Hivyo vifo ndio vinatangazwa sana na ndio vinavyofanya watu waogope corona na kuona ni ugonjwa hatari na ndio maana vinatangazwa sana kuliko wanaoumwa na kupona japo ndio wengi. Sasa kama wenzetu huko wenye huduma bora za afya na kufuata tahadhari zote wengine hadi lockdown ila bado unasikia maelefu ya watu wanakufa kwa siku ndio maana ikaonekana afrika tutaokota maiti barabarani,kuna muda hadi kulitokea ule uvumi wa kwamba hospitali zimezidiwa wagonjwa Tz,ila sasa hivi inaonekana tatizo hatuna takwimu story za maiti barabarani na hospitali kuzidiwa wagonjwa hazipo tena.