Kwanini Tangu waafrika tupate uhuru Hadi Sasa hakuna nchi Tajiri iliyofanikiwa

Kwanini Tangu waafrika tupate uhuru Hadi Sasa hakuna nchi Tajiri iliyofanikiwa

Huwa nikiangalia zile clips za wahzabe wanavyoshindwa kufungua mfuniko wa chupa ya soda na kuishia kukata chupa na kisu huwa najiuliza sana maswali mengi kuhusu sisi waafrika.
Kivipi sasa wale ndo watu wenye furaha duniani Yale ndo maisha halisi,wanaishi kwa kufuata asili.
Hawawazi Kodi, school fees, michepuko, usaliti,danga,ccm chadema, mpira, club.
Wanaishi maisha halisi ya utulivu na amani
 
Mnaongelea mataifa ya wazungu na watu weupe wa mbali huko, mbona humu humu tu nchini bado watu hawana akili timamu za kuchochea hayo maendeleo.

Jitu linaloshinda kutwa kushabikia mipira na ubishani wa simba+yanga unategemea jitu la hivi lifanikiwe na kuchochea maendeleo ya nchi?.

50% ya muda wa waafrika wengi kwa week nzima unatumika au kuishia makanisani/misikitini huko badala ya kufanya kazi mnategemea taifa la watu hawa liendelee?.

Media zote asubuhi mpaka kesho asubuhi hakuna cha maana wanachoweka zaidi ya vipindi vya kutukuza ngono, uzinzi, kamari, miziki, habari za umbea, uchochezi, chuki, kiki za kishamba, udaku na upuuzi wa kila namna bila kusahau media zinazoshinda kutoa vipindi visivyoeleweka zaidi ya uchawa na kusifia upuuzi, yaani kila mahala pameoza

Taifa ambalo vijana na wasomi wanapambana ili wapate ajira serikalini wapate wepesi wa kuiba na kujitajirisha na si kulitumikia taifa, mnadhani kuna maendeleo hapo?

Taifa ambalo watu wako bize kushabikia siasa za kipuuzi za Ccm+chadema, watu wanafarakana kisa vyama vya siasa na wengine wanatoana roho kisa siasa, kwa namna hii watu hawa wakipata uongozi kuna maendeleo?.

Taifa ambalo si wasomi wa elimu na ukufunzi pekee ambao unaweza sema wameelimika na kuyajua mengi, hata hawa pia wameoza akili bado zinawaza mambo yaleyale ya mkoloni, yaani inashangaza tunapodai mabadiriko ya mifumo ya elimu huku wadau wa mabadiriko hayo tunawahusisha walimu ambao kwa upuuzi wao wamechangia taifa la wajinga kufika hapa na wala hawashituki wao wako bize kudai ongezeko la maslahi yao huku wakiendelea kulididimiza taifa kwa kuzalisha vilaza takataka wafananao na wao.

Taifa hili na Afrika kiujumla imeoza kila mahala, kuanzia ngazi ya familia mpaka ikulu ya raisi pameoza, hakuna unafuu, inawezekana vipi mtu unayeipenda nchi yako unakwenda kusaini mikataba ya hovyo itakayoinyonya nchi yako na ya wazawa wako na kuwatajirisha watu wa mbali huko? Je huku sio kuoza akili?.

Mabadiriko ya Afrika hayatakiwi kubase katika mifumo ya kiuchumi na kisiasa pekee bali mpaka kijamii kuwe na control ya mafundisho ya maadili mema, bila kusahau control ya dini na imani chafu(ukristo+uislamu) zinazolenga kuwaharibu akili watoto.

Afrika tulichofanikiwa kutoka ktk ukoloni na utumwa ni uhuru wa kimwili tu lakini akili bado tuko kubaya zaidi ya walikokua babu zetu.

Maendeleo ya Afrika yataanza na mabadiriko ya fikra za waafrika ndipo mengine yatafuata hakuna mchawi hapo ni sisi wenyewe kwa ushenzi wetu.
Inauma na kushangaza baada ya miaka 60 ya uhuru Mrisho Gambo anapanda V8 kuelekea kwenye ufunguzi wa kidaraja cha mbao
 
South ni kati ya nchi tajiri duniani, nigeria ,algeria ,misri ni nchi zilizopiga hatua kubwa sana , au unazungumzia mafanikio ya mtu mmoja mmoja ?

Hata nchi kama angola ni nchi zilizovuna fedha nyingi ,shida tu ni viongozi wanaziangusha nchi zao walio wengi ,wanaruhusu mabeberu wazitumie nchi hizo kujinufaisha 70% alafu 30% ndio inabaki nchini
Generalization ndicho alichofanya but kiukweli hizo ulizotaja ni asilimia chache sana ys mifano bora ya nchi zenye nafuu kstika Afrika.
 
