Kwanini Polepole halioni hili? Ni makusudi au bahati mbaya?

unafanya cherry picking, H.Polepole hajaongelea hilo tu, bali kaongea mengi na kufafanua kwa utulivu na unyenyekevu mkubwa na kutoa sababu za msingi za kwa nini uraisi uliopo ni wa mpito …
TAnzania haina urais wa mpito
 
This is exactly 100%
 
vipi kuhusu suala la uvunjifu wa katiba uliofanywa na CCM kwa katiba ya Tanzania na ya CCM kwa ujumla? Unalizungumziaje hili?
 
Ukiwaambia watu situation ya SSH kuingia madarakani. Hata huko CCM hawakuwahi kudhani kama itaweza tokea situation ya namna ile.

Ndo maana hakuna muongozo maalumu unaoeleza nini kifanyike ndani ya chama chao.


Wanatakiwa kukubali kwamba huyu ni Mgombea wao



Na wanaosema taratibu hazijafatwa --- ni kwa sababu wezi wanajuana sasa ikifika muda wanataka kuibiana inabidi waviziane 😁


Toka siku anaapishwa hii hali ya hapa 2025 likikua jambo la wazi lazima liwe la mshikemshike



Hata polepole ni tapeli anayepambania kikosi chake -- waendelee kutoana damu tu sisi tupo nao mpaka mwisho
 
Kasema asemi sana analinda KIAPO inabidi tumuelewe na tusimamie hapo
 
Mkuu my fellow learned brother Advocate Petro E. Mselewa, kwanza forgive me, naomba unikumbushe LL.B yako ni ya chuo gani? na LL.M yako ni ya chuo gani?.
P
Nimekuuliza hivyo kwasababu Polepole ni akili kubwa, hivyo msomi wa sheria wa level ya ubobezi ukielekea ubobevu, ulipaswa kuwa na uwezo mkubwa wa uelewa kumuelewa Polepole Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?

Kwenye uendeshaji chama kuna kitu kinachoitwa katiba, sheria, taratibu na kanuni, pia kuna miongozo na desturi na utamaduni.

Katiba, sheria, kanuni na miongozo, zinaandikwa kwa maandishi, taratibu, desturi na utamaduni, zinapangwa na kutekelezwa kwa mazoea tuu bila ya kuandikwa. Mfano akitoka rais Muislamu, anaingia Mkristu.

Mtu ukiisha kuwa kwenye zile nafasi za juu za uongozi, Rais, VP, PM, Spika na JM, hutakiwi kuja kugombea urais, utakatwa na vikao!.

Enzi za Nyerere, John Malechela akiwa Makamo Mwenyekiti Bara, aligombea urais ile 1985, wakati wa kikao cha CC kuwajadili wagombea, wagombea ambao ni wajumbe, wanatakiwa watoke nje wajadiliwe, Mzee Malecela akaamka kutaka kutoka nje, Mwalimu Nyerere akasimama na kumsimamisha kwa kumuita We Joni, unakwenda wapi?, sisi ndio viongozi tunao wajadili hawa, wewe utaondokaje?, akaamuru fomu ya Malecela iondolewe kwenye wagombea, kaa chini!.

That was it.

Baada ya kufa JPM Samia kuchukua nchi, ilitazamiwa Samia awe ni rais tuu wa mpito kukamilisha ngwe ya JPM, 2025 wajitokeze wengine.

Kwa vile Samia tayari aliisha wahi kuwa VP, aliposhauri 2025 twende na mwanamke, ilidhaniwa ni mwanamke mwingine yeyote Pre GE2025 - Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! tena tukashauri Pre GE2025 - Ukimuondoa Rais Samia, kama ni lazima awe mwanamke, then mwanamke huyo ni Dkt. Tulia, ameonesha uwezo, anaweza! Tumchagize au tuache tu bora liende?

Na kitu kizuri, hata rais Samia mwenyewe tumemuandikia barua, personal letter kumshauri Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

P
 
Hapa tumeona tatizo kwenye katiba,..katika katiba Mpya ingefaa Rais ambaye yupo madarakani akifariki,mtu atakae chukua nafasi yake Akaimu nafasi Ya urais Kwa muda tu then nchi iingie katika uchaguzi Mkuu,sio kumaliza miaka yote iliyobaki,.kua na rais Kwa miaka 4 Wakati hajachaguliwa na wananchi sio sawa..
 
