Habari;
Kwasasa Dunia inafanya mapitio ya mitaala ya kufundshia/kujifunza huko mashuleni, huku swala la Elimu za Walimu ambao ndio wadau wa mitaala hiyo likiwa gizani, kwamfano, kwa Tz muundo wa kiutumishi wa Walimu wa shule za msingi na sekondari unaanzia Elimu ya cheti mwisho shahada ya kwanza tu, ambapo mwl akiwa na shahada ya Pili (masters/PhD) mfumo haumtambui kimasilahi (salary) na kimuundo, tofauti na nchi zingine Kama Kenya, south Africa, Nigeria, Zimbabwe na kwingineko,
Serikali ingelitazama hili swala kwa jicho la utatu kwa kuwaandalia muundo wa kiutumishi na kimasilahi Walimu wenye shahada ya Pili (Masters/PhD) waliopo huko mashuleni, ifikie kipindi Sasa iwe ni kawaida kumwona mwl mwenye PhD anafundsha shule za msingi huko, hii ishu italeta Mapinduzi makubwa sana kwenye idara ya Elimu na ualimu hasa huko mashuleni, tofauti na Sasa ambapo mwl akishapata shahada ya Pili tu huanza kuomba kuhamia idara zingine ambapo anaona atapata maslahi kulingana na Elimu aliyonayo wakati hyo elimu yake (masters/PhD) ingetambulika kimuundo na kimasilahi angetulia kituoni pake alipokuwa anafundsha bila kutafuta fursa mahala pengine.
NAOMBA KUWASILISHA