Bora hata hao wasiofunga hesabu lakini wameandika kiasi. Kuna hospitali ya meno nilienda Magomeni wao hawajaandika chochote zaidi ya kutaka nisaini tu.
Nilipokataa akaja daktari mkuu (mwenye hospitali) akajifanya kumuwakia aliyekuwa reception lakini wazi inaonekana ndio mchezo wao.
Kuna TMJ polyclinic iliyopo chang'ombe, wao wana kawaida ya kutuma msg baada ya siku 2 ya kwenda hospitali kuonyesha matibabu yako yaligharimu kiasi gani. Nilikwenda nikacheki malaria tu na kuonekana sina na sikupewa hata paracetamol, baada ya siku 2 msg imekuja matibabu yaligharimu 170,000.
NHIF ni wapigaji lakini wamiliki wa hospital wapigaji zaidi.