Kwanini Tangu waafrika tupate uhuru Hadi Sasa hakuna nchi Tajiri iliyofanikiwa

Kwanini Tangu waafrika tupate uhuru Hadi Sasa hakuna nchi Tajiri iliyofanikiwa

Tatizo ni kuwa na viongozi wasio na maono, ubinafsi
Kila mmoja anawaza madaraka,kupiga pesa ajitajirishe ye na ukoo wake mbaya zaidi wanaenda kuwekeza ulaya, ila sio kuweka Taifa mbele kwanza na kuwekeza kwenye nchi yake!
Ndo maana wako tayari Kwa gharama yyt kulinda vyeo,maslahi....

Hayo mambo ya dini uongo mnayasingizia tu ,huko walikoendelea Hawana dini?
Hata wewe ukipewa nafasi utact the same ni asili ya waafrika wote
 
Hatuna

  • Teknolojia
  • Masoko
  • Mitaji mikubwa

Wazungu walishare teknolojia yao na Mchina, check China alivyopiga hatua.

Afrika bado tunasafirisha Malighafi, kwenda Ulaya.

Kwasababu teknolojia yao hawajatupa.

Mitaji mikubwa hatuna, na bank zao hazitukopeshi sisi, wanapeana wenyewe ili waje kuwekeza huku.

Lakini pia, malighafi kama madini hatuna kabisa teknolojia ya kuyachimba kwa ukubwa, hatuna teknolojia ya kuyasafisha na pia hatuna masoko ya hayo madini.

Kwahiyo, kwa vyovyote lazima tuwe nyuma mpaka tukiweza kuiba teknolojia na mitaji ya Wazungu.
Hakuna kisingizio hapa.
Vyote vipo tele tu
 
Tatizo ni ngozi?

Ubongo?

Au tuliumbwa tuwe masikini na Tegemezi?

Au hii sehemu Mungu aliiweka kama mashambani pa dunia watu watoke kwingineko waje wapige pesa na kuondoka.

Maana Sasa hivi DUNIANI Kila rangi inayoamua kuendelea duniani inaendelea tena faster isipokuwa hii nyeusi rangi ya kichawa.

Hata Afrika kusaini inayoonekana kama imefanikiwa lakini waliofanikiwa ni Wazungu tu sio rangi nyeusi.

Jiji la Singapore Mwaka 1960s Wenda ilikuwa inazidiwa na jiji la mzizima lakini walipopata uhuru wakaamua Hadi Sasa ni kama wazungu.

Kuna shinda mahala wakuu.

Ni hilo tu
Matunduizi
South ni kati ya nchi tajiri duniani, nigeria ,algeria ,misri ni nchi zilizopiga hatua kubwa sana , au unazungumzia mafanikio ya mtu mmoja mmoja ?

Hata nchi kama angola ni nchi zilizovuna fedha nyingi ,shida tu ni viongozi wanaziangusha nchi zao walio wengi ,wanaruhusu mabeberu wazitumie nchi hizo kujinufaisha 70% alafu 30% ndio inabaki nchini
 
Tunajiuliza kwanini afrika nchi zetu bado masikini? Mimi nauliza ni nchi gani afrika viongozi wake wana amini au kuwa na mtazamo kuwa upo uwezekano nchi yao kuwa tajiri au kuwa na maendeleo makubwa?

Mitazamo yetu ndio inayofanya tuendelee kubaki hivi tulivyo, hata kwenye maisha binafsi ya mtu mmoja mmoja mitazamo ina nafasi kubwa sana.
Hakuna nchi yoyote Wala kingozi wa namna hiyo. Umasikini wa akili na fikra na mtazamo huu ndio umasikini
 
Kuna watawala vibaraka, wanaotafuta shortcut.

Mtu anaiba nchini kwake, aningia mikataba ya kikoloni, pesa anaenda kuweka huko huko Ulaya ananunua na majumba Ulaya.

Anaona hana sababu ya kuhangaika kujenga nchi yake, wakati anaiba pesa anaishi Ulaya sehemu ambayo tayari ilishajengwa.
Nini jukumu la wananchi wanaoibiwa wanashindwa nini kuwawajibisha wezi, mbona wananchi wa ulaya wanaweza kulinda raslimali zao
 
Hatuna

  • Teknolojia
  • Masoko
  • Mitaji mikubwa

Wazungu walishare teknolojia yao na Mchina, check China alivyopiga hatua.

Afrika bado tunasafirisha Malighafi, kwenda Ulaya.

Kwasababu teknolojia yao hawajatupa.

