Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

Kwa sababu ukubwa wa madhara ya kuvunja sheria hizo ni yale yale bila kujali ukubwa wa engine.
Kwanini kusiwe na madaraja ya makosa barabarani na faini zake kama ilivyo kwa P.A.Y.E ukifanya kosa dogo ulipe faini kulingana na kosa husika kama ni dogo unalipa kidogo kama ni kubwa unalipa faini kubwa?...
 
Anayegongwa na Lorry na anayegongwa na Bajaj zote zikiwa katika speed sawa, ni nani yupo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha?

Bajaj na Lorry zikigongana na IST kwa speed sawa na nyakati tofauti impact zake zitafanana?
Mwenye Lorry alibeba mzigo akavuka redlight na akasababisha ajali , na mwenye bajaji aliyebeba abiria wa 5 akavuka redlight, kwenye bajaji wakafariki wote, kwenye Lorry akagongana na Lorry mwenzake na wakaumia tu, ni nani ana madhara zaidi kwenye makosa? Hivyo ukubwa waengine sio kigezo.
 
Kigezo ni nini sasa? Mbona kwa PAYE ukubwa wa mshahara ndio kigezo?
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na ukubwa wa engine ya chombo (CC-Cubic Centimetres) kama ambavyo kodi ya PAYE inavyoshabihiana na ukubwa wa mshahara wa mtumishi?

(1) Kwanini gari kama IST pamoja na Landcruiser V8 yote yakitenda kosa moja la usalama barabarani kama vile overspeeding wanalipa tozo inayofanana ya 30,000/=?

(2) Mbona mfanyakazi anayepokea mshahara basic wa 1,500,000/= pamoja na mwingine anayepokea 300,000/= wanalipa viwango tofauti vya kodi ya PAYE?

(3) Katika kuvuka daraja la Mwalimu Nyerere pale Kigamboni wanalipa kulingana na ukubwa wa gari na kwanini hakuna tozo za kufanana?

(4) Kwanini kusiwe na madaraja ya makosa barabarani na faini zake kama ilivyo kwa P.A.Y.E ukifanya kosa dogo ulipe faini kulingana na kosa husika kama ni dogo unalipa kidogo kama ni kubwa unalipa faini kubwa?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kaka kajipange upya. Mada kimeo
 
Kaka kajipange upya. Mada kimeo
Sawa kaka. Lakini kwanini fine/tozo ni flat rate mkuu?

Kwanini kusiwe na madaraja ya makosa barabarani na faini zake kama ilivyo kwa P.A.Y.E ukifanya kosa dogo ulipe faini kulingana na kosa husika kama ni dogo unalipa kidogo kama ni kubwa unalipa faini kubwa?
 
Kwanini kusiwe na madaraja ya makosa barabarani na faini zake kama ilivyo kwa P.A.Y.E ukifanya kosa dogo ulipe faini kulingana na kosa husika kama ni dogo unalipa kidogo kama ni kubwa unalipa faini kubwa?...
Hoja yako (kwenye heading) ilikuwa ni ukubwa wa engine , na ndio hoja niliyojibu. Hilo la ukubwa wa kosa itaymiza tu madereva, maana kosa la chini kabisa litakuwa 30,000/= hii hii, halafu mengine ndii wataangalia waongeze kiasi gani juu ya hiyo 30k, hivyo naona wasuongeza maana itaumiza madereva kwa kutozwa tozo zaidi ya 30k
 
Madhara yanatofautiana sana mkuu. Kama wewe unaendesha Bajaj kisha ukagongwa na IST impact haiwezi kuwa kubwa kama ukigongwa na Scania
Lakini si kweli pia kwamba bajaji aliyebeba abiria akavuka redlight na akagonga na lory ataua watu wengi zaidi ya Lorry la mchanga likivuka redlight na akagongwa na Lorry ambapo mafereva wote wanauwezekano mkubwa wa kupona? Kwahiyo ukubwa wa engibe sio kigezo consistent na hakiqualify kuwa base of reference
 
Kigezo ni nini sasa? Mbona kwa PAYE ukubwa wa mshahara ndio kigezo?
You earn more you paymore, benefits/faida za mshahara mkubwa zinamaanisha kwamba unauwezo wa kuchangia zaidi ya yule mwenye kipato kidogo, point ni kukusanya mapato, hiyo ni tozo na sio faini. Kwenye faini lengo si kukusanya mapato bali ni kuzuia ajali, sasa unless uniambie kwamba engine ikiwa kubwa zaidi then madhara ya ajali yanakua consistently makubwa zaidi ya engine ndogo then hoja yako inaweza ikawa na mantiki, otjerwise ni upuuzi tu
 
Mbona hamna Relation hapo....jaribu tena kufikiria mfano
Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika kama ambavyo kodi ya PAYE inavyoshabihiana na ukubwa wa mshahara?
 
Mmh nini sasa, daladala akavuka redlight na akaua watu 20 baada ya kugongwa na lorry ni sawa na mwenye semi la mahindi akavuka na kisha akagongwa na lorry hilo hilo na asife mtu?
Kuna jamaa mmoja humu amenipa ufafanuzi mzuri sana kwa kusema ya kuwa "fines" sio za magari bali ni za dereva
 
Kuna jamaa mmoja humu amenipa ufafanuzi mzuri sana kwa kusema ya kuwa "fines" sio za magari bali ni za dereva
Kwamba gari huwa halipigwi faini? Kuna makosa ya gari na makosa ya dereva , yote hutozwa faini, kama huamini, mwambie mtu akuazime gari lisilo na taa , na wewe dereva usifanye kosa lolote uone kama hukamatwi
 
Gari likikosa taa ni kosa la dereva mkuu. Kwanini ameshindwa kuweka taa katika gari lake?
 
Back
Top Bottom