Kwanini Rais mstaafu Kikwete hakupewa nafasi ya kuongea katika uzinduzi wa Kavazi la Dkt. Salim?

Huyu alishiriki kampeni chafu za kumchafua Salim wakati wa kampeni za kugombea Urais 2005.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Adui yako apewe jukwaa aongee nini?
 
Unashangaa kutopewa nafasi ,mshangao ungekuwepo kama angepewa!
 
Inafahamika ccm wakati ule Imemezwa na mtandao wa Chikwete na Mamvi Walimchafua sana Dr Salim.
 
Hahahahahaaaaa! Huyo magufuli wenu mjini kaletwa na kina JK
Magufuli mjini hakuletwa na JK.... Magufuli aliingia mjini enzi ya Mwinyi chini ya bahasha toka kwa Julius Nyerere na kukabidhiwa kwa Mkapa aliyemfikisha hapo alipoishia.

Unajua nani aliileta familia yao nchini? Dhumuni lake unalijua? Unaonekana mtoto sana kwa siasa za nchi hii.
 
Nawe umekuwa mtoto mno kuelewa mantiki ya nilichokisema.......fasihi. Kuna hidden meaning niliyoimaanisha, sikumaanisha kuwa JK ndiye aliyemlipia Lori alilopanda wakati anakuja wala aliyemwita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…