Nchi yetu watu milioni 65 kama mmeshidwa kuendesha mwendo kasi hii bado unaitaji ushaidi mwingine kwamba waafrika sio binadamu kamili
 
Kipi kinacho wazuia nanyi kurithisha watoto wenu au mnarithishana ujinga tu na kuamini kila mtu atafute mali zake.
Mifumo bro. Yaani kama mtoto wako kasoma kayumba kuanzia primary hadi secondary na isitoshe chuo kasomea hapa nafasi zake za kutoboa zinakuwa finyu ukilinganisha na mtoto wa mhindi aliyesoma International primary na secondary halafu chuo akasomea nchi za Ulaya. Na kumbuka hao wahindi wanaconnection na viongozi wa serikali na wana makampuni yao kwahiyo watoto wao ni rahisi kupata kazi.
 
Tatizo ni ngozi?

Ubongo?

Au tuliumbwa tuwe masikini na Tegemezi?

Au hii sehemu Mungu aliiweka kama mashambani pa dunia watu watoke kwingineko waje wapige pesa na kuondoka.

Maana Sasa hivi DUNIANI Kila rangi inayoamua kuendelea duniani inaendelea tena faster isipokuwa hii nyeusi rangi ya kichawa.

Hata Afrika kusaini inayoonekana kama imefanikiwa lakini waliofanikiwa ni Wazungu tu sio rangi nyeusi.

Jiji la Singapore Mwaka 1960s Wenda ilikuwa inazidiwa na jiji la mzizima lakini walipopata uhuru wakaamua Hadi Sasa ni kama wazungu.

Kuna shinda mahala wakuu.

Ni hilo tu
Matunduizi
IMG-20250515-WA0029.jpg
 
Mifumo bro. Yaani kama mtoto wako kasoma kayumba kuanzia primary hadi secondary na isitoshe chuo kasomea hapa nafasi zake za kutoboa zinakuwa finyu ukilinganisha na mtoto wa mhindi aliyesoma International primary na secondary halafu chuo akasomea nchi za Ulaya. Na kumbuka hao wahindi wanaconnection na viongozi wa serikali na wana makampuni yao kwahiyo watoto wao ni rahisi kupata kazi.
Hao wabongo matajiri wa mabus,na malori, mahotel,nk
Kina king msukuma,Kishimba walisoma international school ipi.
Kutoboa na kusoma shule ni maisha maiwili tofauti
 
Endeleeni na ujinga wenu na kurithishana uchawi lakini sio utajiri.
 
Hao wabongo matajiri wa mabus,na malori, mahotel,nk
Kina king msukuma,Kishimba walisoma international school ipi.
Kutoboa na kusoma shule ni maisha maiwili tofauti
Nakubali kuna wabongo wametoboa na wamesoma shule za kawaida. Ila hapa tunaongelea in general ukisoma International chances za kutoboa ni kubwa.
 
Mkoloni mweusi ni mkoloni hatari, mbaya, mbinafsi, mzandiki, mnyonyaji mno kuliko mkoloni mweupe.

Siku Africa ikikomesha wakoloni weusi, ndivyo utajiri utakapojidhihirisha.
 
Afrika yani sisi weusi kuna vitu vingi sana tumefichwa na hawa weupe hasa TEKNOLOJIA. lakini wa kumlaumu zaidi na zaidi ni MUNGU, kwani ndie ameamua iwe hivi kutunyima maarifa.
 
Afrika yani sisi weusi kuna vitu vingi sana tumefichwa na hawa weupe hasa TEKNOLOJIA. lakini wa kumlaumu zaidi na zaidi ni MUNGU, kwani ndie ameamua iwe hivi kutunyima maarifa.
 
Tatizo ni akili ndogo za kuamini ktk dini za kuja uislam na ukristo kwamba ndiyo za Mungu na ndizo zitakupa maendeleo kwa maombi kupitia mohamad na yesu wa mchongo
 
Tatizo ni akili ndogo za kuamini ktk dini za kuja uislam na ukristo kwamba ndiyo za Mungu na ndizo zitakupa maendeleo kwa maombi kupitia mohamad na yesu wa mchongo
Mbona hata hao wachina wahindi wanadini zao tena dini zenyewe wanaamini udongo mende hata ng'ombe. Afadhalj hata hizi kidogo zina logic.

Tatizo ni kubwa kuliko dini mkuu. Tatizo ni nini?
 
Back
Top Bottom