Najua kuna wabaya wako wanajaribu kukushauri uchelewe kutoa pongezi kwa Ruto eti wakidai usubiri taratibu za ki mahakama zimalizike endapo Odinga ataenda Mahakamani!
Kama mshabiki wako ninayekutakia mema na mazuri naomba usiwasikilize, wengi wao ni watu wa yule mtu wasiokutakia mazuri. Marais wa South Africa, Zimbabwe, Nigeria wametoa pongezi tayari. Naomba uwe wa kwanza kwa Africa Mashariki kutoa pongezi za wazi kwa Ruto kwa sababu uchaguzi umeshafanyika na Ruto ndo ametangazwa mshindi.
Tengeneza rafiki wako sasa kwa maslahi makubwa ya Tanzania hapo baadae!
Asante.