Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Mimi nilikuwa nasikia sifa zake tu nilipokuwa Azania. Alikuwa anawatembelea mabesti wake pale Azania wakijiita Barcelona lkn zaidi ya usela, hawakuwahi kufanya jambo lolote la ajabu shuleni kwetu Azania zaidi ya utoro wa kawaida wa watukutu kutoingia darasani kwa kujichinbia vichakani.

Kilichokuwa kibanisikitisha kwenye lile kundi kulikuwa na dada mmoja akisoma Zanaki akiitwa Herieth ambaye alikuwa akishinda pake Azania kwa boyfriend wake aitwaye Gift ambaye alikuwa member wa group la kina Puza liitwalo Barcelona. Sijui yule dada aliishia wapi na upuuzi wao maana mwaka aliojinyonga Puza mimi nilikuwa namaliza F 4.

Vv
 

Mkuu ulikuwa F3 session A au B? Ulikuwa darasa gani? Mimi nilikuwa session B lebo nyekundu, F1 hadi F2 nilikuwa darasa N, nilipoingia F3 nilikuwa R (commerce).

Vv
 

Ni kweli Marehemu Omary au Omario a.k.a Puza alijiua ila naomba nikusahihishe kidogo ni kwamba hakujiulia Riverside na wala alikuwa haishi Riverside bali alikuwa ni ' Mtoto ' wa Magomeni na hata Msiba wake ulikuwa hapo hapo Magomeni. Leo mnamwogopa Scorpion wakati Puza alikuwa akiyafanya makubwa na ya hatari zaidi yake na Masela wote wa Dar enzi hizo walikuwa ' wanaufyata ' kwake ila na yeye Marehemu Puza na ujanja wake wote alikuwa akisikia tu Marehemu Nkama Sharp yule Police ' mbabe ' na ' mtemi ' kuliko Police wote wa kipindi hicho au miaka hiyo anakuja tu alikuwa anatoka ' nduki ' kujificha. Puza alikuwa akipanda tu ' Daladala ' Makondakta walikuwa wakianza kukusanya nauli siti za mbele yake tu na kama akikaa siti ya mbele basi Makondakta walikuwa wakianza kukusanya nauli zao siti za kuanzia nyuma yake tu huku wakimtolea ' tabasamu ' la kumnunia kimoyo moyo. R.I.P Omary Puza na Nkama Sharp.
 


You are quite right. Aliyetuletea sheria ya kuchomekea mashati alikuwa Mwalimu Andrew Kwayu aliyekuja kuchukua nafasi ya Mzee Kisamo nadhani 1990, nilikuwa na-enjoy kutochomekea mashati.

Vv
 

Umenikumbusha kikosi cha Azaboy Footbal. Kina Robert Mwampembwa, Edward Mpandang'ong'o, Cecil/Sisili, Tilla, Sasi .... Dah, Azania my school, the school of gentlemen.

Vv
 

Aisee jamaa umeongea sawa kabisa, kipindi hicho nilikuwa la saba pale muhimbili na bro zangu watatu walikuwa.pale. Na kuna mbabe mwingine alikuwa anaitwa Chino. Haitakuja kutokea shule kama Tambaza Boy.
 

Sonda boy tumeishi nae kino tu, jamaa alikuwa na mwili kama Wa Tyson.
 
UMENIKUMBUSHA WADOGO ZAKE PUZA WAKINA GWANTWA N'A GWAKI WALIYOKUWA WANAKAA KOTA ZA TANESCO...OPOSITE N'A DRIIVE IN(UBALOZI WA MAREKANI SAHV)

OVA

Gwantwa sijui alipotelea wapi. Alikuwa anatisha sana kwenye kikapu
 
Jamii forum ni tofauti na social forums zengine za whatsapp au facebook.Wengi wanaotumia JF ni waajiriwa au watumishi wa umma,wenye elimu zao au watu wenye heshima zao.Kama unaona umepotea kwa bahati mbaya unaweza kurudi kwenye groups za whatsapp au facebook.
 


Siku zote damu ya mwanadamu haimwagwi hovyo, ukiua tu basi juwa umejipa laana na usije shangaa unakuja kujiua bila kutaka kwani roho ya marehemu inakudai.
 
miaka hiyo azania na tambaza vijana walikua machachari na akili zao zilikua machachari ila sasa azania na tambaza zimepoa na vijana akili zao zimekua baridiii, matokeo yao yanatuumiza sana tuliosona ktk shule hizi huko nyuma
Na kibaya zaidi zote zmewah kushika mikia hivi karibun ktk matokeo ya kitaifa[emoji20] [emoji20]
 
R.I.P labda angekuja kuwa Scorpion mwingine pengine mungu tunamwitaga fundi.
 
Hivi unajua umenichekesha kwa sauti! !! Eti vijamaa vifupi hivi havijachomekea mashati... vingi lakini vibabe mbaya..
 
Unajuaje! ?Labda angekuja kuwa Putini wetu. huoni alishaanza kuonyesha dalili za kutetea wanyonge! ?
 
RIP Puzza mara ya mwisho nilikuwa nae camp ya skauti 77 nadhani mwaka 1990 nikuwa form three R hapo Tambaza yeye akiwa form one ,alikuwa ni best yangu tunacheza ngumi hapo jengo waliokuwa wanakaa bording form 5 and six ,Apumzike kwa AMANI nimekumbuka mbali sana mzee Kalumuna na second master Mwaipopo, na babu TALIBARI mhindi aliyekuwa anauza juice dukani pale mbele ya stamico
 
Kama alivyojiua john mjema. Kuchanganya cha arusha na cha tabora ni shida.
 
Kipindi hiki wakati kina Puza Wanajivunia ujinga hata mimi nilikuwa O level, ndio kilikuwa kipindi cha kwenda Zenj na passport, kwenda UK bila viza ilikuwa unakata tu ticket unakipa kitu, na walioingia UK kipindi hicho karibu wote sasa hivi wana uraia.
Michongo ya kwenda Marekani ilikuwa kwa summer Camp na Jambo lee kupitia boy scout hakika nimekumbuka zamani.

Kuna walimu waliniwekea bifu za kitoto kisa navaa mokasini za dukani maduka ya samora avenue wao wanavaa bora shoes.

Ila ilinishangaza zaidi kipindi chetu mafisadi walikuwa mafisadi kweli watoto zao walikuwa wanadrive magari kuja nayo shule kuanzia form one mpaka form four.

Kampani yangu ya kutokea mtaani ilikuwa wote wapo Tambaza mimi nilikuwa ni mmoja ya wanafunzi wachache tuliokuwa tunaingia Tambaza na uniform za shule nyingine na tulikuwa powa na msosi wa bure wa shule nilikuwa napiga bila kubaguliwa.

Namkumbuka mshikaji mmoja wanamuita kiuno jina lake nimemsahau alikuwa karibu na kina Saigon wa Diplomats huyu jamaa alikuwa anatisha kwenye kucheza na gari.

Wakati kina Puza wanatamba na usela mavi wao mimi nilijiongeza kwa watoto wa kishuwa tukitoka na mikoko ya madingi zao breki Forodhani secondary school kwa mademu wenye TBS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…