Nashangaa hawa hasa watangaza dini wanaochipukia kwanini wote kutwa kujazana miji ya pembezoni mwa mji kwanini mitaa nikiyoitaja hawaendi?
Sijawahi kuona tangazo wala mkusanyiko kule mtu akihuburi injili
kule kuna watu wamejaa kiburi cha maisha, watu ambao kwa nje unawaona wamevaa nguo nzuri ila viunoni wame mahirizi, wamejaa machale na wengine majini na misukule wanaishi nayo. watu walioshinda kwa waganga kutafuta vyeo na pesa, wamezipata na wapo kifungoni kutoacha ushirikina kwasababu wakiacha tu shetani anabeba mali zote wanarudi kuishi manzese. jambo hili linawafanya wawe watumwa hadi siku ya kifo chao na wanaelekea moja kwa moja motoni kwa shetani baba yao.
masaki na oysterbay hakuna viwanja vya kuweka mikutano na kule wanakaa watu wenye hadhi/viongozi n.k. ni sawa na uzunguni zozote zile nchini. hao viongozi wengine wa serikali hawataki makelele, ukiweka mkutano tu watapiga tu simu polisi waje wauondoe. ni watu wanaokataa Neema ya Mungu, wanaona kama injili ni mambo ya kipuuzi kumbe katika upuuzi huohuo Mungu anaokoa watu. hao ni watu ambao wanaamini zaidi katika materialism kulili nguvu za Mungu, akiumwa anaamini tu kutibiwa na uzima wake upo kwenye mali zake kwamba zitamsaidia ndio maana hata kungekuwa na uwanja ukaweka mkutano kule wanaweza wasije kwasababu hawana njaa jikoni wala mifukoni, wanaweza kuwa na shida kiafya tu ila sasa hela ya hospitali wanayo, tofauti na ndugu zetu ambao hata hela ya hospitali hana sasa anageukia kwa Mungu. hao wa masaki hawajui tu kwamba hata ukiwa na hela ukakodi madoctor wote duniani wakutibu, uzima wako bado upo mikononi mwa Mungu ambaye ndiye Mungu huyo huyo wa wote. masikini kwa matajiri.
maisha ya duniani tunapita tu, makao yetu ni mbinguni kwa Mungu, whenever you live on this earth, try to figure out where you will spend your eternity. kuna sehemu mbili tu jehanum na uzimani. nafasi ya kuchagua aina ya maisha utakayoishi baada ya kifo ni sasa kabla hujafa, ukishakufa tu ni hukumu hakuna kuokoka hata ukiombewa na mapadre na maaskofu.
Okoka leo, mpe Yesu Maisha yako, atayabadilisha nawe utaupata uzima wa milele hapa duniani na ukifa mbinguni.