Kwanini Tangu waafrika tupate uhuru Hadi Sasa hakuna nchi Tajiri iliyofanikiwa

Kwanini Tangu waafrika tupate uhuru Hadi Sasa hakuna nchi Tajiri iliyofanikiwa

Kutokana na historia ugumu unaongezeka.

Tukikuwa na matatizo ila matatizo mengine tumerithi, kama mambo ya ubepari, ujamaa na dini.

Ncji nyingi za kibepari hao mabepari hawakuondoka.

Kwahiyo, nchi yako inaweza kuonekana ni tajiri kumbe ni wao ndio matajiri nchini kwako na raia wako hawanufaiki kitu.
Mabepari ndio uleta maendeleo kwenye nchi kupitia ajira,upatikaji wa uhakika wa masoko,ulipaji kodi nk
 
Safi sana.

Kwahiyo, serikali wewe inakuzuia nini, kubuni kama huo uwezo unao???

Mambo ya ubunifu ni tofauti na utajiri.

Wabunifu wengimwa Ulaya na Marekani walikufa masikni.

Kwahiyo, tenganisha hoja yako kati ya umasikini na ubunifu.

Kama hilo V8 kanunua kwa pesa yake hakuna shids.

Ila kama ni serikali ubunifu wa teknolojia hauwahusu

Kelele za biashara ya utimwa zilishapita.

Mida ulishapita, maisha lazima yaendelee
Fuatilia kwanza ni vumbuzi ngapi za hapa hapa kwenu zimeuwawa na mawazo mgando badala ya kuziboresha halafu njoo mtetee huyo serikali,
Wabunifu ( individual) kufa masikini sio hoja ila ubunifu wao umeleta mabadiliko chanya kwenye mataifa yao na kuendeleza mataifa yao....sio lazima wote tuwe matajiri(ukwasi) ila ni lazima wote tupate mahitaji muhimu(unayajua)
V8 siongelei ya kwako..... naongelea iliyoagizwa kwa kodi yako na yangu kisa Barabara za huku Africa ni mbovu....lakini kumbe tungeanza na Barabara tusingehangaika na v8 maana wa namtumbo angeleta bidhaa zake nanenane,au ilala bila shida na huyu wa v8 angeondoka hata na premio na akafika huko lukozi, mkuzi, bushangaro, au kibimba bila hofu ya Barabara!
Utumwa ulishapita but tumejifuza lolote....leo anayemuua mkongo ni mkongo, msudani kwa msudani, msomali vilevile mrundi na safu inaendelea....ukiwauliza lawama wanatupiwa mabeberu si ufala huo!
 
Mabepari ndio uleta maendeleo kwenye nchi kupitia ajira,upatikaji wa uhakika wa masoko,ulipaji kodi nk
Ni suala la uchaguzi.

Bepari wa kwanza ni serikali.

Spender mkubwa ni serikali.

Na mwajiri mkubwa duniani kote ni serikali.

Hizo serikali ndio zinatengeneza hao watu.

Kwahiyo, si lazima bepari awe mmoja.

Staye capitalism ubepari pia, ambao hufanywa kwa manufaa ya wengi
 
Mnaongelea mataifa ya wazungu na watu weupe wa mbali huko, mbona humu humu tu nchini bado watu hawana akili timamu za kuchochea hayo maendeleo.

Jitu linaloshinda kutwa kushabikia mipira na ubishani wa simba+yanga unategemea jitu la hivi lifanikiwe na kuchochea maendeleo ya nchi?.

50% ya muda wa waafrika wengi kwa week nzima unatumika au kuishia makanisani/misikitini huko badala ya kufanya kazi mnategemea taifa la watu hawa liendelee?.

Media zote asubuhi mpaka kesho asubuhi hakuna cha maana wanachoweka zaidi ya vipindi vya kutukuza ngono, uzinzi, kamari, miziki, habari za umbea, uchochezi, chuki, kiki za kishamba, udaku na upuuzi wa kila namna bila kusahau media zinazoshinda kutoa vipindi visivyoeleweka zaidi ya uchawa na kusifia upuuzi, yaani kila mahala pameoza

Taifa ambalo vijana na wasomi wanapambana ili wapate ajira serikalini wapate wepesi wa kuiba na kujitajirisha na si kulitumikia taifa, mnadhani kuna maendeleo hapo?

