Maonyesho yote mimi niliyaona ni upuuzi na matumizi mabaya ya raslimali tu; ni afadhali Magufuli aliyefuta sherehe hizo na kuelekeza pesa hizo kujenga barabara ya Morocco , na sote leo tunajua matokeo yake. Kuonyeshana silaha za zamani za kivita na mbinu za kizamani sana ni ulimbukeni mkubwa sana. Kwani kama wangefanya gwaride la kawaida na maonyesho ya kawaida kabisa yasiyokuwa ya kuonyeshana silaha na uwezo wa kijeshi wangepungukiwa nini? Mwaka 1979 ndege mojawapo ya hizo shenyang J-5 ilikuwa ikifanya maonyesho kama hayo hayo ya kijeshi ikaanguka mbele ya Nyerere pembeni mwa chuo cha Chang'ombe; nadhani mnara ule bado upo. Kama ndege hiyo ilianguka kwa mechanical failure miaka zaidi ya 40 iliyopita, mnaimani vipi kurika leo mbele za umati namna ile. Ndege za kivita za Jeshi ni zile zilizoachwa na Nyerere, sidhani kama Airforce imewahi kupata ndege mpya za kivita miaka ya hivi karibuni. najua hata Kenya bado wana ndege za kizamani F-5 lakini sijawaona wakizionyesha hadharani kwa mbwembwe kama tulivyofanya sisi.