#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Licha ya kuwepo mapungufu kupambana na covid lkn nchi hakuiweka
Lockdown,magufuli ni kama alikuwa anataka
Watanzania tuishi nayo tu

Ova
Uingereza wameshaongelea hiyo kitu kuwa huu ugonjwa inabidi waishi nao
 
Sasa hawa wanaosema Jiwe kafa kwa corona wamejuaje? maana unaambiwa fulani kafa kwa corona ila wale watu wa karibu wa marehemu huoni kama wameambukizwa huwaoni hata na mafua sasa hii corona ya bongo ni ya aina gani?
Kwa sasa yeyote anaweza kusema vyovyote.
 
Mkemia aliharibu kwa kuzuia takwimu kuchukuliwa akidai wote wamepona kabisa. Sasa Mama anatoaje maamuzi bila analysis na tafiti ya kitaaluma?

Mwanzoni tulianza vizuri ila walipoingiza siasa wakaharibu kila kitu....
Ni tafiti gani ya kitaaluma iliyowaambia wasishikane mikono kwa sababu ya corona ila barakoa wasivae wala kuepuka mikusanyiko?

Maana tunaona wanasalimiana kwa kutoshikana mikono hilo tunaelewa ni kwa sababu ya corona ila tunaona hawavai barakoa wala kuepuka mikusanyiko,sasa hapo nako kuna ushauri gani wa kitaalamu ambao utakuja na mapendekezo mengine tofauti na watu kuvaa barakoa? sasa nashangaa hata hilo nalo Mama kashindwa kulitangaza ukiachilia na yeye kufanya et tunatetea hadi aambiwe na wataalamu.
 
Mimi na familia yangu tutachoma chanjo Kama kamati itayoundwa ikipendekeza tuchomwe chanjo..siwezi kufuata mambo ya kichawi na kuacha ya sayansi
 
Chanjo lazima Ili kutotengwa kimataifa, mbona mataifa mengine wametumia wewe ulitakaje
Chanjo sio lazima ni hiari ya mtu kudungwa ama kutodungwa,yeye mama anaonekana anataka zilitwe ila sasa asitumie mgongo wa kamati,tunajua hilo ndio lengo lake sasa yeye alete tu asizunguke zunguke zikija watakaochoma watachoma basi tutakuwa tunaelewa na wazungu maisha yaendelee.
 
Naomba kujua mh mollel Ana hali gani? Alikuwa anataminisha mambo hovyo hovyo wakati yeye Ni daktari..
 
Hiyo ni wave mbona huelewi..... Ukisikia third wave ndio iliyopita hapa Tz mwezi december ika peak February. So waliopona ewaa waliokufa walienda na nmeshaeleza humu kwamba Baba yangu mzazi almanusura afe kama sio kumpeleka hospital ya kibeberu baada za serikali kudai "ana homa ya kawaida tu".

Wote tunajua hata influenza za kawaida tu zinawaua wazungu kuliko hata Corona.... So sio jambo jipya kwa mafua hatari kma swine au bird flu kuua sana nchi za magharibi. Otherwise wangekufa wengi zaidi if wasinge weka sheria kma za lockdown au wasingekua na medical facility nzuri.

Tanzania waliugua wengi na sisi pia 5% walifariki tofauti ni kwamba hatutangazi takwimu. Ila mie mtaani tu na ukoo wangu, peers,friends, kulikua na misiba multiple mwezi February. Hili hta ww unafahamu ni WAVE

Kama mngetaka kucompare na wazungu kwanini hujiulizi Ukimwi au malaria inatuua sisi kuliko wao? Ama Miili yetu ina nguvu tu kwenye corona na magonjwa mengine haifui dafu?

Twende kwa hoja
 
Mtaongea sana sukuma na Burundi gang!
Jifariji ila unasahau alikuwa mwenyekiti mwenza bunge la katiba, alikuwa makamu wa rais na bado yupo ccm utakuja baadae kulalamika usichojua ccm ni ileile ni sawa na chupa mpya mvinyo wa zamani
 
Tunasubiri muujiza gani mwingne Watanzania kudhihirisha kwamba Mama alikuwa tofauti na mtangulizi wake!
 
Jifariji ila unasahau alikuwa mwenyekiti mwenza bunge la katiba, alikuwa makamu wa rais na bado yupo ccm utakuja baadae kulalamika usichojua ccm ni ileile ni sawa na chupa mpya mvinyo wa zamani
Ccm ikipata mtu anayetumia akili na sio makalio wala tumbo kufikiri lazima tumuunge mkono huyo mtu. Kwa iyo ni sawa tunavyomuunga mkono mama samia
 
Tunasubiri muujiza gani mwingne Watanzania kudhihirisha kwamba Mama alikuwa tofauti na mtangulizi wake!
We unaisi akili za mtangulizi wake zilikuwa sawa??? Yule si shetani aliyekuwa kwenye umbo la binadamu tu! Sasa kuna shida gani mama kuwa tofauti nae?
 
Nia yako unataka kumlinganisha na Magufuli?
 
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
Kwani njia pekee ya kupambana na Corona ni lockdown tu? Mbona umeng'ang'ania lockdown, kakuambia ikidhihirika kuwa kweli Corona ipo Tanzania ataweka lockdown? Hiyo ni hofu yako tu na huna sababu ya kujenga hofu kwa kuwa utatuzi utatolewa na wataalamu na bila shaka Mh. Rais atazingatia ushauri huo katika uamuzi wake. Au huna imani na wataalamu wetu?
 
Kumekucha!

Yupo sahihi kabisa kwa sababu ile kamati ya mwanzo iliongozwa na PM Majaliwa na Ummy Mwalimu ilikuwa ni ya kisiasa siyo ya kitaalamu na haijawahi kuvunjwa!

Ndio maana ukaona Jaffo amejiingiza na nyungu zake.
Leo hii mshaanza kumbana Magu kama vile wasaliti walivyo mkana yesu kristu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…