Taifa ambalo watu wako bize kushabikia siasa za kipuuzi za Ccm+chadema, watu wanafarakana kisa vyama vya siasa na wengine wanatoana roho kisa siasa, kwa namna hii watu hawa wakipata uongozi kuna maendeleo?.

Taifa ambalo si wasomi wa elimu na ukufunzi pekee ambao unaweza sema wameelimika na kuyajua mengi, hata hawa pia wameoza akili bado zinawaza mambo yaleyale ya mkoloni, yaani inashangaza tunapodai mabadiriko ya mifumo ya elimu huku wadau wa mabadiriko hayo tunawahusisha walimu ambao kwa upuuzi wao wamechangia taifa la wajinga kufika hapa na wala hawashituki wao wako bize kudai ongezeko la maslahi yao huku wakiendelea kulididimiza taifa kwa kuzalisha vilaza takataka wafananao na wao.

Taifa hili na Afrika kiujumla imeoza kila mahala, kuanzia ngazi ya familia mpaka ikulu ya raisi pameoza, hakuna unafuu, inawezekana vipi mtu unayeipenda nchi yako unakwenda kusaini mikataba ya hovyo itakayoinyonya nchi yako na ya wazawa wako na kuwatajirisha watu wa mbali huko? Je huku sio kuoza akili?.

Mabadiriko ya Afrika hayatakiwi kubase katika mifumo ya kiuchumi na kisiasa pekee bali mpaka kijamii kuwe na control ya mafundisho ya maadili mema, bila kusahau control ya dini na imani chafu(ukristo+uislamu) zinazolenga kuwaharibu akili watoto.

Afrika tulichofanikiwa kutoka ktk ukoloni na utumwa ni uhuru wa kimwili tu lakini akili bado tuko kubaya zaidi ya walikokua babu zetu.

Maendeleo ya Afrika yataanza na mabadiriko ya fikra za waafrika ndipo mengine yatafuata hakuna mchawi hapo ni sisi wenyewe kwa ushenzi wetu.
Kaka sikusoma yooote ilaaa dah nakosa cha kuchangia watu wapitie comment yako tufunge mjadala big up
 
Wakati waislam wengi hasa waarabu sio wachapakazi kama sisi watu weusi na siamini kama wanatuzidi akili. Tatizo ni nini?
Tatizo ni fikra zetu zilivyo. Tunaamini sisi hatuwezi kufanikiwa kwa chochote pia Afrika hatuna umoja kama walionao UAE na EUROPE. Nilitegemea bunge la AU ndo likemee ufisadi hapa Afrika lakini chakushangaza bunge la EU ndo linafanya hii kazi imagine hata kesi ya Lisu imajadiliwa na EU.
 
Fuatilia kwanza ni vumbuzi ngapi za hapa hapa kwenu zimeuwawa na mawazo mgando badala ya kuziboresha halafu njoo mtetee huyo serikali,
Toa mifano hata miwili
Wabunifu ( individual) kufa masikini sio hoja ila ubunifu wao umeleta mabadiliko chanya kwenye mataifa yao na kuendeleza mataifa yao....
Sawa.

Sasa hapa kwenu mbona hamfanyi huo ubunifu, mnataka serikali ndio ifanye???

Huko Ulaya ni serikali ndio zilifanya ubunifu??
sio lazima wote tuwe matajiri(ukwasi) ila ni lazima wote tupate mahitaji muhimu(unayajua)
Sasa hili linahusiana nini na matumizi ya raslimali, hasa uchimabji, mauzo, mitaji mikubwa, teknolojia na masoko??
V8 siongelei ya kwako..... naongelea iliyoagizwa kwa kodi yako na yangu kisa Barabara za huku Africa ni mbovu....
V8 ndio italeta teknolojia ya matumizi ya raslimali?
lakini kumbe tungeanza na Barabara tusingehangaika na v8
kwahiyo ukijenga barabara, ndio matumizi bora ya raslimali?
maana wa namtumbo angeleta bidhaa zake nanenane,au ilala bila shida na huyu wa v8 angeondoka hata na premio na akafika huko lukozi, mkuzi, bushangaro, au kibimba bila hofu ya Barabara!
Kwahiyo Namtumbo wakileta bidhaa, nchi itakuwa kama Ulaya?
Utumwa ulishapita but tumejifuza lolote....leo anayemuua mkongo ni mkongo, msudani kwa msudani, msomali vilevile mrundi na safu inaendelea....ukiwauliza lawama wanatupiwa mabeberu si ufala huo!
Hoja ni ile ile, hayo madini yanayoleta vita huko Congo, yanauzwa wapi?

