Kwanini Rais Samia aliamua kujibu hivi kuhusu Katiba Mpya?

Kwanini Rais Samia aliamua kujibu hivi kuhusu Katiba Mpya?

Kwa kweli majibu aliyoyatoa kuhusu Lissu na Katiba ya aonyeshaye ni jinsi gani ambayo bado hajaiva. Pamoja na kushindwa au kukata a kuyajibu vilevile ameonekana kuchukizwa na hayo maswali.

Maza anajifanya hajui kuwa Watanzania wanataka Katiba Mpya wakati wote tunajua walivyojitokeza kwenye Tume ya Warioba kutoa maoni yake. Na yeye kama Naibu Spika wa Bunge la Katiba kujifanya hajui ni kiburi au jeuri ya Madaraka.

Maza kudai kuwa Lissu aje asaidie uchunguzi wa kesi yake imeonyesha pia how naive she could be kwenye maamuzi yake. Yaani bado anatumia majibu rahisi ya Sirro ambayo kila mtu aliyaona hayana mashiko. Uwepo wa Lissu utasaidia vipi uchunguzi. Mbona yule Mfanyabiashara wa Mtwara aliuawa aliagiza uchunguzi umefanyika na umefanyika. Kwa nini hawakutumia majibu hayo rahisi....!!?
Kuhusu Lisu alikuwa sahihi sana! Hivi Lisu anajiona yeye nani?

Eti uhakikishiwe ulinzi kwani hawa watz wengine wakiwemo kina Mnyika, Zitto, Mbowe nk wamehakikshiwa ulinzi na nani?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Kikeke: Unaweza kuhakikishia waTz au kutoa ahadi kuwa kabla hujaondoka madarakani Tz itakuwa na Katiba Mpya?
SSH: Kwa nini nihakikishe hilo? Kwa nini unataka nihakikishe hilo?
Kikeke: Kwa sababu watu wanadai kuwa Katiba hii imepitwa na wakati.
SSH: Basi niachie mi na waTz tutaelewana.
Kikeke: Kwa hiyo Katiba itapatikana?
SSH: Si we huishi Tz? Mi na waTz tutaelewana..
Kikeke: WaTz wanasema wanataka Katiba..
SSH: ...wamekwambia wewe?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Safi sana!

Ntaiscreen shot niweke ukutani hii

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Hata wanaodai Katiba mpya wangekuwa wao madarakani hiyo isingekuwa kipaumbele
Katiba mpya ni hitaji la nchi,haijalishi nani yuko madarakani.

Hao unaowaona kama ndio wanaodai nikwasababu nirahisi kusikika kwasababu tayari ni chama,ila kungekua na njia nzuri ya wananchi wote wa kawaida kuelezea maoni yao ya huitaji wa katiba mpya naamini wananchi wengi wangetaka katiba mpya.
 
Rais alijibu kwa usahihi kabisa! Katiba ni ya Watanzania. Watajadili na kuamua wenyewe muda ukifika. Pia haiwezi kuwa ajenda ya kikundi cha watu. Hii si Katiba ya Saccos wala NGO.[emoji120][emoji120][emoji120]
Ata serikali ni kikundi cha watu.Sasa siku itakapofika Ccm wakaweka swala la agenda ya katiba mpya kwenye ilani yao usije ukabadilisha mtazamo.

maana hapa unajitutumua tu kulingana na mtazamo wa raisi,naamini siku rais akibadilisha msimamo nawewe utabadilika.
 
Katiba mpya ni hitaji la nchi,haijalishi nani yuko madarakani.Hao unaowaona kama ndio wanaodai nikwasababu nirahisi kusikika kwasababu tayari ni chama,ila kungekua na njia nzuri ya wananchi wote wa kawaida kuelezea maoni yao ya huitaji wa katiba mpya naamini wananchi wengi wangetaka katiba mpya.
Kwanini unaamini hivyo mkuu ni kwa sababu ya kuwepo maoni ya uhitaji katiba mpya huku mitandaoni?
 
Ila kama raisi katukosea anasema eti

Kwani watanzania wamekwambia wanataka katiba mpya

Ina maana hajui kelele zote hizi.
Ukia
“Niachie mimi na watanzania wenzangu ”

