Kwanini Serikali imeweka Mawakili wake kuwatetea akina Mdee? AG akichafuka wakubwa zake watabaki wasafi?

Wakina Halima hawajaishtaki CHADEMA pekee, wamemshtaki pia AG pamoja na NEC.
kwa taarifa ni kwamba akina mdee wamekimbilia mahakamani kuomba mahakama ipitie upya ifanye review ya utaratibu waliopitia chadema kuwafukuza uanachama
Na ni kama haukufuatilia hilo shaurila kina kovid nimeshangaa huyu Solicitor General na siyo AG bwana gabriel malata kujihusisha
kwa mujibu wa majukumu yake hahusiki .
kwa mujibu wa ishu za kina kovid hawajashtaki mtu wanataka tukutumia mahakama kuvunja katiba ya nchi.
Kama bunge lilivyofanya ila wajijue hawachomoki kwenye hii ishu
 
Kwa hiyo unamaanisha akina Kibatala pia walienda kuiomba mahakama isiwaondolee ubunge wao? vichwani mmejaa ug.oro tupu.

akina kibatala walienda mahakamani kwa niaba ya chama chao kwani ndiokilichofanya maamuzi ya kuwafukuza uanachama wanachama wake
sasa mshtaka mkuu wa serikali anamaslai gani watu waliofukuzwa uanachama chama chao cha siasa huko
Bwana Gabriel Malata hacha kujishushia hadhi kwa kutumika kipumbavu unatumia vibaya ofisi ya serikali na unashusha P yako uliyojijengea kama wakili wa serikali, kamishana wa kazi, na sasa solicitor general
 
Huwa nikihoji uwezo wa Waandishi wa Tanzania kama huyu Beatrice Kamugisha kuna watu wanashangaa!!
Katika kesi ambayo akina Halima Mdee wamefungua, AG (Attorney General) na NEC ni Respondents na lazima Mawakili wa Serikali na NEC wawepo yeye anasema wanawatetea akina Halima Mdee!!!!!!
Haya eti Affidavit imeohojiwa kwahiyo huko ni kuumbuliwa kwa Serikali?!!!
Hivi kwanini Nchi hii ina groom vila.za namna hii?!!!
 
Hakuna wakili wa serikali anatetea mtu binafsi.

Sheria inataka serikali ikishitakiwa AG awe part ya kesi.

NEC imeshitakiwa hivyo mawakili wa serikali lazima wawepo.
Chadema wameishitaki NEC? Wewe unaongelea nini?
 
Kna wkt kina Mdee walonekana kuilivuruga bunge Ndugai akawa akimtimua bungeni mara kw mara, wapinzani walionekana tatizo bungeni. Ss hv hao wanaoitwa Covid, wanang'ang'niwa na inayoitwa mihimili, yote.
Nlitegmea Bunge lingechklia taarifa zake toka kw msemaji rasmi wa chama kuwa ndizo final. Lkn inaelkea hawaziamini tena na ss hadi kuweka mawakili kuwatetea mahakamani kwa ghrma zetu. Imagine, serikali ya Tz kuwatetea wapinzani...duh!
Halafu hata kabla ya mahakma kutoa tamko lake, tayari Supika kawakingia kifua!
Ngekua mm ngewaacha wakate marufaa yao, washinde wasishinde shauri yao, Mradi sio wanachama. Inashngza serikali kutumia kodi zetu zote hizo kuwatetea watu walokataliwa walikotoka. Chama knasema hakiwatambui, Bunge na Serikali wanasema 'lazima muwatambue' ...dah!
 
Matumizi mabaya ya fedha za umma
 
Serikali ndiyo iliyowapeleka bungeni hao akina Halima
 
Huyu bibi inatakiwa tumtoe anatuharibia nchi yetu, mbona kule kwao Zanzibar hawafanyi haya maigizo?
 
Taahi.ra hilo lisikupotezee muda, hii mijitu hujitia kujua kila kitu wakati kuchwani empty kabisa, mfano huyu mleta mada hajui hata kama AG pia kashtakiwa kwenye hiyo kesi na ndo sababu ya kupeleka mawakili wa serikali.
kwani Nani aliyepeleka kesi mahakamani?, ni covid au CDM
 
Huyu bibi inatakiwa tumtoe anatuharibia nchi yetu, mbona kule kwao Zanzibar hawafanyi haya maigizo?
Huko Zanzibar kuna maridhiano ya kweli kina Zitto kila siku kujipendekeza, huku bara ndio anatuletea maigizo ya kijinga.
 
sasa kwenye hilo suala la kina mdee kuitaka mahakama kuangalia kama taratibu za katiba ya chadema imefuatwa .sasa hapo serikali (NEC) imeshtakiwa kivipi .
Hilo ni suala binafsi la hao kovid 19 na chama chao
Ndio NEC ni necessary party.

Yeye ndio anapokea majina na kuyapeleka Bungeni.

Hivyo akija mahakamani ataisaidia kujua ni kwa namna gani hao wabunge waliteuliwa.

Na sheria inasema pale serikali inaposhitakiwa lazima AG awe sehemu ya kesi.

Ndio kilichofanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…