Kwanini tukienda hospitali zile fomu za NHIF hawafungi hesabu pale chini?

Kwanini tukienda hospitali zile fomu za NHIF hawafungi hesabu pale chini?

Punguzeni lawama wizi dhuluma duniani haiwezi kuisha ukiwa mjinga bwege lazima uibiwe na wajanja hata serikali nyingi za kiafrica zinaibiwa hadi leo hiyo ni formula ya maisha ukishatibiwa nenda nyumbani ili mradi upate matibabu mazuri
 
Wapo na kazi nyingi halafu ni wachache, wanatunza Ili wikiendi wafunge hesabu.
Benki ukikuta kuna tallers wachache wanakuambia saini hapa halafu mengine watajaza wenyewe jioni?
 
Je hawezi kuongeza kitu ambacho sikufanya
Mimi huwa wakiniambia saini hapa kwanza naanza na kufunga pale dawa zilipoishia mpaka mwisho, siachi nafasi yoyote ya wao kuandika kitu kipya. Ila najua huwa wanachukia sanaa na huwa hawanipendi [emoji23] [emoji23]
 
Ni kweli kabisa. Hili tatizo lipo. Kabla ya kusaini inabidi mstari wa kufunga uwekwe halafu nisaini. Kama NHIF mnashirikiana katika Hili, naomba Serikali iingilie kati si kubaki mnalalamika tu kwamba matumizi yamekuwa mkubwa wakati mnaacha mianya ya wizi ikiendelea.

Nssf zamani walikuwa wanafunga, baadaye wakaacha. Kama wanachama tunaomba Hili litazamwe upya.
Funga mwenyewe kama unavyofunga karatasi za Benki mkuu...
 
Sio kila daktari anayekuona anajua bei ya dawa/huduma aliyokupa zilizoko kwenye mfumo wa NHIF
Hospital nyingine tayari wameunganishwa online ukisaini maana yake na gharama zimepigwa papo hapo automatic

Sasa ukija kwenye hizi hospital zetu za Serikali bado changamoto ni kubwa ya watendaji kwa upande wa bima, mtu anayeingiza madai kwenye mfumo unakuta ni mmoja anazikusanya anaingiza mara moja moja sana.

Ila yote kwa yote NHIF hawajui majukumu yao ukija kwa ngazi ya vituo vya kutolea huduma wako ofisini kusubiri waletewe madai mwisho wa mwezi wakati watendaji huku chini wa bima hakuna na hata ku-organize mambo na kituo ili hizi changamoto zitatulike.
This is not an excuse, ni loop hole ya upigaji..
 
Anaweza na wanafanya sana. Kinachotokea mtu akija kutibiwa cash pesa inatiwa mfukoni na charges zinahamishiwa kwenye form yako iliyoachwa blank.
Exactly, mimi huwa lazima nifunge mwenyewe, nachora ile alama kama Z kuanzia dawa ya mwisho mpaka chini then ndiyo nasaini.
 
Hapo utaambiwa anaefunga hesabu ni mhasibu.
Nchi hii sababu tunazo tena za msingi
 
Wanaongeza bill ukitoka kwa nini hesabu hazifungwi ukiwepo na ukiwaambia fungeni hesabu huwa hawapendi lakini mimi nishazoea kuwaambia..
 
Back
Top Bottom