Kwanini Rais Samia aliamua kujibu hivi kuhusu Katiba Mpya?

Kwanini Rais Samia aliamua kujibu hivi kuhusu Katiba Mpya?

Na hapo alishapelekewa maswali akaandaa majibu, lakini alishindwa kuzuia kibri yake......

Hata hivyo iwe funzo kwa Kikeke, aache kumhoji huyu mama, ikiwa ni lazima BBC kufanya mahojiano naye, basi walete mwandishi asiye mtanzania.

Maana dharau iliyoonyeshwa ni kwa sababu ya uraia wa mwandishi. Muulizwa maswali alijisahau akaona ni kijana wake tu na si mwanahabari wa chombo cha kimataifa....
 
Urais mtamu. Unataka abadili katiba aishi kama shetani.
How? Katiba mbovu ndiyo dhamana ya Urais wake?Anauhakika kwa Katiba hii hawezi ukosa huo Urais?

Hii maanake CCM hawatakubali mchakato Wa Katiba Mpya kwa sababu iliyopo ni yao na inawapa unafuu?

Sisi Watanzania tunataka kuandika Katiba Mpya,tunafahamu kuwa wenzetu kwa uroho wao Wa madaraka wameihodhi Katiba chakavu kuliko hats ya chama chao ili waendelee kuwepo.

Tahadhari:Katiba tunayoidai ni ya JMT na CCM hamna uwezo wala uhalali Wa kuzuia.Mnaichelewesha tu lakini kuizuia hamwezi,mbaya zaidi kwenu mnaweza kujifungia hats milango ya kustahili kuwepo wakati tukishaipata Katiba Mpya.

Ushauri:Ibadilisheni hii Katiba ya 1977 kuwa ya CCM maana inaonekana ndiyo inayowapa shibe.
 
Kuna clip naiona ikionesha mahojiano ya Salim Kikeke na mama wa Taifa

Salim alimuuliza mama tutegemee lini katiba mpya

Mama akajibu majibu fulani ya kufarakanisha

View attachment 2158872
Rais alijibu kwa usahihi kabisa! Katiba ni ya Watanzania.

Watajadili na kuamua wenyewe muda ukifika. Pia haiwezi kuwa ajenda ya kikundi cha watu.

Hii si Katiba ya Saccos wala NGO.🙏🙏🙏
 
Majibu yake yanafurahisha sometime.. its like hakutegemea maswali ya namna hiyo)))
 
Kwa kweli majibu aliyoyatoa kuhusu Lissu na Katiba ya aonyeshaye ni jinsi gani ambayo bado hajaiva. Pamoja na kushindwa au kukata a kuyajibu vilevile ameonekana kuchukizwa na hayo maswali.

Maza anajifanya hajui kuwa Watanzania wanataka Katiba Mpya wakati wote tunajua walivyojitokeza kwenye Tume ya Warioba kutoa maoni yake. Na yeye kama Naibu Spika wa Bunge la Katiba kujifanya hajui ni kiburi au jeuri ya Madaraka.

Maza kudai kuwa Lissu aje asaidie uchunguzi wa kesi yake imeonyesha pia how naive she could be kwenye maamuzi yake. Yaani bado anatumia majibu rahisi ya Sirro ambayo kila mtu aliyaona hayana mashiko. Uwepo wa Lissu utasaidia vipi uchunguzi.

Mbona yule Mfanyabiashara wa Mtwara aliuawa aliagiza uchunguzi umefanyika na umefanyika. Kwa nini hawakutumia majibu hayo rahisi....!!?
 
Si ni kwa sababu anajua hizo kelele ni za mitandaoni tu.
Kelele za mitandaoni kivipi wakati Tume iliundwaje na Bunge likakaa.... Yote hiyo ilikuwa kelele za mitandaoni...!!? Akina Kessy na Ndugai walitaka kubadilisha katiba kwa kudai a take asitake watamuongezea..... Na Bunge likashangilia.

Kama Wananchi hawataki, hayo maoni ya Katiba aliyoyakusanya Warioba aliyapata wapi?
 
Mama ni ndugu yetu katika imani, au sio?
Pamoja na hayo yote lakini tukumbuke pia mama ndiye HEAD OF STATE !! na kwamba suala hilo amuachie yeye na wananchi wake wataelewana wafanye nini ndivyo alivyomaanisha !!

Sio kila kitu waelezwe BBC AU ALJAZEERA !! mengine ni yetu wenyewe ! Au nasema uongo bandugu ??!
 
na hapo alishapelekewa maswali akaandaa majibu, lakini alishindwa kuzuia kibri yake......

hata hivyo iwe funzo kwa Kikeke, aache kumhoji huyu mama, ikiwa ni lazima BBC kufanya mahojiano naye, basi walete mwandishi asiye mtanzania.

Maana dharau iliyoonyeshwa ni kwa sababu ya uraia wa mwandishi. Muulizwa maswali alijisahau akaona ni kijana wake tu na si mwanahabari wa chombo cha kimataifa....
We una uhakika Kikeke ni Mtanzania?.. ameambiwa mambo ya watanzania awaachie watanzania wenyewe..
 
Mmoja atuwekee katika mtindo wa maneno, wengine hatuna uwezo wa kusikia.
Kikeke: Unaweza kuhakikishia waTz au kutoa ahadi kuwa kabla hujaondoka madarakani Tz itakuwa na Katiba Mpya?

SSH: Kwa nini nihakikishe hilo? Kwa nini unataka nihakikishe hilo?

Kikeke: Kwa sababu watu wanadai kuwa Katiba hii imepitwa na wakati.

SSH: Basi niachie mi na waTz tutaelewana.

Kikeke: Kwa hiyo Katiba itapatikana?

SSH: Si we huishi Tz? Mi na waTz tutaelewana.

Kikeke: WaTz wanasema wanataka Katiba.

SSH: ...wamekwambia wewe?
 
Kelele za mitandaoni kivipi wakati Tume iliundwaje na Bunge likakaa.... Yote hiyo ilikuwa kelele za mitandaoni...!!? Akina Kessy na Ndugai walitaka kubadilisha katiba kwa kudai a take asitake watamuongezea..... Na Bunge likashangilia.

Kama Wananchi hawataki, hayo maoni ya Katiba aliyoyakusanya Warioba aliyapata wapi?
Mie mkuu nimesema tu kuwa Samia anajua vizuri kwamba kelele za kudai katiba mpya zipo mitandaoni tu na si uraiani huko kwa wamachinga na mama ntilie na ndio maana hili suala la katiba mpya huonekana kuwa ni hitaji la wanasiasa tu na hiyo ndio hali halisi iliyopo.

Kuhusu maoni aliyoyakusanya Warioba hata mimi nashangaa kwamba ndio watanzania hawa hawa ambao maoni yao yalikusanywa na Warioba au nini kimetokea?
 
na hapo alishapelekewa maswali akaandaa majibu, lakini alishindwa kuzuia kibri yake......

hata hivyo iwe funzo kwa Kikeke, aache kumhoji huyu mama, ikiwa ni lazima BBC kufanya mahojiano naye, basi walete mwandishi asiye mtanzania.

Maana dharau iliyoonyeshwa ni kwa sababu ya uraia wa mwandishi. Muulizwa maswali alijisahau akaona ni kijana wake tu na si mwanahabari wa chombo cha kimataifa....
....upeo tu!
 
Back
Top Bottom