Yanasafishwa wapi?

Yanachimbwa kwa teknolojia ya wapi??
 
Binafsi namshukuru mkoloni maana mabaki ya shule zake ndio nilisomea. Mkoloni mtu safi sana.
Unaona ndexi kama huyu kwa vile yy kasoma kwa msaada wa kikoloni anaona yule atae zaliwa kesho poa tu abakie na shida zake ishu ya sustainability haimuhusu kwa comment hz hatudiki
 
Ukisoma kitabu Cha RISE AND FALL OF GREAT EMPIRES (1500-2000) by Paul Kennedy itakupatia picha pana sana ni kwanini Africa ni bara maskini.

Wenzetu wako serious sana na mustakabali wa maisha Yao na sio kumuachia Mungu na maombi ya kijanja janja ya hawa watumishi feki.

Angalia huo mchanganuo halafu tafuta Kuna nchi ngapi za kiafrika humo👇
 

Attachments

  • Screenshot_20250416-221341.jpg
    Screenshot_20250416-221341.jpg
    405.7 KB · Views: 21
Kuna mtu alisema hata wazungu wakija bara letu nasi twende kwao, ndani ya miaka 10, kule kwao tunapafanya panakuwa kama Africa, na wao Africa wataifanya iwe kama kule kwao!
Yote yanawezekana
 
Utafanikiwaje sasa wakati utajiri wako wote ulishanyonywa na wazungu ukaachiwa makopo matupu na umasikini mkubwa!
 
Kuna mambo muhimu ambayo wengi hawayajui:

Wataalam wote wa asili ya mwanadamu na maendeleo wanakubaliana kuwa bara la Afrika ndiyo mwanzo wa maisha ya mwanadamu.

Yaani yapata miaka 200,000 iliyopita, wanadamu wote waliishi bara la Afrika. Kutokana na matatizo mbalimbali, ikiwemo ukame, na hamu ya kuijua zaidi Dunia, kizazi chenye udadisi na chenye uthubutu, kilianza kusafiri kutoka Kusini mwa Dunia, kuelekea Kaskazini.

Kizazi hiki baada ya kufika maeneo yenye baridi kali sana, taratibu miili yao ilianza kubadilika ili kuyakabili mazingira. Ngozi zao zilianza kuwa nene na zenye mafuta mengi kwa ndani ili kutengeneza protection ya mwili dhidi ya baridi kali. Ngozi zao zilianza kubadilika rangi pia. Mpaka leo wale wazungu wanaoishi maeneo ya paridi kali sana, ngozi zao ni nyeupe, wakati wale waishio maeneo ya baridi ya wastani, ngozi zao ni brown.

JIBU KWA SWALI LAKO:

1. Waafrika ni kizazi kilichoachwa barani Afrika. Ni kizazi cha watu waliokuwa waoga na ambao hawakuwa na uthubutu.

Mtu mwoga, asiye na uthubutu hawezi kuwa na mafanikio makubwa. Mtu mweusi ni kizazi cha watu waoga, waliokuwa wamekosa uthubutu. Mapungufu haya wameyarithisha kwa vizazi vyao.
Inawezekana
 
Tunajiuliza kwanini afrika nchi zetu bado masikini? Mimi nauliza ni nchi gani afrika viongozi wake wana amini au kuwa na mtazamo kuwa upo uwezekano nchi yao kuwa tajiri au kuwa na maendeleo makubwa?

Mitazamo yetu ndio inayofanya tuendelee kubaki hivi tulivyo, hata kwenye maisha binafsi ya mtu mmoja mmoja mitazamo ina nafasi kubwa sana.
Upo sahihi
 
Back
Top Bottom