA JANA INBOX
Shalom mchungaji. Namimi naomba kuuliza. Kwanini biblia tunayotumia sisi ina vitabu pungufu ukilinganisha na ile ya kikatoriki?
Na kuhusu kuombea waliolala mauti ipo kwenye kitabu cha wakababayo(kama nakumbuka vizuri) nimesoma kwenye hio Biblia. Naomba kueleweshwa tafaadhali
JIBU LA MWALIMU CONRAD KWA FAIDA YA WOTE
Biblia ya vitabu 72 inakubaliwa na Kanisa Katoliki na ile yenye vitabu 66 inakubaliwa na makanisa ya Kiprotestanti. Hii ni kusema kuwa, kiujumla, vitabu vyote vilivyopo kwenye Biblia ya Kiprotestanti vimo kwenye Biblia ya Kikatoliki; lakini ile ya Kikatoliki ina vitabu 6 zaidi.
Vitabu 6 zaidi
Vitabu 6 vilivyomo kwenye Biblia ya Kikatoliki, ambavyo havimo kwenye ile ya Kiprotestanti ni hivi vifuatavyo:
1. Tobit
2. Judith
3. Maccabee 1 na Maccabee 2
4. Wisdom of Solomon
5. Ecclesiasticus (Sirach)
6. Baruch
Vitabu hivi viliingiaje?
Baada ya Wayahudi kutawanywa na Mungu kwenye mataifa mbalimbali nje ya Israeli kutokana na dhambi, wengi wao walizaliwa wakati dola ya Ugiriki (Uyunani) iliyoenezwa na Alexander the Great ilipokuwa ndiyo dola kuu kwenye dunia ya wakati ule. Kwa hiyo, wengi wao hawakujua Kiebrania. Matokeo yake ilionekana haja ya kuwatafsiria Biblia ya Kiebrania (Agano la Kale) katika lugha waliyoijua, yaani Kiyunani.
Wataalamu takribani 70 walikutana katika mji wa Alexandria, Misri, kwenye mwaka 200 KK na kuandaa Biblia yenye vitabu vyote vinavyopatikana kwenye Biblia ya Kiebrania. Lakini pia waliongezea vitabu hivyo 7 tulivyotaja hapo juu. Biblia hii imekuja kukubaliwa na Kanisa Katoliki pia.
Vitabu hivi viliachwaje?
Kufuatia mwenendo usio wa KiMungu uliokuja kujitokeza kwa miaka mingi ndani ya Kanisa Katoliki, baadhi ya watu, kama vile Martin Luther, walianza kuhoji mafundisho fulanifulani ya Kanisa Katoliki na pia vitabu hivyo 6 ambavyo havikuwamo kwenye Biblia ya Kiebrania. Mfano wa mafundisho yaliyohojiwa ni Kanisa Katoliki kusema kwamba mtu anaweza kutoa fedha kununua msamaha wa dhambi kutoka kwa Mungu kwa ajili yake au kwa ajili ya wafu wake, n.k.
Ilibainika kuwa vitabu hivi vina mafundisho potofu, hivyo haviwezi kuhesabika kuwa ni Neno la Mungu. Matokeo yake, Luther na wanamageuzi wengine waliamua kukubaliana na vitabu vilivyo kwenye Biblia ya Kiebrania na kuacha vile 6 vilivyoongezwa kwenye Biblia ya Alexandria (inayoitwa Septuagint).
Tofauti tu ni kwamba, Biblia ya Kiprotestanti ikawa ina vitabu 39 katika Agano la Kale ilhali ile ya Kiebrania ina vitabu 24. Hivi ni vitabu vilevile ila tu Biblia ya Kiebrania inaunganisha baadhi ya vitabu kama kitabu kimoja. Kwa mfano, vitabu 12 vya manabii ambavyo ni vidogovidogo (minor prophets), inavichukulia kama kitabu kimoja, lakini ni vitabu 12 tofauti kwenye Biblia ya Kiprotestanti.
Hebu sasa tuangalie vile vitabu ambavyo viliondolewa kwenye Biblia ya Kiprotestanti pamoja na baadhi tu ya upungufu wa vitabu hivyo uliosababisha kuondolewa kwake – lakini makosa na mapungufu yake ni zaidi ya haya yaliyoorodheshwa hapa:
TOBIT
Kitabu hiki ambacho kiliandikwa kwenye mwaka 726-722 K.K., kina mafundisho kadhaa kama vile hili linalosema:
For alms deliver from all sin, and from death, and will not suffer the soul to go into darkness. (4:8-11).
Yaani: Sadaka huokoa na dhambi zote, na kutoka kwenye mauti , na hazitakubali roho ya mtu iende gizani (yaani kuzimu).
Pia imeandikwa:
Prayer is good with fasting and alms more than to lay up treasures of gold: for alms delivereth from death, and the same is that which purgeth away sins, and maketh to find mercy and life everlasting (12:8-9).
Yaani: Kuomba ni kuzuri kama kukiambatana na kufunga na kutoa sadaka kuliko kujiwekea hazina ya dhahabu; maana sadaka huokoa na mauti, na pia hutakasa dhambi, na humwezesha mtu kupata rehema na uzima wa milele.
Kwa mtu yeyote anayemwelewa Bwana Yesu na mafundisho yake wala haihitaji ufahamu mkubwa sana kujua kuwa hiki si kitu cha kutoka mbinguni hata kidogo. Haya ni mafundisho kutoka sehemu nyingine kabisa!
USIKOSE SEHEMU YA 02