Hao wenzangu nahisi ni kina mwezi wa kwanza ila sio sisi.
[/QUOTE

Ukifuatilia kwa makini body language ya HE. SSH, hilo swali hakuwa amelitarajia. Na hata kama lingekuja, sio kwa insistence ya Salim Kikeke kwa mtindo wa hard talk. Kwa kuzingatia dilemma inayomkuta Rais SSH kwamba , Kwanza alikuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge Katiba mpya na kwa hiyo ni mwumini wa Katiba mpya. Pili yeye binafsi kwa sasa ndio mnufaika mkuu wa hii Katiba mbovu ya sasa, lakini na Chama chake. Tatu kwamba japo hata viongozi muhimu (objective)wa chama chake kama kina Waryoba, Msuya, Werema, Msekwa, Mongela mama, nk nk walishasema hadharani kwamba Katiba mpya haikwepeki, inampa ukakasi. Nne, baya zaidi Katiba mpya ni Agenda kuu ya CHADEMA, chama kikuu cha upinzani kilichosambaa nchi nzima na chenye nguvu haswaa miyoyoni mwa watanzania watu wazima wanaojielewa, lakini vijana wengi wasomi nchi hii. Hili linamtia hasira kwamba atalazimika kucheza ngoma ya mpinzani. Tano, SSH angependa kuonekana kwa wengine kama mwana diplomasia na zaidi mwana demokrasia kuliko mtangulizi wake japo moyoni sivyo alivyo na hapo hapo anajua msimamo wa viongozi wengi wa Chama chake wa lifanyike lolote hata baya mradi chama kibaki madarakani na hivi pia sio moyo wake ulivyo na yote haya yanamfanya awe mtu wa hasira. Akumbuke tu kwamba nchi hii ni ya wote, dhamana yake yeye itapita na historia yake itaandikwa na itabaki kumbukumbu kwa watu wote - kwamba itasomekaje ndilo linalompa hasira na kuwa na majibu fikirishi. Ushauri wangu, Rais SSH, asibeze hoja ya Katiba mpya maana ni takwa la raia wengi. Asiibeze Chadema na hoja zao. Ni real. Acheze siasa very careful. Hawa watatumia ujanja wao wa kisiasa wakitumia CCM isiyo kitu kimoja, kuchokwa kwake sababu ya kukaa madarakani muda mrefu na tuhuma nyingi za kifisadi na kutokukimbiliwa na vijana wasomi pamoja na hali mbaya ya uchumi ambayo itaaminika chanzo ni CCM.
 
Lugha hizi zinapatikana ,Temeke Mikoroshini,Sandali,Tambuka Reli ,Kwa Maguruwe ,Yombo Kwa Fundi Umeme nk!
Basi itakuwa huko hawahitaji katiba mpya ndio maana Samia kawalenga watu wa huko.
 
Inabidi wananchi nao wanapopata nafasi ya kueleza kero zao mbele ya kiongozi wao wawe wanataja na uhitaji wa katiba sio wanawaachia wanasiasa tu hadi inaonekana katiba mpya ni hitaji la wanasiasa tu na matokeo yake ndio hayo kuonekana wananchi hawaelewi lolote kuhusu katiba.
 
Kuhusu Lisu alikuwa sahihi sana! Hivi Lisu anajiona yeye nani?

Eti uhakikishiwe ulinzi kwani hawa watz wengine wakiwemo kina Mnyika, Zitto, Mbowe nk wamehakikshiwa ulinzi na nani?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Kwenye kuhakikisha ulinzi inaweza kuwa ngumu kwa Rais kulisema wazi. Ila bado Lissu ana point na huwezi kumlinganisha issue yake na uliowataja. Wote tunajua kuwa walitaka kumkamata tena baada ya uchaguzi... Mpaka sasa hatujui sababu ni nini?

Pia Ile ya kudai uchunguzi wa Shambulio la Lissu halijafanyika kwa kuwa Lissu hayupo kutoa ushirikiano hapo kachemka.

Hii inaonyesha kuwa serikali haina Mpango wa kuchunguza na wameshindwa kutoa sababu ya msingi.

Ndiyo maana tunaconclude kuwa ilikuwa ni kazi ya kikosi maalumu.
 
Kwenye kuhakikisha ulinzi inaweza kuwa ngumu kwa Rais kulisema wazi. Ila bado Lissu ana point na huwezi kumlinganisha issue yake na uliowataja. Wote tunajua kuwa walitaka kumkamata tena baada ya uchaguzi... Mpaka sasa hatujui sababu ni nini?

Pia Ile ya kudai uchunguzi wa Shambulio la Lissu halijafanyika kwa kuwa Lissu hayupo kutoa ushirikiano hapo kachemka. Hii inaonyesha kuwa serikali haina Mpango wa kuchunguza na wameshindwa kutoa sababu ya msingi. Ndiyo maana tunaconclude kuwa ilikuwa ni kazi ya kikosi maalumu.
Lisu alidai mbaya wake akikuwa Magufuli na Magufuli hayupo sasa wasiwasi wa nini?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
It doesn't matter whether she agrees or not that ata deal na katiba or not. The way she answered was wrong. She is the President hapaswi kujibu ki mipasho. That was totally unacceptable. Sad

I was shocked [emoji32] to be honest
 
Samia ni Rais wa kikatiba katiba imemupofusha macho ya kutokuona ubaya wake.
 
President amejibu ki mipasho sana hilo swali...

Unamuulizaje mwandishi kwamba Walikwambia wewe?, niachie mm na watanzania..?

Bimkubwa angekuwa anaandaliwa majibu,, kuna siku ataaibisha taasisi ya Urais
 
President amejibu ki mipasho sana hilo swali...

Unamuulizaje mwandishi kwamba Walikwambia wewe?, niachie mm na watanzania..?

Bimkubwa angekuwa anaandaliwa majibu,, kuna siku ataaibisha taasisi ya Urais
Kwani hapo kafanyaje,kama sio kuidhalilisha!

Kuna kundi Fulani la watu halitakiwi kupewa madaraka makubwa ,wata abuse tu...watu wengine wanataka vitu simple...Ngoma ,michezo...Utamaduni!
 
Subirini mumchague Lema 2025 awape katiba mpya, kwa sasa tuache kazi iendelee
 
Back
Top Bottom