Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria?

Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria?

Russia aliingia mkataba wa ushirikiano na urafiki baina yake na Syria kwenye miaka ya 80 huko, mikataba ambayo inatoa faida kwa nchi zote mbili na pia Russia ndio anaempatia silaha Syria za kupambana na waasi ambao wanaungwa mkono na nchi za magharibi. Miongoni mwa mikataba hiyo iliipatia Russia nafasi ya kuweka base yake hapo Middle East na kufurahia uwepo wa Base hiyo kwa muda wa miaka 49 bila ya kulipia chochote. Ndio maana Russia anaisupport na kuilinda Syria.
 
Ha ha ha haa ! Mkuu, nitake radhi ! Mimi ni pro- watanzania, waafrika, na watu wote wenye kuthamini ubinadamu ulimwenguni. Tena mimi ni pro- mtaka ustawi wa maendeleo chanya wa watu hao niliowataja. Ila kama kuwa mfuasi kindaki ndaki wa CCM na serikali yake kuna maanisha msimamo wangu huo wa ' pro-', hapo sina namna nakubaliana na wewe.

Tuko pamoja, Mkuu.
Mkuu Tujitegemee umeniruka futi 7 x 70 😅😂😂🤣😄!!

We bhana hata ukiwa Green Guard, shauri yako utakavyoburuzwa ICC, muhimu kwangu ni kwamba, linapokuja suala la JPM, naamini wewe utakuwa ni Mfuasi wa JPM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio Mfuasi wa JPM kutoka Kanda ya Ziwa!!!!

Na kama ni chama, basi utakuwa mfuasi wa CCM na sio Mfuasi wa Mwenyekiti wa CCM!!!
 
Anyway, sasa unajua ni wapi unapozingua?!!

Nahisi ukiona uzi wako una mamia ya comments ndo unajiona kama unajaza pesa
Ninajaza pesa? Hapana mkuu. Haya ni mawazo yako binafsi wewe pamoja na wengine wengi wa humu JF wasiopenda challenge...
 
Ninajaza pesa? Hapana mkuu. Haya ni mawazo yako binafsi wewe pamoja na wengine wengi wa humu JF wasiopenda challenge...
Sipendi challenge kivipi?!

Hoja uanzishe wewe, halafu mimi ndie nisipende challenge?! How come?!

Umehoji, nikakujibu kwa MIFANO with reference zisizo na shaka!!!

Sasa assume unauliza 1+1 sawa sawa na ngapi, nikakujibu tena kwa kushuka njia kwamba 1+1 = 2, halafu unakaza kwamba haiwezi kuwa 2...

Sasa ni nani hapo asiyependa challenge kama sio wewe usiyetaka kukubali ukweli labda kwavile una ukweli unaojua mwenyewe ambao hata hivyo haujitoshelezi?

Kwa bahati mzuri sana sina silika ya kumpinga mtu bila hoja! Na kama ni hoja inayohitaji reference, more often than not, LAZIMA nitaweka reference!!!

Maybe una tafsiri yako ya maana halisi ya mtu asiyependa challenge, kwa sababu for what I know, asiyependa challenge ni yule ambae atakachosema yeye LAZIMA wote wakikubali hata akithibitishiwa kwamba HAYUPO sahihi!

So, unaweza kutoa mfano wa kile ulichosema wewe au yeyote yule ambae hata baaada ya mimi kuthibitishiwa kwama you're RIGHT lakini bado niliendelea kung'ang'ania hoja yangu isiyo na mashiko!

Jibu hiyo paragraph ya mwisho!!!
 
Sipendi challenge kivipi?!

Hoja uanzishe wewe, halafu mimi ndie nisipende challenge?! How come?!

Umehoji, nikakujibu kwa MIFANO with reference zisizo na shaka!!!

Sasa assume unauliza 1+1 sawa sawa na ngapi, nikakujibu tena kwa kushuka njia kwamba 1+1 = 2, halafu unakaza kwamba haiwezi kuwa 2...

Sasa ni nani hapo asiyependa challenge kama sio wewe usiyetaka kukubali ukweli labda kwavile una ukweli unaojua mwenyewe ambao hata hivyo haujitoshelezi?

Kwa bahati mzuri sana sina silika ya kumpinga mtu bila hoja! Na kama ni hoja inayohitaji reference, more often than not, LAZIMA nitaweka reference!!!
Okay mkuu...
 
Russia aliingia mkataba wa ushirikiano na urafiki baina yake na Syria kwenye miaka ya 80 huko, mikataba ambayo inatoa faida kwa nchi zote mbili na pia Russia ndio anaempatia silaha Syria za kupambana na waasi ambao wanaungwa mkono na nchi za magharibi. Miongoni mwa mikataba hiyo iliipatia Russia nafasi ya kuweka base yake hapo Middle East na kufurahia uwepo wa Base hiyo kwa muda wa miaka 49 bila ya kulipia chochote. Ndio maana Russia anaisupport na kuilinda Syria.
Sawa mzee baba na bila shaka hiyo ndio base pakee ya Russia hapo middle east?
 
