Uchaguzi 2020 Kwanini Tundu Lissu anatumia muda mwingi kutafsiri Katiba na Sheria badala ya kutangaza sera?

Kwendraaaa
 
Yaani Leo katoa Pasi ya ovyo kabisa katika harakati zake za kujijenga kimaslahi. Sijui kama mnaona ninachokiona kwa Lissu. Au ndiyo mmeamua kuvaa miwani ya 'mabao'? Ebu vueni miwani hiyo!
Kwa sababu wewe ni kilaza huwezi kumuelewa Lissu!!! Umekaririshwa juu ya ukoloni kwa iyo ukisikia ukoloni unawaza ulivyokaririshwa!!

Lissu anaongelea kuweka mamlaka ya matumizi ya pesa na mgawanyo wake kwa wananchi kwamba, wananchi wasiwe ombaomba kwa kiongozi mkuu ila wao ndo waweke vipaumbele kwa miradi wanayotaka iwe miradi ya maji, elimu au miundombinu.

Hivi ndo ilivyokuwa kipindi cha mkoloni Ndo mana vyama vya ushirika vya wananchi enzi za mkoloni vilijenga shule na miradi mbalimbali kwa sababu sio gavana aliyekuwa anawaamulia matumizi ya pesa zao.

Baada ya Uhuru Nyerere alibadilisha sheria ya fedha kuweka hela zote chini ya Raisi, Ndo mana leo miradi yote hela lazima ziishinishwe na Raisi.

Ndo mana hadi leo watanzania wamekuwa ombaomba kwa serikali na Raisi , kila sehemu wanalia, Raisi tujengee shule, tuletee Maji, sijui tujengee barabara. Shida ni mfumo uliowekwa baada ya Uhuru kuweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.
 
Kwendraaaa
 
...tuna fundishwa...
Mkuu kumbe na huku unafika....Ha ha haa! Najua kwenye jukwaa hili tunaweza tusiwe njia moja...ndiyo Raha ya Jamiiforums.com. Kila la heri, mkuu. Ila Tanzania kwanza mengine baadaye. Tuna Tanzania moja tu ! Tuilinde.
 
Tatizo lime anzia hapo
 
Mkuu kumbe na huku unafika....Ha ha haa! Najua kwenye jukwaa hili tunaweza tusiwe njia moja...ndiyo Raha ya Jamiiforums.com. Kila la heri, mkuu. Ila Tanzania kwanza mengine baadaye. Tuna Tanzania moja tu ! Tuilinde.
Pamoja mkuu 🙏 haki uhuru na maendeleo
 
Sas alichotafusiri wew ulikuwa unakijua? Kampeni ni pamoja na kutoa elimu ya uraia. Kwa nchi kama zetu elinu ya mpiga kura iko chini sana. Kuna waliofaidika na elimu hiyo. Nchi kama US mtoto wa primary school anajua katiba ya nchi yao maake huwa aina vilaka za kwetu. Sisi uku mtu ana masters hajui katiba na sheria za nchi yetu. Shukuru umepata hiyo elimu vinginevyo unaitaji miaka 3 ya LLB kujua alichoeleza.
 
Kama Kuna MTU Alikudanganya Akakwambia Chadema Imekufa, Nikuambie Sasa Mimi Nimeshuhudia Chadema Iko Mioyoni Mwa Watu, Aseee.

Kwa taarifa yake huyo mpuuzi aliyetoa kauli hiyo ya kidwanzi, ataanza kufa yeye na Chadema ataiacha ikizidi kustawi.
 
Kipi Cha ajabu hujui kuwa kipindi Cha ukoloni tanganyika ilikuwa na majimbo matano ambazo ndio tunayaita Kanda kwa Sasa,,tofauti ni kwamba Kanda baada ya uhuru tulizinyanganya mamlaka na kupeleke kwa mikoa Jambo ambalo limeongeza mzigo kwa serikali.
 
Kwasababu sera kuu Ni Katiba mpya, umeridhika na Jibu?
 
Kwa sababu Katiba ambayo ndiyo msaafu wa nchi umenajisiwa na Magufuli kuliko wakati wowote wa utawala wa nchi yetu.
 
Kabisa anaongea huu ujinga wengine mnashangilia..Sasa umuhimu wa
Amiri jeshi mkuu Ni Nini na maeneo yasiyokua na rasilimali yatapataje maendeleo....huyu jAMAA mlamba miguu ya wazungu mpumbavu sana
 
Simple answer, miaka mitano magufuli amekuwa akivunja Katiba na sheria, therefore sensible candidate lazima agusie sheria katika kila anachokiongea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…