Kwanini sijawahi kuona ama kusikia mikutano ya dini Masaki, Ostebay ama Posta?

Kwanini sijawahi kuona ama kusikia mikutano ya dini Masaki, Ostebay ama Posta?

Makanisa mbona yapo mengi tu,labda mikutano wanakosa eneo la kufanyia mkutano maana huko masaki kupata uwanja kama wa Tanganyika Pakers..huezi pata vyote wamejenga.
Ila makanisa Kote huko yapo.

Screenshot_20220319-194055_Maps.jpg
 
Kweli hujaelewa mada
Mada nimeielewa anauliza kwanini wanaofanya mikutano wapo pembezoni mwa mji,lkn maeneo tajwa haifanyiki.

Nimejibu.
Hakuna maeneo ya kutosha kufanya hiyo mikutano.
Osterbay ,masaki na posta viwanja vya wazi vyote vimetumika.
Kama ni mikutano basi inafanyika ya kanisani mwao ndani maana huko kote alikotaja,makanisa yapo.
Karibu.
 
Jamii iliyoelimika kuna vitu huwa wanavipuuza na havifanyi kazi kwao kamwe wao wanadeal na fact.Hayo maeneo uliyoyataja mara nyingi unakuta wao wameisoma biblia au Quran na kama siasa wao ndio magwiji wa siasa hivyo huna cha kuwaambia sanasana ukiweka mikutano ya dini huko utaletewa polisi tu unapiga kelele
 
Nani amona makaburi yaliyofukuliwa ili 'wachawi' wale nyama ya maiti kama tunavyohubiriwa na makuhani hawa kwa makerubi wao?
 
Huko hata waganga wa kienyeji huwezi wapata, wanapatikana mitaa ya watu masikini.
 
Nashangaa hawa hasa watangaza dini wanaochipukia kwanini wote kutwa kujazana miji ya pembezoni mwa mji kwanini mitaa nikiyoitaja hawaendi?
Sijawahi kuona tangazo wala mkusanyiko kule mtu akihuburi injili
Ukikutana na waumini wa mwamposa,asilimia kubwa ni kada ya chini,wakazi wa mbagala,bunju,wengi shughuri zao ni mama ntilie,machinga,mabinti wanaotafuta waume,
Hakuna watu kutoka masaki,oysterbay,upsnga wanaowasha ma bmw,vogue,V8,yao na kwenda kwa mwamposa!
Watu maskini wanaenda kupewa sababu kwanini wao ni maskini,utaambiwa shetani anakushambulia,unapewa matumaini kwamba ukinywa maji ya baraka na kukanyaga mafuta,shida na magonjwa yataisha!!wenye nazo utawakuta Azania front,saint Joseph!!
 
Back
Top Bottom