#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Wasalaam wana jamvi!

Nimeshangazwa sana na Mh Rais kusema ataunda kamati kuhusu swala la Corona ili baadae tuwe na msimamo kuhusu Corona!

Mimi kwenye hili nimejiuliza maswali hivi ni kweli Tanzania hatukuwa na msimamo kuhusu Corona? Huyu Rais si alikuwa Makamu wa Rais na Rais wake alishasema wazi kuwa Tanzania hakuna Corona na kama ipo ni ndogo sana?

Hii kamati anayounda anataka imwambie nini kipya asichokijua? Anataka aanze kutoa takwimu za Corona sasa anataka kamati imshauri?

Anataka aweke watu Lockdown sasa anataka kamati imshauri?

Anataka kulazimisha watu kuvaa barakoa sasa anataka kama imshauri?

Anataka kupokea chanjo ya Astrazeneca sasa anataka kamati imshauri?

Rais anaogopa nini kusema alikuwa hakubaliani na jinsi mtangulizi wake alivyo kuwa anaikabili Corona? Rais anaogopa nini kusema wamejiandaa kupokea chanjo ya AstraZeneca hivi karibuni?

Sidhani kama Rais anatakiwa kujificha nyuma ya kamati kwenye swala kama hili ambalo liko wazi!

Kuna kitu gani hajui ambacho anataka kamati imwambie?

Kwanini anajificha nyuma ya kamati anashindwa nini kuwambia watanzania wajiandae kudungwa Astrazeneca?

Kama Tanzania hatuna msimamo kwanini yeye havai barakoa? Hajui huo nao ni msimamo? Anataka ashauriwe nini?

Kwanini Tusiamini ana ajenda zake mkononi anataka azipitishe nyuma ya kamati ili watanzania waamini ni msimamo wa kamati kumbe ni msimamo wake?

Wasalaam!

Kwa nini mumeamua kutabiri uamuzi atakaochukua mapema hivyo?

Muacheni na yeye afanye maamuzi baada ya kupata uhakika wa kitaalamu.

Hiyo ripoti iko wapi wakati hata hatujui ni wangapi wamekufa kwa ugonjwa huo lakini pesa za msaada tumechukua.
 
Licha ya kuwepo mapungufu kupambana na covid lkn nchi hakuiweka
Lockdown,magufuli ni kama alikuwa anataka
Watanzania tuishi nayo tu

Ova
Matokeo yake kaondoka nayo
 
Mpendwa wetu alikua ni rais mnajim
Dunia nzima hili jambo limetesa sana
Ila Magu alielewa hii kitu imetokana vp

M/mungu alitaka kuwakumbusha watu wake kwamba wamemsahau vya kutosha hivyo haraka wamrudie

Ile Magu kutamka hadharani kua hili tuna mwachia m/mungu , bas hapo mungu akatupa kinga
Na nan ni mbora wa kinga isipokua ulinzi toka kwa mungu???????

Bas Hakimu Mfawidhi , jiandae hutokuja kusikia watu 800 wamekufa kwa siku kisa korona
Kama NYC, hutokuja kuona jiran zako wanakufa kama kuku.

Hili jambo ni mungu tu anatulinda.

NB: kinyume na msimamo wa mpendwa wetu
Tujiandae na mengi
Kawadanganye MATAGA wenzako ndiyo
 
Nilivyoona id yako nikajua wewe ni mkushi mwenzetu, kumbe ni opposite.

Dah bora ungejiita plato, sio hayo majina yetu wakushi,
Halafu unakuja na mambo ya chanjo.

Jina lako, fake id yako ni vizuri ikaendana na mtamazamo wako.

Ni km upo tayari niambie nikupe id inayoendana na mtazamo wako.

Sisi wakushi hatutaki chanjo.
Ninyi ndio mlioi Hijack ajenda tengezeni chanjo halafu ndio tungee
 
huyo mungu alishindwa nini kumsaidia korona isimuue?
Mungu ndiye pekee aliye mkuu, wa kuabudiwa. ukjikweza au ukikwezwa, kutaka kujifananisha na Mungu, lazima Mungu atawadhihirishia wanadamu kuwa biadamu si chochote mbele yake.
 
We mjinga nini?
Kwani Rais ni Daktari?
Na anafanya weledi kuwatumia wataalam kuliko yule alisema tuijfukize na kula Bupiji, halafu akaondoka yeye!
Mleta huu uzi ni CHAWA haswaa wa Jiwe hivyo huu uzi hakuuleta kwa bahati mbaya.
 
Kumekucha!

Yupo sahihi kabisa kwa sababu ile kamati ya mwanzo iliongozwa na PM Majaliwa na Ummy Mwalimu ilikuwa ni ya kisiasa siyo ya kitaalamu na haijawahi kuvunjwa!

Ndio maana ukaona Jaffo amejiingiza na nyungu zake.
😂 😂 😂
 
Hii nchi wajuaji niwengi ndomana magu alikuwa anadhibiti midomo ya wajuaji!!
Kunaubaya gani kuunda kamati ikakushauri namna ya ku-deal na korona???
Nani hajui maamuzi mengi serikali ilopita yalikuwa ya MTU mmoja akijidai serikali niyake!! Watu waache unafiki!!
 
Uzuri wa corona inawatafuna watu wenye kushupaza shingo kama nyinyi ndiyo inaondoka nao .
Huna Chanjo, nyungu hujapiga, lockdown hujawekwa na huvai barakoa, lakini upo na hujaambukizwa!! Huoni kwamba unachokiogopa kinakuogopa?

Pumbavu mkubwa wewe!
 
Kwani chanjo ya corona ni astrazeneca tu??? Mbona umeshindwa hata kuficha upumbavu wako????

Nyie mapandikizi ya nchi jirani mliyojiunga Ccm Kwa sababu ya pandikizi mwenzenu Magufuli jiandaeni tu. Nchi inarudi kwenye sanity na sio ujinga na upumbavu wenu.

Rais yuko sahihi hafanyi maamuzi kwa kukurupuka, anasikiliza kwanza ushauri wa kitaalamu. Hivyo ndo dunia ya kisasa inavyokwenda
Wachana na hao maboya wasiyo jua kuwa Magu keshaitwa na mungu
 
Wewe ndo ambaye unaogopa Yeye Sasa hivi ni RAIS na njia anayotumia ni njia sahihi hasa ukizingatia kwamba hatukuwahi kuwa na kamati kama hio so my friend let the DEAD rest we subiri majibu ya Taarifa ya kamati.SAWA?
 
Nilivyoona id yako nikajua wewe ni mkushi mwenzetu, kumbe ni opposite.

Dah bora ungejiita plato, sio hayo majina yetu wakushi,
Halafu unakuja na mambo ya chanjo.

Jina lako, fake id yako ni vizuri ikaendana na mtamazamo wako.

Ni km upo tayari niambie nikupe id inayoendana na mtazamo wako.

Sisi wakushi hatutaki chanjo.
Wakush my foot.... Mkush gani ww una akili ndogo hivi? Rwanda/Watutsi na Ethiopia wote hao wamekubali Chanjo ndio sembuse mkush wa Runzewe?

Mbona Yellow fever ndio ulidungwa ili uweze kufika Tanzania? Au hyo haikutoka kwa beberu?
 
Back
Top Bottom