Kwanini Tangu waafrika tupate uhuru Hadi Sasa hakuna nchi Tajiri iliyofanikiwa

Kwanini Tangu waafrika tupate uhuru Hadi Sasa hakuna nchi Tajiri iliyofanikiwa

Waafrika wamezidiwa akili mbali kabisa na wachina,wakorea,wajapan
Mkuu hayo ni mambo ya kihistoria kutokana experience zetu za maisha ndio linalifanya uone kama wametuzidi akili, sidhani kama ukiwachukua watoto wa hayo mataifa kisha uje kuwalea na kukulia afrika kama utaona hizo akili.
 
Hawaelewi,kwanza tafsiri ya waafrika kuhusu maendeleo kabla ya ukoloni ni tofauti.
Waafrika halisi ni wahazbe na bushman waulize kuhusu maana ya maendeleo watakwambia ni uhakika wa kula na kulala.
Huwa nikiangalia zile clips za wahzabe wanavyoshindwa kufungua mfuniko wa chupa ya soda na kuishia kukata chupa na kisu huwa najiuliza sana maswali mengi kuhusu sisi waafrika.
 
Hatuna

  • Teknolojia
  • Masoko
  • Mitaji mikubwa

Wazungu walishare teknolojia yao na Mchina, check China alivyopiga hatua.

Afrika bado tunasafirisha Malighafi, kwenda Ulaya.

Kwasababu teknolojia yao hawajatupa.

Mitaji mikubwa hatuna, na bank zao hazitukopeshi sisi, wanapeana wenyewe ili waje kuwekeza huku.

Lakini pia, malighafi kama madini hatuna kabisa teknolojia ya kuyachimba kwa ukubwa, hatuna teknolojia ya kuyasafisha na pia hatuna masoko ya hayo madini.

Kwahiyo, kwa vyovyote lazima tuwe nyuma mpaka tukiweza kuiba teknolojia na mitaji ya Wazungu.
Mentality tatizo la msingi la waafrika waarabu hawana technology lakini wanafanya collaboration na wazungu kila pande inapata faida
 
Mentality tatizo la msingi la waafrika waarabu hawana technology lakini wanafanya collaboration na wazungu kila pande inapata faida
Mwafrika akiingia makataba na mzungua au mchina au mwarabu ni win loose contract ikiwa taasisi inayoingia mkayaba viongozi wake watahakikishiwa ulaji binafs.
 
Tatizo ni ngozi?

Ubongo?

Au tuliumbwa tuwe masikini na Tegemezi?

Au hii sehemu Mungu aliiweka kama mashambani pa dunia watu watoke kwingineko waje wapige pesa na kuondoka.

Maana Sasa hivi DUNIANI Kila rangi inayoamua kuendelea duniani inaendelea tena faster isipokuwa hii nyeusi rangi ya kichawa.

Hata Afrika kusaini inayoonekana kama imefanikiwa lakini waliofanikiwa ni Wazungu tu sio rangi nyeusi.

Jiji la Singapore Mwaka 1960s Wenda ilikuwa inazidiwa na jiji la mzizima lakini walipopata uhuru wakaamua Hadi Sasa ni kama wazungu.

Kuna shinda mahala wakuu.

Ni hilo tu
Matunduizi
Kusoma ni jambo la kwanza na kuelimika ni jambo la pili. Je tunaweza unganisha mambo yote kwa wakati mmoja?

Nasikitika kusema kwa mtazamo wangu tuna graduate wenye makaratasi ( vyeti ) visivyokuwa na tija katika taifa lao. Chukulia mfano Tulia na elimu yake na anayoyaongea ( tuweke uvyama pembeni )
 
Nikiongelea Tz nitamlaumu Nyerere.
Yeye baada ya Uhuru tu akaanza fukuza watu, hakusomesha watu, akawajengea viwanda, viwanda vikafa
 
Hata kasumba ya dini inaleta umasikini. Mf. Ukipigwa shavu la kulia mgeuzie na la kulia. Maisha mazuri ni mbinguni hapa tunapita njia tu. Angalia Wachina hawana mda na maombi, wao ni kazi tu, mwafrika anakesha na maombi.
 
