Kwanini Rais mstaafu Kikwete hakupewa nafasi ya kuongea katika uzinduzi wa Kavazi la Dkt. Salim?

Ukiona mahali yupo kikwete na samia kisha samia hampi kikwete nafasi ujue kuna kitu nyuma yake.

Mwaka 2005 wakati kikwete akiwania kupeperusha bendera ya urais yeye na kundi lake waliamua kumchafua Dr salim ahmed salim kuwa alihusika na mauaji ya mzee Karume Zanzibar.

Wakati huo dr Salim nae alikuwa kwenye kinyang'anyiro na alikuwa na mvuto kwelikweli Dr. Salim. Alikuwa na cv nzito haswa. Na iliwahi kusemekana kuwa ni moja ya watu ambao Nyerere alitamani aje kushika nafasi za juu kabisa kwa nchi hii.

Ile taarifa ilimnyong'onyeza sana Dr na kuanzia pale ni kama alijitoa kwenye mkondo wa mambo ya kisisasa. Sidhani kama Kikwete na genge lake waliwahi tena kwenda kumpigia magoti Dr. Salim.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
Kiwete na MTANDAO ni matapeli na wezi wakubwa wa nchi hii
 
Jana nilipata wasaa wa kufuatilia mubashara uzinduzi wa Kavazi la Mwanadiplomasia maarufu Dr Salim Ahmed Salim. Watu wengi walipata nafasi ya kusema machache juu ya Dr Salim wakiwepo mawaziri wastaafu na hata wengine kutoka kada mbalimbali za utumishi.

Cha ajabu uzinduzi wa Kavazi ulimalizika bila kumpa Rais mstaafu Kikwete fursa ya kuzungumza mambo adhimu kuhusu Mwanadiplomasia maarufu Dr Salim Ahmed Salim.
Ikumbukwe Kikwete aliwahi kuwa waziri wa mbo ya nje miaka 10.

Kwa vyotevyote vile lazima kakutana na kufanya kazi na Dr Salim Ahmed Salim akiwa OAU.
Pia Kikwete alikuwa mtumishi ktk chama huku Dr Salim akiwa waziri Mkuu na baadae waziri wa nchi za nje katikati ya miaka ya 1980

Wakati Kikwete akiingia bungeni Mara ya Kwanza 1988, Dr Salim alikuwa waziri wa nchi za nje. Hivyo wanafahamiana pakubwa tu, kwani Jk yeye alianza na unaibu waziri wa Nishati na Madini 1988 baada ya kuteuliwa ubunge.

Kwanini jabali hili la siasa hakuzungumza chochote juu ya Mwanadiplomasia Dr Salim?
Mnatafuta majungu tu.labda hawaelewana kisa uchaguzi wa 2005.
 
Magufuli mjini hakuletwa na JK.... Magufuli aliingia mjini enzi ya Mwinyi chini ya bahasha toka kwa Julius Nyerere na kukabidhiwa kwa Mkapa aliyemfikisha hapo alipoishia.

Unajua nani aliileta familia yao nchini? Dhumuni lake unalijua? Unaonekana mtoto sana kwa siasa za nchi hii.
Mkuu

Ongeza nyama hasa paragraph ya mwisho!

Ongeza nyama mkuu!

Ongeza nyama!funguka mkuu!!
 
Bibi FaizaFoxy anasemaje juu ya hili
Dr. Msipende kumpa kiki sana huyo member anayejinadi na kudanganya wajinga humu kwa yeye ndo Rais wa nchi... Rais gani wa nchi uliona ana muda wa kukaa kujibizana mitandaoni hali ya kuwa ana mambo chungu tele ya kufuatilia?! Na yeye kashajizolea umaarufu wa hovyo!

Hii nchi hii 😂😂😂😂😂😂🙌🏾
 
Jana nilipata wasaa wa kufuatilia mubashara uzinduzi wa Kavazi la Mwanadiplomasia maarufu Dr Salim Ahmed Salim. Watu wengi walipata nafasi ya kusema machache juu ya Dr Salim wakiwepo mawaziri wastaafu na hata wengine kutoka kada mbalimbali za utumishi.

Cha ajabu uzinduzi wa Kavazi ulimalizika bila kumpa Rais mstaafu Kikwete fursa ya kuzungumza mambo adhimu kuhusu Mwanadiplomasia maarufu Dr Salim Ahmed Salim.
Ikumbukwe Kikwete aliwahi kuwa waziri wa mbo ya nje miaka 10.