Hapo umeeleza vzr sana.
Saddamu alikuwa kibaraka wa marekani,,lakini tatizo ni kuwa iraq ilikuwa inakuja juu na kuwa tishio kwa israel kipindi hicho kuanzia miaka ya 90,iraq ilikuwa na uhusiano mzuri na marekani,lakini ilikuwa haijawa na amani na israel,kwani bado ikiwasaidia wapalestine,
Ilitakiwa ipatikane njia ya kuipunguza speed iraq,kwani ilikuwa ikija vizuri,kiuchumi na kijeshi hivyo kuwa tishio kwa israel,.
Saddam alikuwa na mgogoro na kuwait,,waarabu wenzie walimpiganisha na iran,vita ya miaka 8 na hawakuwa tayari kumu compensate,,saddam akataka kuvamia kuwait,,marekani wakamtega,,kisiri siri wakamoa ok,saddamu avamie kuwait mwaka 1991,first gulf war,
Alipovamia tu,saddamu kashangaa marekani wanamgeuka,
Wakamtwanga,japo hawakutaka kumpindua,,wakamwekea vikwazo ili kuua kabisa speed ya iraq kupiga hatua,,
Vikwazo vikadumu miaka 12,,lakini sardamu akaendelea kutawala,
Ndiposa 2003,likaja swala la WMD,
Hivyo tokea mwanzo,saddamu hakuwa swahiba mkubwa wa Russia.
 
sadamu alikuwa mlamba viatu wa USA wakati akipigana na Irani miaka ya 80, Usa ilimpa misaada sana baada ya vita kuisha akajiona mjanja kwenda kuivamia Israel yule kapigwa na israel, kwa kile ilicho mfanyia sadamu hiyo USA imetumiwa tu.

km USA ikikutumia jua ina mkono wa Israel, km ilivo leo saudia kwa USA kashog kafa wako USA limyaaaa
 
Short answer ni kwamba:-

George na CIA walifanikiwa kuudanganya ulimwengu kwamba Saddam anamiliki WMD to the point, hata UN Security Council ilivyokaa mwaka 2002 iliitaka Iraq iwe disarmed.

UN Security Council Permanent Members WOTE, including Russia walipiga kura in favor UN kuitaka Iraq iwe disarmed kupitia resolution ambayo ilisema wazi kwamba Iraq kutofuata resolution iliyotolewa ingekuwa ni jambo lisilokubalika na LAZIMA iwe disarmed!

So, ikaonekana Iraq "amegoma" kutii matakwa ya UN kumbe maskini ya Mungu hizo WMD hakuwa nazo but no one, including Russia believed Saddam!!

Na ni kutokana na hilo, ndo maana US walipoamua kuivamia Iraq kwa kigezo cha kusaka WMD, hakuna aliyekuwa tayari kumtetea!!!

Swali la msingi ni: How come taifa kama Russia nao waliamini madai ya CIA?!

Inawezekana Russia walifahamu suala la Iraq kuwa na materials zinazoweza kutengeneza WMD hasa ukizangatia hapo kabla Saddam aliwahi kutumia silaha za kemikali!

So, kutokana na hilo, Russia alikuwa na kila sababu ya kuamini inawezekana kweli Saddam alikuwa na WMD, kwahiyo akamuacha afe peke yake!!

Lakini kwa upande mwingine, Russia na Iraq hawakuwa Maswahib worth to risk kwa sababu, we all know, miaka michache tu nyuma Iraq alikuwa anapigana vita ya CIA dhidi ya Iran!
Uko sahihi ukirudi nyuma kidogo wakati wa vita ya Iraq na Iran. Kumbuka nmvita hii ilikuqa ya wakubwa Mmarekani akiwa nyuma ya Saddam na Mrusi nyuma ya Iran vita ilipigwa sana na Saddam akazidi ndipo Marekani wakampa Saddam mzigo wa Kemikali ili atumie kumaliza vita wa wakaenda UN wakatangaza siku ya kusimamisha vita ili watu waswali siku ya Ijumaa Saddam akatumia mzigo aliopewa na ndugu zake watu wakafa kama kuku sana Iran. Iran ikasitisha vita tokea hapo, tatizo likaja kuwa mgogoro kati ya Saddam na Marekani na akatumia yale yale makombora kupiga Israel. Israel akataka kuingia vitani Marekani akamzuia kihofia ingezuka vita ya kidini haswa pale mashariki ya kati ndipo wakaja na Resolution ile ya Condoriza. Warusi wakifahamu mchezo wote hivyo wao wakakaa pembeni, lkn pia kwa Mrusi kukaa pembeni kulichangiwa na hali ya kiuchumi kipinfi kile hakuwa vizuri na alikua ktk reformation. Kwa Syria ni kwamba Mrusi keshagain uchumi kwa sasa na anasapoti wengi sana sio Syria tu keshafika mlangoni kabisa kwa Marekani na kakaa pale Venezuela na kumbuka kapeleka Nuclear bombers zake pale TU 160 ndege hatari kabisa dunia kwa kipindi hiki, karata aliyoicheza hapa ni kama ile aliyoichezs Cuba kipindi kile, kuwa hiko karibu nawe ukizingua nainula kidogo juu kisha mambo yanaitika uko Washington.
 
Mbona alikuwa disarmed?
Sina uhakika kabisa kama alikua disarmed Syria zaidi kuna kiini macho kilichezeka pale mana baada ya pale kulifuata kichapo si cha mchezo kwa waasi baada ya ile Chemical Attack ya Douma. Allepo ilichapwa si mchezo na waasi wakakimbia na kusalimisha silaha wengi wao baada ya kuwa hawana namna na hawakua na njia nyingine ya kupokeq msaada wa sialaha mana kichapo kinaendelea huku Mrusi kaweka dolia hakuna kitu kukngia
 
Soma hapo chini;

Ilifanyika wapi na muda gani?
The destruction of Syria's chemical weapons began on 14 September 2013 after Syria entered into several international agreements which called for the elimination of Syria's chemical weapon stockpiles and set a destruction deadline of 30 June 2014.
 
Back
Top Bottom