Kwanini Tangu waafrika tupate uhuru Hadi Sasa hakuna nchi Tajiri iliyofanikiwa

Hata wewe ukipewa nafasi utact the same ni asili ya waafrika wote
 
Hakuna kisingizio hapa.
Vyote vipo tele tu
 
South ni kati ya nchi tajiri duniani, nigeria ,algeria ,misri ni nchi zilizopiga hatua kubwa sana , au unazungumzia mafanikio ya mtu mmoja mmoja ?

Hata nchi kama angola ni nchi zilizovuna fedha nyingi ,shida tu ni viongozi wanaziangusha nchi zao walio wengi ,wanaruhusu mabeberu wazitumie nchi hizo kujinufaisha 70% alafu 30% ndio inabaki nchini
 
Hakuna nchi yoyote Wala kingozi wa namna hiyo. Umasikini wa akili na fikra na mtazamo huu ndio umasikini
 
Nini jukumu la wananchi wanaoibiwa wanashindwa nini kuwawajibisha wezi, mbona wananchi wa ulaya wanaweza kulinda raslimali zao
 
Sababu za kipumbavu hizi..... Vyote hivyo unavyovisema hawajashushiwa kama muujiza....waliumiza vichwa...kupasuka na kutatua matatizo yao....wangekaa kisubiri wawe navyo kama tunavyoamini kuwa hatuna....halafu tumekaa na kusema hatuna....nani atakuletea !


Sisi ni wavivu na tunataka shortcut.....ile lala maskini uamke utajiri huu hapa.... kuhangaika no.!
Tuna roho mbaya mno....anayejua hataki wengine wajue.....kuharibiana na kurudishana nyuma....kiufupi umimi ni mwingi kuliko usisi....yaani mtu anataka kuvimba na v8 sio sababu anaahitaji ila ili awakoshe maskini....yeye aonekane amepatia....
Niamini kuwa aliyemuuza mtumwa ni mwafrika na hata leo anayekwamisha Africa ni mwafrika.....labda niseme hivi aliyemuua mwendazake, sankara, ghadafi na wengineo na anayemtafuta traore ni mwafrika mwenzie kwa kitika alichopewa....(Roho mbaya na kutothaminiana) Uchu wa mali za kuilimbikia.....
Mwisho kabisa hapa Tanzania mpaka sasa tumeishaona system iliyopo imefeli na asilimia kubwa tunaona na kujua.....je nani na lini tutasimama maana kwa box tumeishaona haiwezekani .....je tuchukue mkondo upi kubadili system na sio lazima waingie wapinzani but system ibadilike viruses wauwawe.....je lini na nani nani tutasimama bila kwa wingi bila hofu ya kupotezwa....sio anatoka mmoja wawili ....kumi wakipotezwa huoni chochote kama vile damu yao si chochote.....!
 
Safi sana.

Kwahiyo, serikali wewe inakuzuia nini, kubuni kama huo uwezo unao???
Sisi ni wavivu na tunataka shortcut.....ile lala maskini uamke utajiri huu hapa.... kuhangaika no.!
Tuna roho mbaya mno....anayejua hataki wengine wajue.....kuharibiana na kurudishana nyuma....kiufupi umimi ni mwingi kuliko usisi....
Mambo ya ubunifu ni tofauti na utajiri.

Wabunifu wengimwa Ulaya na Marekani walikufa masikni.

Kwahiyo, tenganisha hoja yako kati ya umasikini na ubunifu.
yaani mtu anataka kuvimba na v8 sio sababu anaahitaji ila ili awakoshe maskini....yeye aonekane amepatia....
Kama hilo V8 kanunua kwa pesa yake hakuna shids.

Ila kama ni serikali ubunifu wa teknolojia hauwahusu
Kelele za biashara ya utimwa zilishapita.

Mida ulishapita, maisha lazima yaendelee
 
Hata wewe ukipewa nafasi utact the same ni asili ya waafrika wote
No ,usinisemee
Ht ktk hao wapo wazuri wachache ila mfumo unawapiga vita!

Kwani huoni ht maofisini aliye vzr anasimamia haki anaonekana mbaya?
Kwahiyo katikati ya hao Mungu anao wazuri tu wenye nia njema ila wanazidiwa na hao wengine
 
Jibu ni rahisi sana, mfano mzuri uko mbele ya macho yako angalia utawala wa serikali ya ccm na wote wanao waunga mkono ndio utapata jibu sahihi kwa nini afrika ni maskini na itaendelea kua maskini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…