Polepole anasema aliyewahi kuwa makamu wa rais haruhusiwi kugombea urais sio kuwa rais. Hapo samia alikuwa makamu kwa mujibu wa katiba ya nchi akawa rais sio wa kuchaguliwa sasa hapa amemalizia muda wake haruhusiwi kugombea urais.
 
Samia alichaguliwa na wananchi-- katiba ndivyo inavyosema, makamu anachaguliwa pamoja na rais
 
Polepole anasema aliyewahi kuwa makamu wa rais haruhusiwi kugombea urais sio kuwa rais. Hapo samia alikuwa makamu kwa mujibu wa katiba ya nchi akawa rais sio wa kuchaguliwa sasa hapa amemalizia muda wake haruhusiwi kugombea urais.
Kwenye chama cha ccm tupe muongozo unaozungumzia. - scenario ya makamu akipanda kuwa rais kwenyw uchaguzi ujao wanatakiwa wafanye nini?
 
Sina maana ya kupuuza hoja za Polepole kwamba uteuzi wa mgombea wa CCM umefanywa bila kufuata utaratibu na pengine hata katiba ya CCM na ya nchi (Rev. Dr. Malisa anatoa hoja kwamba kuanza kampeni -kimsingi nomination ni kuanza kampeni- kabla ya bunge kuvunjwa ni kuvunja katiba).

Ila, Polepole anaweza kuwa na hoja nzuri upande mmoja na hoja dhaifu upande mwingine. Hoja ya kusema uteuzi umeharakishwa na haujafuata utaratibu ni muhimu. Kiukweli kuteua mgombea kwa jina moja, kwa mkutano wa ambush vile, ni jambo la aibu.

Ila, Polepole anaweka hoja zake kwa namna inayoweza kuhojiwa kirahisi, na kuonekana kuwa licha ya maneno yote hayo, anayasema si kwa sababu ya ombwe la uongozi (kama anavyodai) bali kwa sababu hamtaki mgonbea ana wake mwingine. Which is not a crime.

Kwangu mimi, habari nzima ya chama kuendeshwa kwa desturi ni ujinga. Chama au nchi havitakiwi kuendeshwa kwa desturi, vinaendeshwa kwa katiba na kanuni zilizoandikwa.

Kwa sababu habari za desturi na utamaduni hazijaandikwa. Hazina clarity. Hatujui zimewekwa na kikao gani, na hivyo siku tukiona hazifai zimepitwa na wakati tunataka kuzibadilisha, hatuna kikao cha kuzitengua.

Pia habari za desturi na utamaduni ni chaka la kujiwekea arbitrary objections kwa watu usiowataka, na kuwaachia unaowataka. Kuweka ubaguzi usio wazi.

Kama kuna utamaduni ulio muhimu sana, uwekwe kwenye katiba kwa maandishi, uwekwe na vikao rasmi, tujue watu wakitaka kuuondoa wakae vikao gani kuuondoa. Habari iwe wazi mtu anapojenga hoja aweze kujenga hoja kwa vifungu vya katiba, si maneno tu ya "utamaduni na desturi" ambayo hayajaandikwa popote.
 
Kama anamalizia awamu ya 5 ambayo iliachwa wazi na Hayati Mag, Inakuwaje wanasema ni awamu ya 6, au ni mtu wa 6 kuwa Rais wa TZ ndo maana halisi ya awamu!?
 
Unataka Samia amalizie miaka mitano wakati Samia alichukua uongozi kwa bahati mbaya na huu ndo mwaka wa nne ...Mwanasheria msomi kama wewe bado hujui tu kuwa huu ulikua utawala wa awamu ya Sita kwa kinyongo chake Samia akaibadili na kuita awamu ya sita wakati mwenye awamu ya tano alifariki na Samia yeye na Magu walikuwa wanamalizia ngwe yao ya awamu ya tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…