Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

Gari likokisa taa ni kosa la dereva mkuu. Kwanini ameshindwa kuweka taa katika gari lake?
Gari la muajiri wako, sio lako, wewe dereva unalipwa laki 3 mfano, na mwahiri wako kakupa V8 ambayo taa moja inauzwa milioni 2, sasa wewe dereva ukanunue taa? Hilo si kosa la dereva, ni kosa la gari, na mmiliki ndie hubeba huo mzigo. Narudia, barabarani kuna makosa ya dereva na makosa ya gari; na yote huoigwa faini.
 
Kwanini dereva anakubali kuendesha gari mbovu ambayo haina taa?
 
You earn more you paymore, benefits/faida za mshahara mkubwa zinamaanisha kwamba unauwezo wa kuchangia zaidi ya yule mwenye kipato kidogo, point ni kukusanya mapato, hiyo ni tozo na sio faini. Kwenye faini lengo si kukusanya mapato bali ni kuzuia ajali, sasa unless uniambie kwamba engine ikiwa kubwa zaidi then madhara ya ajali yanakua consistently makubwa zaidi ya engine ndogo then hoja yako inaweza ikawa na mantiki, otjerwise ni upuuzi tu
Okay
 
Safi sana. Jibu la kifilosofia.
Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika kama ambavyo kodi ya PAYE inavyoshabihiana na ukubwa wa mshahara?
 
Kwanini dereva anakubali kuendesha gari mbovu ambayo haina taa?
Yeye ni vehicle inspector? Maana hata tairi likiisha tarehe zake za kufanya kazi ni kosa la gari, sasa kuna dereva atakayeweza kukagua hadi tarehe za tairi among a tonne of other things, kwa kila gari? Ni jukumu la mwenye gari kupeleka kwa wataalam wakague regularly, sio kazi ya dereva, taa ilikuwa ni mfano tu, ila kuna vitu vingi sana; mfano taa ya indicator inaweza ikaungua na dereva asijue hata wiki, ila akikaguliwa na traffic gari linapigwa faini si dereva
 
Makosa uzito wake unapimwaje?!
Na hukumu inapimwaje ili ilingane uzito, ukubwa, ujazo, urefu, umbali au ufupi wa kosa.

Hivi vitu havipimiki hivyo havina standard yoyote kuvipa usahihi.
 
Makosa uzito wake unapimwaje?!
Na hukumu inapimwaje ili ilingane uzito, ukubwa, ujazo, urefu, umbali au ufupi wa kosa.
If that's the case, kwanini murder na manslaughter zina adhabu mbili tofauti?...
 
Yeye ni vehicle inspector? Maana hata tairi likiisha tarehe zake za kufanya kazi ni kosa la gari, sasa kuna dereva atakayeweza kukagua hadi tarehe za tairi among a tonne of other things, kwa kila gari? Ni jukumu la mwenye gari kupeleka kwa wataalam wakague regularly, sio kazi ya dereva, taa ilikuwa ni mfano tu, ila kuna vitu vingi sana;
Ndio yeye ni vehicle inspector wa kwanza hata kabla hayawasha engine ya gari...
 
Ndio yeye ni vehicle inspector wa kwanza hata kabla hayawasha engine ya gari...
Dereva hana taaluma ya 'motor vehicle inspector', hiyo ni kazi ya mtaalam, Dereva ana limits zake, atakagua oil, maji na vitu vidogo vidogo, so haliwezi kuwa kosa lake, ni kosa la gari, na mzigo atabeba mwenye gari
 
Kama kosa ni la gari, kwanini askari wa usalama barabarani anaandika number ya gari pamoja na number ya leseni ya dereva katika ile mobile machine yake?
 
Kama kosa ni la gari, kwanini askari wa usalama barabarani anaandika number ya gari pamoja na number ya leseni ya dereva katika ile mobile machine yake?
Ili kuweka records sahihi, maana madereva wengine huiba magari yard na kwemda kupiga day worker bila kumtaarifu bosi, hivyo lazima tujue aliyekuwa anaendesha
 
Sawa mkuu. Sasa mkuu waliwezaje kupima uzito na kujua kuwa fine inapaswa kuwa 30,000/= kwa kila kosa na sio 20,000/=?
Hapo nadhani hakuna mzani ndio maana iko Flat rate ya 30000; Inawezekana wameangalia uwezo rafiki wa wamiliki magari wengi wastani ukaangukia hapo (sina hakika kigezo gani walitumia, inawezekana waliamua tu)
Yaani Kosa halijapimwa, ndio maana fine yake ni moja; Kosa likiwekwa kwenye mizania basi nadhani hapo fine zitaanza kutofautiana. Fine haiitaji kupimwa, maana inategemea zaidi Kosa lililopimwa ili fine yenyewe iwe Applied.
 
Back
Top Bottom