Kwanini tukienda hospitali zile fomu za NHIF hawafungi hesabu pale chini?

Punguzeni lawama wizi dhuluma duniani haiwezi kuisha ukiwa mjinga bwege lazima uibiwe na wajanja hata serikali nyingi za kiafrica zinaibiwa hadi leo hiyo ni formula ya maisha ukishatibiwa nenda nyumbani ili mradi upate matibabu mazuri
 
Wapo na kazi nyingi halafu ni wachache, wanatunza Ili wikiendi wafunge hesabu.
Benki ukikuta kuna tallers wachache wanakuambia saini hapa halafu mengine watajaza wenyewe jioni?
 
Je hawezi kuongeza kitu ambacho sikufanya
Mimi huwa wakiniambia saini hapa kwanza naanza na kufunga pale dawa zilipoishia mpaka mwisho, siachi nafasi yoyote ya wao kuandika kitu kipya. Ila najua huwa wanachukia sanaa na huwa hawanipendi [emoji23] [emoji23]
 
Funga mwenyewe kama unavyofunga karatasi za Benki mkuu...
 
This is not an excuse, ni loop hole ya upigaji..
 
Anaweza na wanafanya sana. Kinachotokea mtu akija kutibiwa cash pesa inatiwa mfukoni na charges zinahamishiwa kwenye form yako iliyoachwa blank.
Exactly, mimi huwa lazima nifunge mwenyewe, nachora ile alama kama Z kuanzia dawa ya mwisho mpaka chini then ndiyo nasaini.
 
Hapo utaambiwa anaefunga hesabu ni mhasibu.
Nchi hii sababu tunazo tena za msingi
 
Wanaongeza bill ukitoka kwa nini hesabu hazifungwi ukiwepo na ukiwaambia fungeni hesabu huwa hawapendi lakini mimi nishazoea kuwaambia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…