Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Wewe si ulikoswakoswa kupigwa mtama karibu na Azania? Kama nakukumbuka hivi
 
Wakati ule puza ulikuwa tishio kwa migomo,fujo baina ya Shule Na shule .nilikuwa Na mwalimu alikuwa anaitwa otieno ulikuwa Mwl.mkuu musoma alliance kama ulikuwa mkorofi shuleni ulikuwa huwezi kuendelea Na masomo kwani ndiye alikuwa mkuu wa body selection.lakini sidhanii kama ndio ulikuwa sababu zaidi ila kuna makosa nafikiri aliyafanya akawa anatafutwa.
 
.....acha kuua soo kipusti we chocolate!...

Naona umeamua kuja na ID nyingine! Kweli GENTAMYCINE ni homa ya jiji humu JF yaani mpaka ' naogopwa ' na Watu wanaona njia pekee ya kuzima ' moto ' wangu ni kunishambulia kwa ma ID's mbalimbali lakini pamoja na ' mbinu ' zote hizo bado tu nawapelekesheni ' puta ' kwa hii hii ID yangu. Haya hii ID yako nyingine nimeshaijua sasa njoo basi tena na zile mbili zingine Mkuu.
 
miaka hiyo azania na tambaza vijana walikua machachari na akili zao zilikua machachari ila sasa azania na tambaza zimepoa na vijana akili zao zimekua baridiii, matokeo yao yanatuumiza sana tuliosona ktk shule hizi huko nyuma
Siku hizi wanakula sana chips.. Wanakuambia zikaushee
 
Dogo unaijua Jf kweli wewe team wema
 
Kwa nini mkuu ? Funguka
Puza Fala,

Mwenyewe ndivyo alivyokuwa akijiita Tambaza na masela wake ndivyo tulivyomuita.

Puza alikuwa na split personality, moja boonge la mtemi halafu nyingine bonge la mtu wa kawaida hivi, kama fala, basi ukimkuta kakaa nyuma kule mesi na machizi kanyong'onyea anasikiliza story ukimwambia "Puza Fala" na yeye utamsikia "niambie kichaa wangu". Hapo kila mtu ana "Nom de Guerra". Jina la vita. Kuna Msoviet, Bedui. Mpalestina. Tyson. Buchiza. Carlos. Bokassa. Abacha. Mkonda, duuh, machizi kibao nawasahau majina wengine.Miaka 26 sasa.

Ila siku moja Puza alijichanganya anga za Herman, form one. Herman alimrusha Puza makata mbele ya darasa sitasahau mpaka leo. Puza alichezea kichapo bila kutegemea halafu ile issue ikawa imeishia pale pale kama haijatokea. Halafu ukimuangalia Herman mwenyewe aliyemchapa Puza kama mtoto mtoto tu hana jina wala mwili.

Nikasema kila mtemi ana mtemi wake.
 
Matola kumbe we mtoni kitambo ee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…