Mitaji mikubwa hatuna, na bank zao hazitukopeshi sisi, wanapeana wenyewe ili waje kuwekeza huku.

Lakini pia, malighafi kama madini hatuna kabisa teknolojia ya kuyachimba kwa ukubwa, hatuna teknolojia ya kuyasafisha na pia hatuna masoko ya hayo madini.

Kwahiyo, kwa vyovyote lazima tuwe nyuma mpaka tukiweza kuiba teknolojia na mitaji ya Wazungu.
Sababu za kipumbavu hizi..... Vyote hivyo unavyovisema hawajashushiwa kama muujiza....waliumiza vichwa...kupasuka na kutatua matatizo yao....wangekaa kisubiri wawe navyo kama tunavyoamini kuwa hatuna....halafu tumekaa na kusema hatuna....nani atakuletea !


Sisi ni wavivu na tunataka shortcut.....ile lala maskini uamke utajiri huu hapa.... kuhangaika no.!
Tuna roho mbaya mno....anayejua hataki wengine wajue.....kuharibiana na kurudishana nyuma....kiufupi umimi ni mwingi kuliko usisi....yaani mtu anataka kuvimba na v8 sio sababu anaahitaji ila ili awakoshe maskini....yeye aonekane amepatia....
Niamini kuwa aliyemuuza mtumwa ni mwafrika na hata leo anayekwamisha Africa ni mwafrika.....labda niseme hivi aliyemuua mwendazake, sankara, ghadafi na wengineo na anayemtafuta traore ni mwafrika mwenzie kwa kitika alichopewa....(Roho mbaya na kutothaminiana) Uchu wa mali za kuilimbikia.....
Mwisho kabisa hapa Tanzania mpaka sasa tumeishaona system iliyopo imefeli na asilimia kubwa tunaona na kujua.....je nani na lini tutasimama maana kwa box tumeishaona haiwezekani .....je tuchukue mkondo upi kubadili system na sio lazima waingie wapinzani but system ibadilike viruses wauwawe.....je lini na nani nani tutasimama bila kwa wingi bila hofu ya kupotezwa....sio anatoka mmoja wawili ....kumi wakipotezwa huoni chochote kama vile damu yao si chochote.....!
 
Sababu za kipumbavu hizi..... Vyote hivyo unavyovisema hawajashushiwa kama muujiza....waliumiza vichwa...kupasuka na kutatua matatizo yao....wangekaa kisubiri wawe navyo kama tunavyoamini kuwa hatuna....halafu tumekaa na kusema hatuna....nani atakuletea !
Safi sana.

Kwahiyo, serikali wewe inakuzuia nini, kubuni kama huo uwezo unao???
Sisi ni wavivu na tunataka shortcut.....ile lala maskini uamke utajiri huu hapa.... kuhangaika no.!
Tuna roho mbaya mno....anayejua hataki wengine wajue.....kuharibiana na kurudishana nyuma....kiufupi umimi ni mwingi kuliko usisi....
Mambo ya ubunifu ni tofauti na utajiri.

Wabunifu wengimwa Ulaya na Marekani walikufa masikni.

Kwahiyo, tenganisha hoja yako kati ya umasikini na ubunifu.
yaani mtu anataka kuvimba na v8 sio sababu anaahitaji ila ili awakoshe maskini....yeye aonekane amepatia....
Kama hilo V8 kanunua kwa pesa yake hakuna shids.

Ila kama ni serikali ubunifu wa teknolojia hauwahusu
Niamini kuwa aliyemuuza mtumwa ni mwafrika na hata leo anayekwamisha Africa ni mwafrika.....labda niseme hivi aliyemuua mwendazake, sankara, ghadafi na wengineo na anayemtafuta traore ni mwafrika mwenzie kwa kitika alichopewa....(Roho mbaya na kutothaminiana) Uchu wa mali za kuilimbikia.....
Kelele za biashara ya utimwa zilishapita.

Mida ulishapita, maisha lazima yaendelee
 
Hata wewe ukipewa nafasi utact the same ni asili ya waafrika wote
No ,usinisemee
Ht ktk hao wapo wazuri wachache ila mfumo unawapiga vita!

Kwani huoni ht maofisini aliye vzr anasimamia haki anaonekana mbaya?
Kwahiyo katikati ya hao Mungu anao wazuri tu wenye nia njema ila wanazidiwa na hao wengine
 
Jibu ni rahisi sana, mfano mzuri uko mbele ya macho yako angalia utawala wa serikali ya ccm na wote wanao waunga mkono ndio utapata jibu sahihi kwa nini afrika ni maskini na itaendelea kua maskini
 
Back
Top Bottom