Kwa vyotevyote vile lazima kakutana na kufanya kazi na Dr Salim Ahmed Salim akiwa OAU.
Pia Kikwete alikuwa mtumishi ktk chama huku Dr Salim akiwa waziri Mkuu na baadae waziri wa nchi za nje katikati ya miaka ya 1980

Wakati Kikwete akiingia bungeni Mara ya Kwanza 1988, Dr Salim alikuwa waziri wa nchi za nje. Hivyo wanafahamiana pakubwa tu, kwani Jk yeye alianza na unaibu waziri wa Nishati na Madini 1988 baada ya kuteuliwa ubunge.

Kwanini jabali hili la siasa hakuzungumza chochote juu ya Mwanadiplomasia Dr Salim?
wengi tunajiuliza hilo. ila nadhani salim angekuwa Rais angekuwa ametufaa sana.
 
Nawe umekuwa mtoto mno kuelewa mantiki ya nilichokisema.......fasihi. Kuna hidden meaning niliyoimaanisha, sikumaanisha kuwa JK ndiye aliyemlipia Lori alilopanda wakati anakuja wala aliyemwita.
Magufuli kawa Naibu waziri wakati Jakaya Bado mchanga kwenye Corridors of Power! JK hana mchango wowote katika kumjenga na kumkuza Magufuli! Hata 2005 JK alitaka kumtema Magufuli kwenye baraza baada yakupelekewa umbeya na Salva Rweyemamu je wamjua nani alimfanya JK ambakishe Magufuli barazani? Kwanini?
 
Jana nilipata wasaa wa kufuatilia mubashara uzinduzi wa Kavazi la Mwanadiplomasia maarufu Dr Salim Ahmed Salim. Watu wengi walipata nafasi ya kusema machache juu ya Dr Salim wakiwepo mawaziri wastaafu na hata wengine kutoka kada mbalimbali za utumishi.

Cha ajabu uzinduzi wa Kavazi ulimalizika bila kumpa Rais mstaafu Kikwete fursa ya kuzungumza mambo adhimu kuhusu Mwanadiplomasia maarufu Dr Salim Ahmed Salim.
Ikumbukwe Kikwete aliwahi kuwa waziri wa mbo ya nje miaka 10.

Kwa vyotevyote vile lazima kakutana na kufanya kazi na Dr Salim Ahmed Salim akiwa OAU.
Pia Kikwete alikuwa mtumishi ktk chama huku Dr Salim akiwa waziri Mkuu na baadae waziri wa nchi za nje katikati ya miaka ya 1980

Wakati Kikwete akiingia bungeni Mara ya Kwanza 1988, Dr Salim alikuwa waziri wa nchi za nje. Hivyo wanafahamiana pakubwa tu, kwani Jk yeye alianza na unaibu waziri wa Nishati na Madini 1988 baada ya kuteuliwa ubunge.

Kwanini jabali hili la siasa hakuzungumza chochote juu ya Mwanadiplomasia Dr Salim?

Mahakama ya ndani ilimsuta, aliikata hiyo nafasi.

Unaweza kuzishinda MAHAKAMA ZOTE DUNIANI
Lakini mahakama ya ndani kamwe hutaishinda
 
Funguka
Magufuli kawa Naibu waziri wakati Jakaya Bado mchanga kwenye Corridors of Power! JK hana mchango wowote katika kumjenga na kumkuza Magufuli! Hata 2005 JK alitaka kumtema Magufuli kwenye baraza baada yakupelekewa umbeya na Salva Rweyemamu je wamjua nani alimfanya JK ambakishe Magufuli barazani? Kwanini?
mkuu
 
Vijana mnapenda miteremko ndio maana mnalia lia sijui dr.Salim alifanyiwa figisu niwakumbushe mamlaka hajawahi kuja kirahisi rahisi duniani kote.Nyie mnaona akina Putin wanaua wanaenda kinyume nao au kuwa challenge Bure.Figisu kwenye siasa kawaida sana.Acheni kulia lia
 
Kikwete kashiriki pakubwa sana chini ya wanamtandao kumsulubu vibaya sana Salim Ahmed Salim. Angekua muungwana angetumia hiyo fursa kutubu!
Huyu mkwere hajawahi kuwa muungwana hata siku moja! Ni mtu mwenye roho ya kimaskini, fitina, visasi na juu ya yote fisadi aliyekubuhu. Angepewa nafasi ya kuzungumza angenajisi shuhuri yote afadhali hawakumpa nafasi. Inanikumbusha alivyoshushuliwa alipozungumza kwenye mazishi ya Magufuli kule Chatto.
 
Back
Top Bottom