Tajiri Kichwa
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 9,021
- 22,016
Kikeke: Unaweza kuhakikishia waTz au kutoa ahadi kuwa kabla hujaondoka madarakani Tz itakuwa na Katiba Mpya?
SSH: Kwa nini nihakikishe hilo? Kwa nini unataka nihakikishe hilo?
Kikeke: Kwa sababu watu wanadai kuwa Katiba hii imepitwa na wakati.
SSH: Basi niachie mi na waTz tutaelewana.
Kikeke: Kwa hiyo Katiba itapatikana?
SSH: Si we huishi Tz? Mi na waTz tutaelewana..
Kikeke: WaTz wanasema wanataka Katiba..
SSH: ...wamekwambia wewe?
Chui jike amevurugika duuh, hakuna mwimba mgumu kwa viongozi kama katiba mpya