Hii ni kanuni moja unaweza kuiacha ukashika nyingine nyingi za maendeleio.
Mfano Wayahudi matajiri dini pia imesababisha wakawa mabilionea hasa vitabu vya agano la kale.
 
Tatizo la msingi la waafrika ni mentality
Kilichowafanya waarabu kuwa na maendeleo ni dini ya kiislam.
Hata nchi za Morocco Misri Algeria Libya Tunisia Mauritania angalau wananafuu ya maisha kuliko nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ni dini ya uislam.
Kwa maana ya kupitia mafundisho ya dini angalau viongozi wao wanawajali wananchi kupitia udugu wa kiislam kupitia dini wao hawana mkubwa wala mdogo hivyo mambo kama dhuluma, ufisadi, wizi, kuiba pesa na kuficha ulaya hayapo sababu viongozi na wananchi wote wapo chini ya mfumo mmoja wa dini.
Kivipi dini inaleta maendeleo? Kuna nchi kama Mali na Senegal zina waislamu zaidi ya 90% lakini maskini, kama dini inaleta maendeleo why isiplay party na hizo nchi .
 
Mentality tatizo la msingi la waafrika waarabu hawana technology lakini wanafanya collaboration na wazungu kila pande inapata faida
Shida ni wahuni, wabinafsi mnaowapeleka ku-negotiate mikataba na mabepari.

Bepari siyo mjomba wako.
 
Mimi ni mwafrika tena mweusi,nadhani waafrika walio wengi tunasumbuliwa na mambo ya kutojali hata kama tunaelewa madhara au faida ya jambo.

Pili matumizi na mapato hayaoani.Tunapenda luxury while we cannot afford it.

Tatu tunashindwa kujituma hata pale mazingira ni rafiki.

Nne japo tunatumia juhudi katika kilimo,ufugaji,uvuvi,uchimbaji madini lakini mara zote yanakosekana maarifa.

Tano hatuchungi uzazi wa mpango,single mothers nao shida kubeba majukumu peke yake.

Mwisho tusikate tamaa.tunaweza kubadirika,it can be done play your part.
 
Elimu Elimu Elimu

Tukiweza Kulitatua hilo swala kwakuwa na Elimu Bora Nadhani Maendeleo Yatafuata
 
Hata kasumba ya dini inaleta umasikini. Mf. Ukipigwa shavu la kulia mgeuzie na la kulia. Maisha mazuri ni mbinguni hapa tunapita njia tu. Angalia Wachina hawana mda na maombi, wao ni kazi tu, mwafrika anakesha na maombi.
Mkuu muarabu ni mvivu na mfuata dini kuliko waafrika ila mbona hali ipo tofauti? Wewe unaona muafrika anakesha na maombi ila viongozi wa dini wanaona sasa jamii imekuwa busy na maisha ya kidunia zaidi hawapati hata muda wa kuabudu.
 
Mkuu hayo ni mambo ya kihistoria kutokana experience zetu za maisha ndio linalifanya uone kama wametuzidi akili, sidhani kama ukiwachukua watoto wa hayo mataifa kisha uje kuwalea na kukulia afrika kama utaona hizo akili.
Watanzania wenye asili ya Asia walioshikilia uchumi wenu wamekulia hapa hapa.
 
Wazungu baada ya kuathirika vilivyo na vita ya kwanza na pili ya dunia Wakarudi chini kabisa . Ujerumani ilirudi chini njaa kali uchumi mbovu hadi watu wakaanza kula mizoga ya farasi. Huko Uingereza Hali ilikuwa mbaya zaidi. Urusi na Japan ndo usiseme ukichukulia mfano wa binadamu mgonjwa sana tuseme walikuwa wamebaki mifupa tu. Miaka chini ya 20 baada ya vita waliibua chumi zao viwanda maelfu, vumbuz bora za kiteknolojia Leo so wenzetu tena.
Ila sisi baada ya miaka 60+ ya uhuru bado tunasingizia unyonyaji wa kizungu kama factor ya backwardness. Pole mimi pole Afrika
 
Back
Top Bottom