Inakuaje Serikali ya nchi flani ijipange kuifuta nchi nyingine?
Hapa najiuliza sipati jibu. Taifa kutafuta NGUVU za kivita ukiwa na lengo ya kuzitumia sio kujilinda bali kwenda kuliangamiza taifa lingine ambalo liko zaidi 2000 km kutoka hapo ulipo.
Mbona Kuna mataifa MENGI ya kiislam tena yenye uelewa mkubwa kama Indonesia lakini hawana hayo malengo.
ALafu KWA nini aweke wazi, KWA nini asingefanya Siri ili mlengwa asijiandae?
Dunia inavitu vya ajabu kimojawapo ni huu msimamo wa kulifuta taifa lingine tena KWA kusema wazi.
Wajuvi mtujuze nini Msingi wa msimamo huu
Ukipata muda utasoma EZEKIELI 38 yote. Ezekiel nabii aliyeishi miaka 600 kabla ya Kristo alitabiri mambo ya siku za mwisho.
5. Uajemi, na Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo;
7. Ujiweke tayari, naam, jiweke tayari, wewe na majeshi yako yote waliokukusanyikia,
nawe uwe jemadari wao.
8. Na baada ya siku nyingi utajiliwa; katika miaka ya mwisho, utaingia nchi
iliyorudishiwa hali yake ya kwanza, baada ya kupigwa kwa upanga, iliyokusanywa toka
kabila nyingi za watu, juu ya milima ya Israeli, iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini
imetolewa katika kabila za watu, nao watakaa salama salimini wote pia.
-- kwa hiyo kifupi hii vita ni sehemu ya kutimia kwa unabii wa Ezekieli kuelekea kurudi kwa Yesu na mwisho wa dunia. Majina ya nchi kwenye hii sura yameandikwa kulingana na yalivyojulikana zamani. UAJEMI ni Iran ya sasa.