Kwanini Rais Samia ameondoa zuio la mikutano ya vyama vingi sasa na si mara tu alipokabidhiwa madaraka?

Mchanya

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
997
Reaction score
1,568
Kama wengi mlivyofuatilia leo Januari 3, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alifanya mkutano na viongozi na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini Tanzania. Pamoja na hoja mbalimbali alizozungumza mojawapo ni kuondoa zuio la mikutano ya vyama vya kisiasa.

Niliisikiliza hotuba hiyo ya Rais Samia na ilipofika mwisho nilijikuta nina maswali mengi ya kutafakari na ningependa kupata majibu ya maswali hayo. Kama una majibu ya maswali haya naomba tusaidiane kuyatafakari na hatimaye kuyajibu.

1) Kwanini Rais Samia ameondoa zuio la mikutano ya kisiasa SASA, (Nasisitiza SASA - Why NOW?) wakati alishakaa zaidi ya mwaka madarakani? Kwanini hakuondoa zuio hilo wakati ule mara tu alipoingia madarakani, wakati kuna mambo aliyatolea maamuzi mapema mara tu baada ya kuingia madaraki? Mfano suala la chanjo ya Corona, kurejesha uhusiano na nchi za magharibi ambazo kabla zilibatizwa jina la 'mabeberu', kufuta kesi za baadhi ya waliotuhumiwa kufanya ufisadi, n,k.

2) Unadhani amesukumwa na nini kufanya uamuzi huu? Kwasababu anataka kutenda haki? anawapenda wananchi wake? Unadhani kwanini?

3) Kuhusu Katiba mpya, kwanini bado ana kigugumizi kuhusu katiba mpya? Rais ni mmoja wa watu wanaojua vema umuhimu wa katiba mpya kuliko yeyote, kwani yeye ndiye aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba, tukikumbuka uanzishwaji wa tume ya Jaji Warioba, kupatikana kwa rasimu ya Warioba hadi 'Katiba pendekezwa. Ina maana umuhimu wa katiba mpya ulishaonekana tangu wakati ule? Sasa kigugumizi cha katiba mpya kinatokea wapi?

Hebu tusaidiane kujibu na kutafakari maswali haya, ili tuweze kujenga nchi yetu
 
Acha woga, aliyewawega madarakani tayari amekufa kitambo na kuoza, jiandae na siasa za ushindani.
 
Kila jambo na wakati wake. Ameona wakati ni sasa kuruhusu. Hiyo ni kwasababu kulikuwa na msululu wa mazungumzo na majadiliano na wadau, pale mazungumzo yanapofikia mwisho inabaki utekelezaji.
 
Kwa watawala huchukua muda kuondoa kile kilichowekwa na mtangulizi wake taratibu kwa kuwa awali walikuwa pamoja na haileti picha nzuri kuondoa zuio ghafla itaonesha hawakuwa pomoja. Ingekuwa ni mpinzani kachukua madaraka mambo yangeondolewa haraka sana. Na ndivyo ilivyo siku wapinzani wakitwa madaraka wataondoa vizuizi vingi kwa muda mfupi katika utawala wao
 
Back
Top Bottom