Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Unajuaje! ?Labda angekuja kuwa Putini wetu. huoni alishaanza kuonyesha dalili za kutetea wanyonge! ?
Kama huna cha kunijibu usinijibu ujinga mimi sio mtoto mwenzio, huyo Putin na wanyonge wanakujaje hapa!?
 
Dah! Mkama Sharp alishavuta!
Udongo unameza si mchezo.

Yap Mkuu na Jeshi la Police halitawahi kuja kuwa na ' Askari ' mahiri, mpambanaji na very committed kama Marehemu Nkama Sharp na labda ningeshauri tu Jeshi la Police liwe linatumia ule ' ujuzi ' na ' umahiri ' wa Nkama Sharp katika kuweza kuwajenga hawa Askari Police wetu wa sasa ambao kimsingi binafsi naona hawajafikia hata tu 25% ya uwezo aliokuwa nao Nkama Sharp na laiti Marehemu angekuwepo hadi leo Jeshi la Police lingeheshimika mno. Ombi kungekuwa na siku ' maalum ' ndani ya Jeshi la Police ya kumuenzi Marehemu Nkama Sharp. ' Masela ' tulinyooka mno enzi zake!
 
ndio unavyojidanganya hao uliowataja kila siku wako IBIZA au kwenye Private Jet zao kwenda kula raha. wanaopost na kuendesha hizo account zao za social media ni ****** kama mimi na wewe kwa ujira mdogo
Wee kibwengo usijifananishe na mimi nyambafu wee.Usitaje ibiza tuu,taja na Ipanema,Copa Capbana na kwingineko,mara ngapi tunawaona na tabs,laptops nk,unafikiri wanakuwa wanafanya nn zaid? Akili yako imefungwa kwenye chips yai wee kijibwaa tuu,nenda kwa jike supa lako likakupime tezi dume,bahau weee
 
Alikuwa konda, Na o level ilifutwa kuanzia hapo
 
Daaah umenikumbusha mkuu enz zetu tukiwa vijana unalazimika kujifunza karate ili konda akizingua anakula nakozi hapoo ilikuwa mboga moto mchuz moto
 
ndio akili yako ilipoishia hapo halafu eti mnajiita watu wazima wa JF. kweli Njaa Mwanaharamu
 
Sijui unaongea nini, lini JF iliundwa ili iwe ya watu wa umri fulani? Sijui umeshawahi kufuatilia baadhi ya maneno ya rais katika hotuba zake, anaongelea/ anajibu yanayojadiliwa humu, hivyo si ajabu yumo humu
Ndio umeandika nini sasa. Social Media zina Umri wake ukishaona umegonga forty six na upo humu jua upstairs hauko vizuri. Wamama watu wazima wakivaa vimini au wababu waakipiga mlegezo na kutinga club mnaona mmomonyoko wa Maadili ila vizee kuja kushindana na vijana humu mnaona poa tuu. Busara zinahitajika kwenye familia yenu umri wa kujenga nchi umeshawapita tulieni majumbani na muwafundishe watoto na wajukuu zenu wasijekupotea kama mlivyopotea nyinyi
 
Mkuu we acha tu, enzi hizo za beach party na sealeander pink coconut club kumekucha ilibidi hadi pamba kali tuwe tunaazimana za kwenda kupigia bakora.
Mkuu we acha tu, enzi hizo za beach party na sealeander pink coconut club kumekucha ilibidi hadi pamba kali tuwe tunaazimana za kwenda kupigia bakora.
 
Mimi nilikuwa R 1990 na 1991 na lebo yetu ilikuwa nyekundu. Sisi ndio tuliokuwa wa kwanza kutumia mikondo kwa herufi, waluotutangulia walitumia majina ya ama 'Science' au ' 'Commerce'.

Vv
Ulimaliza form four lini?, maana kuanzia miaka ya ya 90 U na Z ndio yalikuwa madarasa ya commerce na form one Z lilikuwa linapaka na UVCCM tawi la TSS na kisha linapakana na U
 
Kwa hiyo puza akachezea KO!!
Hakuja kulipa kisasi?

Hakulipa kisasi watu waliomba msamaha mapema Na dogo alisepa mbaali Sana siunajua miaka hiyo hata kupata pesa ya shati sio mchezo Ada yenyewe ilikuwa 5000 Na tunakula Tambaza. Shule zikifungwa watu wanakonda.
 
Ulimaliza form four lini?, maana kuanzia miaka ya ya 90 U na Z ndio yalikuwa madarasa ya commerce na form one Z lilikuwa linapaka na UVCCM tawi la TSS na kisha linapakana na U
Nilimaliza 1991, enzi ya double session nilikuwa group B, hayo madarasa U na Z hayakuwa kwenye group B. Sisi madarasa yetu yalikuwa L, M, N, P, Q, na R.

Mwalimu wetu wa darasa alikuwa Maliki. Baadhi ya walimu waliofundisha darasa letu ni Ntambi, Hatibu, Mchwampaka, Temba, na Faustin. Mkuu wa shule aliyempokea Mzee Kisamo aliitwa Kwayu, msaidizi wake ni L. Luiwana ( Mzee Meja) ambaye 1991 alihamishiwa Same Secondary .

Vv

Vv

Vv
 
Duh kumbe tumechanganya madesa, naona wewe unazungumzia Aza boy na sio Tambaza, Ok nimekusoma mkuu, kwa Tambaza R lilikuwa darasa la Science
 

mazee umenikumbusha sie miaka ya 1990s sie bado wadogo siku ikicheza tambaza na jitegee au azania pale don bosco inabd kufungiwa ndani... tambaza wanakimbia na minyororo na mabumu ya chupa.. mara tukasikia walimchomaga mama mjamzito na bisibisi.. tulikua tunasoma pale muhimbili siku wakijisikia wanatusaidia tukicheza umitamshumta ... siku nyingine watupe makonzi.... barabarani wakikikuta wanakwambia fungua tuone lebo...aisee!!!
 

ohooo nyie ndo wale mlikua mnakuja kantini pale muhimbili mnatupa makonzi kinoma hlf mnakula chips zetu.. mkazuaga bonge la timbwili pale ule ukuta ulivyojengwa.. ijumaa moja mkazuiwa wote kutoka nje ya shule na askari kibao wengine wakajifanya kuvaa kanzu wanaenda msikitini..sie tulikua tunaona muvi kupitia vitobo ghorofani.. ila tulikua tunawafagilia maana tulikua hatuonewi kwenye umitashumta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…