Kwanini TFF mnaipeleka fainali Zanzibar?

Kwanini TFF mnaipeleka fainali Zanzibar?

Acheni siasa mnaharibu soka letu mechi ya bara mnapeleka visiwani ili mgundue nini? TFF mnaipeleka Fainali Zanzibar, sehemu ya nje ya utawala wa FA husika?

Lini mmewahi kuona FA ya Uingereza imepeleka fainali Ireland, au Scotland?

Lini mmewahi kuona FA ya Ujerumani imepeleka fainali zao Uturuki?

TFF MJITATHMINI.
Bora kuliko uwanja wa mara swali fikirishi atakaye kosa pesa za kiingilio ni nani?
 
Si walisema inafanyika manyara sijui, niliangalia ule uwanja majuzi nilipita huko nikabaki nashangaa, mashabiki wengine watalazimika kusimama mwanzo mwisho wa game
Hii ndio sababu wamehamishia nchi jirani ya Zanzibar na hii ni baada ya wananchi wengi kulalamikia uwanja usiokidhi matarajio ya watazamaji wengi wa mpira.
 
TFF na Bodi ya Ligi wameonesha udhaifu mkubwa sana kwenye huu ubabaishaji wao. Na sijui wanafanya hivi ili kumkomesha/kumfurahisha nani!
 
Hata mimi nilishangaa. Timu za zanzibar hazipo kwenye haya mashindano 🤔
 
Acheni siasa mnaharibu soka letu mechi ya bara mnapeleka visiwani ili mgundue nini? TFF mnaipeleka Fainali Zanzibar, sehemu ya nje ya utawala wa FA husika?

Lini mmewahi kuona FA ya Uingereza imepeleka fainali Ireland, au Scotland?

Lini mmewahi kuona FA ya Ujerumani imepeleka fainali zao Uturuki?

TFF MJITATHMINI.
Vipi kuhusu Spain hakuna mechi zao wanazopeleka uarabuni?
 
Ni maamuzi mazuri tu kuwarudishia burudani wazenji wakawaone watoto wao kina Fei na Mudathir wakicheza fainali CRDB cup.

Ila Yanga hatutaki ukolokoloni wa Karai mechi ichezeshwe kwa haki, na kwa uwanja ule Azam watapigwa kama ngoma!!

Katika hili nawapa maua TFF, wamewaza vizuri, uwanja mzuri Yanga huwa hatufungwi never, boli inatembea. Sasa tuna uhakika wa kubeba hili kombe, wapi Pacome, Aucho, Muda, Ki na Max!!

Azam si ni wazenji wale? Ni vizuri tukiwapiga kwao na itapendeza zaidi kombe likirudi jangwani na chopa!!
 
Haya ndiyo madhara ya kuwaruhusu wanasiasa na makada wa chama tawala kuisimamia michezo. Shirikisho la mpira lingekuwa linasimamiwa na wataalamu wa mpira, ubabaishaji kama huu usingetokea.
Kuna mtaalamu wa mpira yupi kafanya zaidi ya karia ?maana wote walikuwa wezi mpaka fifa ikasitisha ruzuku ,wakati wanatawala watalamu wa mpira wakina rage ,ndolanga,malinzi tenga nk. wazamini walipatikana kwa kupigiwa magoti na walitoa milioni 100 kwa masharti magumu,wakati huo mpira ilionyeshwa mara moja moja kuliko harusi maana thamani ya mpira wadhamini hawakuiona ,leo mwanasiasa kafanya unamuona azizi,guede,chama na wengine wakigeni kumi wa kigeni unamdharau,vipi team za taifa zilifanya nini wakati wa utawala wa watu wa mpira?mishahara ya wachezaji ilikuwa vipi? Umeshasikia team iliyo ligi kuu au championship ikishindwa kusafiri kama wakati wa utawala wa watu wa mpira?vipi soka la vijana na wanawake mbona watu wa mpira walishindwa kabisa kusukuma mzigo huu uende mpaka mwanasiasa Karia akasema yeye ni mnyamwezi utaenda tu,KUNA KARIA mmoja tu sio mpaka mtu afe ndio sifa zimwagikie.
 
Wapumbavu sana hao jana taarifa ilipotoka nilishangaa sana... Wanaendeshwa na mihemko ya wanasiasa. Idiots
 
Acheni siasa mnaharibu soka letu mechi ya bara mnapeleka visiwani ili mgundue nini? TFF mnaipeleka Fainali Zanzibar, sehemu ya nje ya utawala wa FA husika?

Lini mmewahi kuona FA ya Uingereza imepeleka fainali Ireland, au Scotland?

Lini mmewahi kuona FA ya Ujerumani imepeleka fainali zao Uturuki?

TFF MJITATHMINI.

---

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza mabadiliko ya mchezo uwanja wa mchezo wa Fainali ya Kombe la FA kuwa kwa sasa utachezwa Amaan Zanzibar na sio Babati Manyara kama ilivyotangazwa awali.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya uwanja wa Babati kutokuwa sawa kwa baadhi ya miundombinu na usalama hivyo kupelekea mchezo huo kuhamishiwa Zanzibar.

Mchezo wa fainali ya FA utazikutanisha Yanga na Azam FC June 2, 2024 saa 2:15 usiku.
Kuna kitu cha kujifunza kwa muendelezo wa baadae huu utatumika km mfano
 
Back
Top Bottom